Baba " mwanangu upo tayari taratibu za ndoa ziendelee'' @Etugrul bey" ndio baba''

Ww jamaa unaleta uongo sasa, kama tabia ndo inaleta upendo mbona mkeo alikua na tabia njema kwa mujibu wako na bado ukamuacha na kuchepuka na mtu unaehisi ana tabia mbovu.
Basi akili yako ina shida mahala.
 
Mkuu sio kwamba nakupinga saana ulichofanya uko sahihi kwa upande wako, ila naamini alistahili zawadi bora kuliko hicho ulichofanya.

Kwa upendo aliokuonesha, ulipaswa kumuonesha upendo zaidi. Wanaume tunaweza ishi na mwanamke anaetupenda kwa dhati,bila shaka hilo linawezekana.

Umempa donda lisiloponeka kirahisi.
 
Una umri gani kwanza
 
Siku nyingine Jifunze kutiisha hisia na matamanio yako.

Ningekuwa wewe ningebaki na huyo mke uliyedumu naye miaka 7.

Siwezi Acha mwanamke mzuri mwenye nidhamu,mke mwema kisa matamanio na hisia za moyo wangu.
Labda huyo Dada Hakuwa Mzuri wa maumbile.

Sifa ya mwanamke ili awe Mke wangu,
1. Lazima awe msikivu na mtiifu kwangu.
2. Lazima Ajue wajibu wake kama Mke ndani ya nyumba.
3. Awe msafi hapa namaanisha Asiwe Malaya.

Huyo Dada umemuonea tuu,

"Moyo ni mdanganyifu na unaugonjwa wa kufisha ni Nani awezaye kuujua?"
 

Jamaa kaniskitisha Mno.

Huyo Dada Kwa Karne hii kumpata ufanye kazi, sio ajabu hapa Dar wasizidi 100 wanawake WA namna hiyo.

Jamaa kafuata matamanio na hisia zake na kuuza Future Bora ya kizazi chake.
 
Jamaa kaniskitisha Mno.

Huyo Dada Kwa Karne hii kumpata ufanye kazi, sio ajabu hapa Dar wasizidi 100 wanawake WA namna hiyo.

Jamaa kafuata matamanio na hisia zake na kuuza Future Bora ya kizazi chake.
Ndio maana nikamwambia asijiite ertugrul bey... Katumia hisia zaidi kwenye mahitaji ya akili.

Huwa naamini wanaume tumapaswa kutumia akili kuliko hisia.
 
Sasa kama swala ni tabia mbona unatuaminisha kwamba hata huyo dada wa watu alikuwa na tabia njema?
Ni sahihi kabisa kuhusu Tabia wote Mashallah wamejaaliwa.....lkn hivi vitu vinaenda pamoja....kwamaana Tabia na mvuto wa mtu husika au ndio kupenda huko....siamini Nakadori kama wewe binafsi unaweza kuwa na mtu ktk mahusiano kwasababu Tu ana Tabia nzuri? Lazima utavutiwa nae Kwa mwonekano wake....

Na UZURI WA mtu upo Kwa Yule anayependa....na hapa hatuangalii zile sifa kubwa za kidunia sijui mshepu mkubwa au kalio kubwa na mambo kama hayo....muhimu ni nini kile kinakuvutia Kwa mpenzi wako....baada ya hapo sasa ndo unacheki je na Tabia unaipenda?

Lakini lazima kuwe na mvuto Kwanza.
 
Kama ni tatizo la kisaikolojia litaendelea kujitokeza hata huko mbeleni, fikiria kujitafutia tiba ya kisaikolojia kuliko kufikiria kutoka taraka. Agano la ndoa ni kubwa sana, ukiamua kuingia fanya kila linalowezekana kubakia, oa acha oa tena sio mtindo wa maisha wa mtu mstaarabu kama wewe shekhe, hilo ni kuwaachia wanyama na binadam wa aina hiyo, changamoto za ndoa ni nyingi hiyo yako ikiwa mojawapo, kila linalowezekana kufanyika lazima lifanyike ndoa iwe salama na hakuna lisilowezekana chini ya jua.
 
Mkuu umenena vizuri Sana lazima kuwe na uwiano WA hisia,mitazamo na Tabia kinyume cha hapo hakuna mapenzi.

