Baba " mwanangu upo tayari taratibu za ndoa ziendelee'' @Etugrul bey" ndio baba''

Baba " mwanangu upo tayari taratibu za ndoa ziendelee'' @Etugrul bey" ndio baba''

Niliwahi kuwa katika mahusiano ya namna kama hiyo ilikuwa ni shida kubwa sana. Meanzoni mambo yalikuwa mazuri show inapigwa hadi Binti akikaa anacheka tu mwenyewe, ukimuuliza anakwambia nimekumbuka tu venye unanifanya vizuri hadi huku chini kunatamani kuongee kukushukuru.

Tatizo lake ni kauli mbovu na lugha chafu. Akikasirika hachagui neno la kukuambia anaropoka tu, ile hali ilikuwa inanipa tabu sana kuweza kuivumilia. Nilifanya kila namna kumueleza lakini alirudia tabia ile mara kwa mara.

Mwili na hisia zangu kwake vikapoa kama barafu, nikakosa stamina nikapoteza hamu ya kuwa naye mwishowe akawa ananituhumu kuwa namsaliti. Nilibwaga manyanga nikatembea nikasonga mbele.

Akina mama chungeni sana kauli zenu kwa waume zenu zinakata sana stimu kauli chafu
Ipo siku utapata kauli nzuri ila 0 chemistry😅
Maisha haya
 
Mkuu huyo mdada ana shepu la maana Tu....ukitembea nae unajua hapa Nina mwanamke...lkn mwisho wa siku shepu yake hainipi ridhiko la moyo wangu......

Mkuu huwa sibabaishwi na matamanio linapokuja swala la kuchagua mwanamke WA kuishi nae....huwa naangalia Tabia za msingi Sana lkn bila kusahau mvuto Kwa mwanamke husika....na mvuto sio shepu kubwa au rangi au UZURI...ni vile ukimuangalia unajisikia Raha,we hujawahi kuona mtu anampenda mwanamke kimbau mbau kama mstimu wa nguzo ya umeme? Kuna kitu ambacho anavutiwa nacho...huenda ni Sura au umbile lile kipotabo ndo ugonjwa wake......kwahiyo hata Mimi Nina uchaguzi wangu na utashi wangu jamani....😂😂😂 naomba mniache Tu jamani
Mkataa pema.....
 
Pole yake mke wa kwanza,mi mtu akishanipenda kwakweli nampenda automatic na kinyume chake ni kweli,maisha yangu yamekuwa mazuri kwa sababu hiyo
 
Asante Kwa maoni yako mkuu.....ishu sio kupendwa Bali ishu ni upendo ndani ya ndoa....kama yeye ananipenda Ila Mimi simpendi je huoni hapo kuna tatizo....ujue yeye ni mwanadamu itafikia kipindi ataona yeye ndo anajitoa zaidi kuliko Mimi....na kibaya Zaidi wanawake ni watu WA hisia Sana...wanapenda kupendwa na kuonyeshwa mahaba...na kama ulifuatilia maelezo yangu vizur...nilisema alikuwa analalamika kuwa hakuna mapenzi ndani ya ndoa...tunaishi kama wazee! Kwahiyo mwisho wa siku angeshindwa na kutafuta faraja nje na ndo yangekuwa haya haya coz kama ningegundua amecheat basi ndoa ingevunjika vile vile....kwahiyo bado naamini nimefanya uamuzi sahihi.

Huyu ambaye natarajia kuwa nae kiukweli ananipenda pia nimejiridhisha juu ya Hilo....na alimhurumia Sana mwanamke mwenzake na akataka pia ikiwezekana nimrudie mke wangu pia wawe wote....so itategemea na maamuzi ya huyo aliyekuwa mke wangu kama ataafiki au laa.
Eti umejiridhisha anakupenda
Wewee moyo wa mtu kichaka subiria show
 
Ni Kama Vile sikuelewielewi..

Yaani ulimuoa mara ya kwanza, ukawa hujampenda.. mkaachana.

