urithi atapata mzee akifa, sio sasaivi msimsumbue. binafsi mabinti zangu nikija kuwa mzee mstaafu kama nawapa nyumba au zawadi yeyote nitahakikisha nimeandika na jina lake binafsi kwenye nyaraka, la mwanaume wake sitahitaji hata kulisikia, yeye kama ni mwanaume akatafute huko, na hawatajua kama niliwapa hadi siku nikiwa nimeenda mbinguni. kuna mzee moja actually yeye ana pesa nyingi, alimwita kijana wake mwaka jana kama anamfanyia sapraizi ivi, dogo akajikuta anaonyeshwa bonge la lodge/guest house mkoa fulani hivi, dingi kamwambia hii ya kwako hangaika nayo. huyo nii mwanaume, ila angekuwa mwanamke kama ni mimi namwambia tu awe mlinzi bila yeye kujua kama kwenye nyaraka nimemwandika yeye. sitaki mali zangu aje ale mwanaume wa binti yangu, ajibembeleze kwake sio awe sharobaro anayelelewa na pesa zangu.