Baba mtoto kanitelekeza

Baba mtoto kanitelekeza

Mbona mnatutisha sasa, miaka 32 bado mnasumbuka na mapenzi [emoji848][emoji848]
Mapenzi hayana ushujaa mkuu hata kama umestaafu unaweza ukatoa machozi kwa kitoto cha form 1 ruge na ujanja wake wote ila alitoa machozi kwa zamaradi bila aibu.
 
Ni kweli lakini mnachoshangaza, ukiona huyu akufai, unamganda ili iweje? Why wasting ur time? Ama unakua na watatu, wote pia Wana shida?
Ni kweli sometimes ni mazoea tu ,kuchepuka kupo lakini kila mtu ana mtu wake wa kudumu, huyo ni baba mtoto haitoi wako hiyo historia haifutiki na kuna bond tayari kati yenu ambaye ndo huyo mtoto haikwepeki, sometimes ni vizuri kukaa chini na siyo kiburi, ila kama mlikutana type kila mtu ni kiburi kazi ipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mara nyingi mwanamke atabadilika kutokana na vile unavyomlazimisha awe. Atakuheshimu kama utamuheshimu. Atakujali kama utampenda. Ukifanya tofauti, tutakulipa mara mbili yake. Kwa hiyo Kwa sasa sina hisia zozote kwake. Ingawa ameshaomba radhi mara kadhaa. Ila sioni haja ya uwepo wake kwangu.
Bora basi angekua na mmoja anayemuheshimu na kumjali, wote kilio Ni kimoja. Amelazimishwa kuoa hadi wamemchoka kwao. Ndugu zake wamejikatia tamaa. Kuna muda anadaiwa pombe hadi wanamfata kwa wazaz wake. Ni kama karogwa au kachanganyikiwa.
 
Mapenzi hayana ushujaa mkuu hata kama umestaafu unaweza ukatoa machozi kwa kitoto cha form 1 ruge na ujanja wake wote ila alitoa machozi kwa zamaradi bila aibu.
Kwakweli nimeanza kuamini mapenzi hayana umri
 
pole sana dada na hongera kwa msimamo huo, ila jamaa kama hajiamini hivi kama ndo amekupa katoto? au ni mawazo yangu tu? .baadae jiandae kwani atakusumbua kuhusu kudai mtoto.
Ana uhakika ila ni muoga sana wa maisha. Ni kawaida yake kuwapa wanawake zake dawa za kuua watoto Kwa kisingizio kuwa hana maisha. Aliwahi kuwa na mtoto mmoja ambaye hajui ada wala chakula. Kiufupi ni mtu asiyependa majukumu. Yeye anachojua ni pombe.
 
Sasa kwa nini ulijiingiza kwenye maisha ya mtu disign hii
 
Habarini?

Ninaomba nieleweke kwamba mimi si mgeni, nimekua nikisoma mijadala mbalimbali lakini leo nami nimewiwa nilete kisa changu ambacho ninaamini kwa namna moja au nyingine kitawasaidia watu kadhaa.

Mimi mwanamke wa miaka 32, nimeajiriwa mahala Fulani. Kiukweli, nilikua kwenye mahusiano Kwa muda mrefu sana tangu nikiwa chuo hadi hivi majuzi. Hali ya mahusiano yetu yalikua ya kusuasua mno. Leo mko poa, kesho majanga hali ambavyo ilinikatisha tamaa sana. Ingawa jamaa alinitamkia ndoa wakati Fulani lakini binafsi kwa tabia za jamaa, sikuona hata kivuli endapo tungefunga ndoa.

Mwenzangu kwanza ni mnywaji sana wa pombe kiasi kwamba mara kadhaa ilimletea shida kwenye ajira yake na alisimamishwa mara nyingi sana. Mbali na hiyo, ni mtu ambaye bado hajui anataka nini. Leo mtapanga hiki, kesho mtagombana muanze upya so mnakua mara kadhaa hakuna mtakachokamilisha.

Mara nyingine anadai anataka kuoa mtu wa kabila lake, mara anaweza kuanzisha mahusiano na vitoto vya chuo ingawa yeye ana 36 years.

Kwa mahusiano yetu ya miaka Zaidi ya nane, hatukuwai kujaliwa mtoto ingawa jamaa alinitamkia mara moja akisema ananiacha sababu simpi mtoto then baadaye akaomba msamaha na maisha yakaendelea.