Sasa hivi unataka kumuoa kama mke wa Pili, na kwa maelezo yako bado hujampenda.

Mbona kama unataka kurudia kosa lilelile.
 
pole yake mke wa kwanza,mi mtu akishanipenda kwakweli nampenda automatic na kinyume chake ni kweli,maisha yangu yamekuwa mazuri kwa sababu hiyo
Samahani Kwanza unaongea kama me au ke...usinielewe vibaya tafadhali
 
Ni Kama Vile sikuelewielewi..

Yaani ulimuoa mara ya kwanza, ukawa hujampenda.. mkaachana.

Sasa hivi unataka kumuoa kama mke wa Pili, na kwa maelezo yako bado hujampenda.

Mbona kama unataka kurudia kosa lilelile.
Kama ikatokea kumrudia sasa HV ni Kwa AJILI ya malezi ya watoto na hata hivyo hilo Jambo kutokea ni asilimia ndogo sana....na let's say Kwa mfano limetokea nitakuwa na utulivu WA nafsi Kwa mke mwingine,kwahiyo hata kama kwake nikikutana naye mara chache chache itakuwa sio mbaya....ishu ni kwamba sitalazimika kuzini ktk mazingira haya.

Lkn ukifikiria kiundani ni mtihani kumrudia .kwasababu je kipindi hiki ambacho nimemuacha je kama amempata mwamba anaye mkuna vizur unafikir akiwa ndani ya ndoa.....hawezi kuchepuka kwakuwa kumbuka Mimi tayar sitamtafuna kihivyoo kwasababu sina appetite nae Sana!
 
Hapa naongelea uhalisia sababu uhalisia upo. Sasa unapoleta habari ambazo hazina uhalisia tunazirudisha katika uhalisia ambao ndiyo mzani wetu.
Kaka labda nikusaidie Kitu kimoja huenda umekimiss kwenye story yangu....kifupi ingetakiwa nisimuoe kabisa huyo mwanamke nilishajua simpendi....Ila kosa nililolifanya ni kutositisha ndoa isifungwe...na hii kutokana na je ningewaambia nini ndugu zangu na mke mtarajiwa tena dakika za mwisho?

Yaani hata kuishi naye hiyo miaka Saba nimejitahidi Sana tena Sana.....msio elewa haya mazingira mnalaumu Tu....kuna watu wanapendana haswaa na wamedumu miezi mitatu Tu! VP khs Mimi ambaye sikumpenda kabisa?

Ndio maana nimetoa hii story ili watarajiwa wajifunze wasijeingia ktk mazingira kama niliyo ingia mimi kwakuwa yanahuzunisha sana
 
Sawa kabisa kingunebe ....tangu Jana nilihisi huu ni mwandiko wa kike ingawa sikuwa na uhakika💯......kama ni hivyo upo sahihi kabisa.

Wanawake huwa wanapenda kupitia kusikia ndio asili Yao au Kwa maana nyingine mwanamke akionyeshwa upendo nae automatical anapenda...ndio maana si ajabu kukuta mwanamke anapenda sex voice ya mwanaume hata hajamuona....au ukachat nae Kwa maneno mazuri mazuri akajikuta ana fall in love mazima!

Lkn kinyume chake mwanaume anapenda kwa kuona,yaani tunamuona mwanamke Kwanza ndio tunampenda....hlf mambo mengine yanafuatia baadae

Kwahiyo nakubaliana na wewe kabisa unavyosema mtu akikupenda automatical unampenda....

Halafu dada yangu weka basi hata avatar ya kike hapo bhana utawafanya watu washindwe hata kuja kukusalimia pm wakijua ni me 😂😂😂😂
 
Hii ni story ya kweli ya ndoa yangu iliyodumu kwa miaka Saba (7)....lengo la kuandika bandiko hili ni Kwa wadau ambao wanataka kufunga ndoa au kuingia katik Maisha ya ndoa..wajifunze kitu Fulani hapa

Kabla ya kukutana na mke wangu nilikuwa katika mahusiano na binti mmoja hivi....lkn mahusiano yetu haya kuwa mazuri Kwa maana mwenzangu alikuwa na option nyingi na hivyo kushindwa kujua yupi anafaa kuanza nae Maisha ya ndoa...hivyo baada ya kuona mwenzangu haeleweki nikaona isiwe tabu nikaachana nae na kuendelea na Maisha mengine.