Unajua kuna udhaifu kama labda kisirani,au kiburi na kadhalika waeza kuvumulia....na utaweza kuvumilia Tu kama Una mapenzi ya dhati Kwa mwenza wako.....lkn kama huna hisia juu yake ni vigumu kuwa nae na hata kuvumilia madhaifu mengine
 
Na ni tatizo kubwa ambalo litaikumba jamii Kwa sasa.....chukulia wewe unaogopa kupenda asilimia 100 na huyo utakaye muoa naye ataogopa kukupenda asilimia 100.....ina maana upendo utakuwa hakuna katika familia coz kila mtu ataona mwenzie hampendi...je mwisho wa siku inakuwaje?

Binafsi nashauri penda kama hujawahi uumizwa kabla....kwasababu kwanini uhukumu kosa la mwingine na apate shida mwingine? Unajua kuna msemo mmoja unasema hivi '' kabla ya kukutana na malkia basi lazima Kwanza utakutana na chura'' huenda hao uliokutana nao huko na kukumiza au kukufanya usitamani kupenda tena...walikuwa vyura....je inakuwaje kama huyo sasa ndiyo malkia wako?
 
Hii ishu kuwa wengi hasa wanaume tunapitia, watakaokushangaa bado hawapo kwenye mahusiano, mdada mwingine mmesex mara mbili anakushikia mimba,anaanza kufosi ndoa.
 
Ww jamaa unaleta uongo sasa, kama tabia ndo inaleta upendo mbona mkeo alikua na tabia njema kwa mujibu wako na bado ukamuacha na kuchepuka na mtu unaehisi ana tabia mbovu.
Basi akili yako ina shida mahala.
Mkuu....labda nikuulize pale unapokutana na mwanamke Tu je unavutiwa na Tabia Kwanza au mwonekano wake? Naamini utampenda Kwanza jinsi alivyo then ndo utakuja ktk Tabia sasa.....kama ana Tabia mbaya ndo utaona hakufai kama nzuri utakuwa nae au sio.....kwahiyo lazima uvutiwe nae Kwanza! Sijui kama tunaelewana mkuu?
 
Kuwa na Amani Tu mkuu ni sehemu ya mjadala.....eti mkuu unaweza kuwa na mwanamke yeyote Tu Yule maadam ana Tabia nzuri? Nakuulizo hivyo Nina maana yangu mkuu kuwa mkweli na jibu lako
 
Mkuu huyo mdada ana shepu la maana Tu....ukitembea nae unajua hapa Nina mwanamke...lkn mwisho wa siku shepu yake hainipi ridhiko la moyo wangu......

Mkuu huwa sibabaishwi na matamanio linapokuja swala la kuchagua mwanamke WA kuishi nae....huwa naangalia Tabia za msingi Sana lkn bila kusahau mvuto Kwa mwanamke husika....na mvuto sio shepu kubwa au rangi au UZURI...ni vile ukimuangalia unajisikia Raha,we hujawahi kuona mtu anampenda mwanamke kimbau mbau kama mstimu wa nguzo ya umeme? Kuna kitu ambacho anavutiwa nacho...huenda ni Sura au umbile lile kipotabo ndo ugonjwa wake......kwahiyo hata Mimi Nina uchaguzi wangu na utashi wangu jamani....πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ naomba mniache Tu jamani
 
Hivyo ndivyo ilivyo lakini wewe hiyo comment niliyoquote umeandika kua unapenda zaidi tabia kuliko umbo/sura ya mwanamke.

Sasa ndo hapo penye walakin, ikiwa unapenda ziaid tabia na mkeo alikua na tabia njema kwanini hukumpenda badala yale ukaenda kuchepuka na mtu unayedhani ana tabia mbovu kwasababu ya kazi yake ya mapokezi hospotalini.
 
Sio naogopa kupenda, sijui kupenda.

Kila nnaekua nae namuona wa kawaida na wa kupita tu. Sina ile ya kua na malengo ya muda mreefu coz mpango wa ndoa kwa sasa upo kando.
 
Ndio maana nikamwambia asijiite ertugrul bey... Katumia hisia zaidi kwenye mahitaji ya akili.

Huwa naamini wanaume tumapaswa kutumia akili kuliko hisia.
Mkuu ertugrul nae ana moyo....kuna jamaa mmoja ameongea point Sana kuwa....ukiona madhaifu ya mwenzako ni mazito kuyabeba basi ujue,Hilo sio chaguo lako la moyo na akili....nakubaliana na point yake

Kwenye mapenzi panatumika akili na Moyo mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…