Mungu si Athuman! Mwezi wa tano nilijigundua ni mjamzito. Nikamshirikisha mwenzangu ambaye hakuwa na furaha nayo kabisa. Akanishauri sana tutoe tukizingatia bado tunajitafuta and blablabla.

Kiukweli mimi nilifurahi mno nilipojigundua ni mjamzito. Hata wazo la kutoa sikua nalo kichwani. Niliamua moyoni hata kama jamaa ataamua kuondoka lakini priority ya kwanza ni mtoto wangu.

Kweli, jamaa alihangaika sana kunishawishi kutoa ili tuendeleze mahusiano (ambayo hayana dura) nikaamua kuweka msimamo wangu kwamba akijisikia kuondoka, aondoke ila mtoto kama lolote likitokea basi liwe limepangwa na Mungu ila sipo yeye. Aliamua kuondoka na wala sikujushughulisha naye kabisa.

Ninamshukuru sana Mungu kwa kunisaidia safari yangu ya ujauzito hadi sasa, hakuna kilichonisumbua. Kiukweli, nina furaha na amani zote, sielewi ni kwa nini. Nimejikuta natamani kuwaambia wanawake wenzangu, wasikubali kuendeshwa na wanaume wa namna hii ili kuendeleza mahusiano.

Focus na unachokichagua kwani hata ningetoa, sio kweli kwamba mahusiano yangeboreka, tena yangekua mabaya zaidi. Ninamshukuru sana na niwatakie jioni njema.
Mkiambiwa msimvulie mtu chupi mpaka muoane kihalali hamtaki.

Umelikoroga ulinywe sasa. Unafikiri utasaidiwa nini kwenye mitandao ya kijamii?

Nenda ustawi wa jamii.
 
Mmhh!
There must be something wrong on your side. Mmeishi miaka minane bila kupata mtoto, sasa hivi umepata ujauzito halafu ghafla tu mwanaume akuambie kwamba utoe ujauzito na kisha baadaye akukimbie eti kwa sababu hutaki kutoa ujauzito??!!!? Is it possible under normal circumstances? Nina mashaka makubwa sana juu ya maelezo yako, utakuwa umetificha mambo Fulani Fulani ili tusijue.
 
Mmhh!
There must be something wrong on your side. Mmeishi miaka minane bila kupata mtoto, sasa hivi umepata ujauzito halafu ghafla tu mwanaume akuambie kwamba utoe ujauzito na kisha baadaye akukimbie eti kwa sababu hutaki kutoa ujauzito??!!!? Is it possible under normal circumstances? Nina mashaka makubwa sana juu ya maelezo yako, utakuwa umetificha mambo Fulani Fulani ili tusiju
 
Mmhh!
There must be something wrong on your side. Mmeishi miaka minane bila kupata mtoto, sasa hivi umepata ujauzito halafu ghafla tu mwanaume akuambie kwamba utoe ujauzito na kisha baadaye akukimbie eti kwa sababu hutaki kutoa ujauzito??!!!? Is it possible under normal circumstances? Nina mashaka makubwa sana juu ya maelezo yako, utakuwa umetificha mambo Fulani Fulani ili tusijue.
I wish ungefahamu wanaume wa aina hii wasiojua nini wanahitaji kwenye maisha yao.
Unaweza ukaamini chochote ila ujue tunatumia majina fake, hatuna haja ya kuficha kama mtu anaamua kusema yaliyomsibu.
 
Kuna vitu 3 nimevipata kwenye mada yako ambavyo vinasumbua sana waafrika na kuwafanya kuendelea kuwa maskini.

(a) Jamaa ana 36 mke ana 32 lkn bado wanajitafuta. Mpk mkajipate mngefikisha miaka 50. Hii ndiyo Afrika. Halafu utasikia kuna kuku anaongea eti life begins at 40.

2. Kigugumizi ulichokuwa nacho kwenye kufanya maamuzi ya kumuacha mlevi asiyejielewa na anayedanga na videnti vya chuo kimekuponza.

3. Kupata mtoto ni jambo jema. Lkn tuzingatie misingi na kanuni za kupata mtoto kutoka kwenye mbegu bora (mtu mwenye sifa bora). Hivi mwanao akija kuwa mlevi na asiye na msaada kwako utalalamika? Maana mtoto wako katoka kwa baba mlevi, mzinzi na asiye na msimamo na maisha. Mtoto akiwa na tabia hizo utalaumu??
 
Back
Top Bottom