Mara paap .....nikakutana na mwanamke mwengine,kwakweli alinijali Sana na kunitreat vizur kiasi nikaona mapenzi si ndo haya sasa...lkn kiukweli ni kosa kubwa Sana kuingia ktk uhusiano mwengine mara baada Tu ya kuachana na awali...kwani unaweza dhani unampenda mtu kumbe sio kweli,ni kwasababu Tu Kwa Wakati huo unapata faraja kwake.

KOSA NAMBA MOJA.....inashauriwa mara baada ya kuachana na uhusiano WA Kwanza usijiingize katika mahusiano haraka haraka take time na upate uhakika kama hisia zako ni za kweli....kwahiyo mm fasta nikaingia na ndani ya miezi minne tukakata shauri tufunge ndoa..lkn binti akasema tusi sex mpaka tufunge ndoa any way kwangu haikuwa na shida kabisa...tulichofanya tukapima afya zetu na kujua status yetu....lkn wakati matayarisho ya ndoa yanaendelea nikawa na mashaka na hisia zangu...lkn nikapuuzia Tu!
Wakati matayarisho yanafikia ukingoni napata uhakika sasa kuwa hapa hakuna hisia za kweli.......

Tafuta pop corn au karanga hapo Kwa mangi ushushie taratibu huku unakula madini....usiwe serious Sana kana kwamba unasoma tangazo la kifo au unaangalia dodoso la Sensa...just relax okaaay!

KOSA NAMBA MBILI....Kipindi cha mwisho mwisho cha maandalizi ndio hisia zangu zinakataa au zinanisaliti hivi hivi...swala linakuja nitaanzaje kuahirisha ndoa,nitamwambiaje mwenzangu na ndugu zangu pia....hlf kumbuka Mzee wangu aliniuliza my son tuendelee na taratibu za ndoa nikamjibu ndio! Halafu baadae nije na habari nyingine? Nikajisemea Baharia haogopi kuchafuka Kwa bahari lazima meli ikate Mawimbi Tu iwe mvua iwe jua!

Mungu mkubwa ndoa ikapita salama salimini,na Maisha ya ndoa yalikuwa na furaha Sana na Amani ,kifupi mke nilipata Sana Tu,anajali,msikivu na anajua nini maana ya kuwa mke. Tatizo baharia Mimi ndio hisia Kwa mke wangu sina....show zilikuwepo lkn sio zile zinazo takiwa haswaa....yaani mpaka nijilazimishe wkt Yale mambo yanatakiwa yaje automatic Tu kama kuvuta pumzi vile!

Mwenzangu akawa analalamika kuwa mbona tunaishi kama tumekaa kwenye ndoa miaka 20 vile au kama wazee vile Kwa maana hakuna maneno matamu ya mapenzi,simwambii kama nampenda daah ikawa changamoto...mtu mzima najitahidi kumwambia lkn baadae nasahau na hata nikimwambia naona unafiki Tu coz najua simaanishi....ukisikia mke na mume wanaishi kama house mate ndo hiyo sasa,yaan mnakula vizur,hakuna ugomvi na mnaishi vizur lkn chemistry hakuna.

Ndo baharia nikatafuta faraja nje ya meli ya yangu mwenyewe...nikachepuka lkn sijisifii Kwa hili hata kidogo kwani huu ni udhaifu mkubwa Sana...lkn ndo hivyo tena nimeingia Choo cha kike inabidi nichutame!

Chukua hii....watu mara nyingi huwa hawachepuki na watu wapya Ila ni watu wao WA zamani kwahiyo kuwa makini Sana na wapenzi WA zamani WA mtu wako...sio unaambiwa '' unajua huyu ex wangu ndio ananisumbua nilimwambia asinifuatefuate Ila mbishi tu'' nah aisee utapigwa na kitu kizito sasa hivi shtuka fasta.....hapa sikuchekupa na Yule mwenye option nyingi laa! ila kabla sijakutana na huyo aliye zingua,kulikuwa na mwingine pisi Kali ila level zake kubwa na alikuwa anafanya kazi hospital Fulani ushuani halafu yupo mapokezi just imagine anakutana na washua wangapi?

So nilimpotezea Tu kimya kimya lkn nilimtafuta Tu nipate faraja na bahati nzuri alikuwa hajaolewa bado....naogopa Sana wake za watu! Na ukisikia kila mtu na mtu wake ni kweli kabisa...Yani hii pisi kwangu haichomoi hata akiolewa na Putin Mzee wa KGB atajua anafanyaje ilimradi baharia Mimi nisihuzinike,ndio maana unakuta unaoa mwanamke unampa kila kitu lakini ana mtu wake daah Maisha haya!

Kiukweli nilikuwa namuonea huruma Sana mke wangu,,napenda kukiri wazi kama ningempenda kama ninavyotaka wallah ningekuwa mwanaume mwenye furaha Sana duniani,nakumbuka kuna wakati nilikwama mpaka kulipa Kodi ya nyumba ilikuwa tabu maana tulipanga nyumba nzima,lkn aliongea na familia Yao...kwanza walikuwa tayar kutupa Mda tukae ktk hiyo nyumba mpaka nitakapo kuwa vizur lkn kwenda kukaa Kule nikaona sio Sawa nikaona Bora apangishwe mtu then akilipa kodi tunachukua na kulipa huku walau inakuwa poa hivi..walikuwa na nyumba kadhaa za kupangisha hivyo akakubali wazo langu daah she is an angel kwakweli mpaka nilipo kaa Sawa alinistiri Sana.

Na ndani ya miaka Saba ya ndoa yetu sikuwahi kupata mashaka yoyote juu ya uaminifu wake na wala sikuwaza hata siku moja kupekua Simu yake,na alikuwa ananiambia ujue mume wangu wanawake wengi wanapenda Sana kuliwa lkn shukuru Mimi sipo hivyo...na nikweli hata ukiangalia tafiti mbali mbali wanawake wanapenda kuliwa na ndio maana wanawake walio ndani ya ndoa wengi wanachepuka Sana nje na sababu ni Sisi....tunajifanya tuko busy Sana,mara tumechoka plus hatuonyeshi mahaba kwao kwanini wahuni wasiruke nao!

Kibaya zaidi ikafikia kipindi wakati WA maandilizi dushe linasimama vizur lkn likizama baharini linanywea daah hapo ndo ikawa shida nyingine,kwahiyo nikawa namuwacha mwenzangu katika hali mbaya Sana,au nikipiga Gia namba moja basi ya pili ujue shughuli,sasa alivyokuwa analalamika namna vile ndo ugonjwa kwangu unazidi,Kwa maana nikawa nimeathirika kisaikolojia sasa,kwahiyo tukianza kufanya tendo kuna kitu kinakuja akilini kwangu...najiuliza je ikinywea tena itakuwaje nakweli Bana lile nililo waza linakuja vile vile tena....kwahiyo mwisho wa siku kujiamni kukaondoka kabisa,mwenzangu akanishauri nitafute dawa lkn binafsi najua tatizo liko wapi Kwa maana najua kabisa nipo fiti lkn hisia Kwa mwenzangu sina,na ndio maana nawashauri Sana wanaotarajia kuingia katika ndoa hakikisha unampenda haswaa unayetaraji kuwa nae,migongano mingine ktk ndoa ni ya kawaida Tu lkn ukikosekana upendo wa dhati basi ndio chanzo cha kukosa furaha ya kweli na kuchepuka kunaanzia hapo.

Ikafikia kipindi nikaona hapana ingawa sipendi talaka lkn siwezi ishi maisha ya uongo,sikupenda watoto wetu watatu ambao mmoja nilimkuta nae na wawili tuliozaa pamoja waishi Bila wazazi wao wawili lkn nikaona siwezi ishi ktk Maisha haya kwa kutafuta furaha Kwa mchepuko....na je nitaishi ktk Maisha yasiyo mpendeza mungu Hadi lini....nakumbuka hata mwenyewe alianza kuniambia ''au mume wangu huenda haujanipenda ndio maana huna hamu Sana na mimi'' natamani nimwambie ndio daah lkn nitaanzia wapi baharia Mimi!

Mwisho wa siku nikampa talaka,ingawa aliniambia siku ukipona urudi tuishi tena mume wangu...ishu ikaja je sababu ya kuwaambia wazazi wetu nimemuachia nini coz within seven good years hatujawahi peleka au kutokea ugomvi wowote mpaka ufikie Kwa wazazi...haikuwa na jinsi ingawa ni aibu ukweni ila ikajulikana Tu sina nguvu za kiume..kwangu aibu hiyo ilikuwa afadhali kuliko kuishi ktk ndoa ya kuiigiza,ingawa kwetu wazazi Tu ndo wanajua hiyo sababu ingawa nahisi Dada zangu wanaweza jua Hilo pia si jua bimkubwa na wanawe wa kike tena.

Ni miaka miwili imepita sasa tangu nimuache,tuna lea watoto vizuri Tu sometime mpaka kulipia Ada ananisaidia Kwa mapenz yake....na juzi Kati namwambia bimkubwa natarajia kuoa hivi karibuni kuna binti nimezaa nae mtoto wa kiume,akaumia Sana na kusema mzazi mwenzako vipi maana hata Leo hii yupo tayar umuoe tena...Kwa waislamu kama mwanamke umemuacha Kwa talaka moja au mbili unaweza kumuoa tena upya...ikabidi nimwambia mama ukweli kuwa Mimi sio mgonjwa nipo vizur Tu tatizo sijampenda Sana mwenzangu,ndo amenielewa Ila kumchana mshua ndo bado ila nitamueleza pia,Ila ndugu zangu waliumia Sana kumwacha mke wangu yaani anakubalika Sana.

Ila kwakuwa Mimi ni muislamu naweza kuwa na wake wawili nafikiria kama atakuwa bado hajaolewa na akiridhia uke wenza naweza muoa tena ingawa hapo awali alishaniambia kuwa ukioa mke mwingine mi natoka...huwezi jua with time huenda akakubali lkn akikataa Maisha lazima yaendelee!

Wakati naanza mahusiano na huyu mke wangu mtarajiwa sio Siri nilisha hasirika Sana kisaikojia lkn bahati nzuri nilimweleza kila kitu nikamtaka awe mvumilivu na anisaidie show zirudi kama kawaida...kweli mwanzoni ilinipa taabu lkn baadae nikawa Sawa na show show zimerudi kama kawaida tena Kwa ubora wake,kwahiyo wanawake wakati mwingine sio Kila mwanaume ambaye ana tatizo la nguvu za kiume ni mgonjwa laa! Saa nyingine kauli zako zaweza mfanya akashindwa kupafomu na kumsababishia matatizo ya kisaikolojia....jaribu Sana kumsoma mumeo na kumsaidia linapokuja swala hilo na mwisho wa siku ni show show!

Ni hayo Tu.
Mimi imenitokea bahati Mwanamke ana akili mpaka kwenye dini hayuko vibaya kaniomba nimuoe Mimi nimechomoa sababu sina hisia nae kabisa tokea enzi tunasoma pamoja nikahisi hata tukiwa kwenye ndoa sitokuwa na appetite nae .Kama najiona hata show nisingepiga vyema yangenikuta kama yako kuonekana dhaifu na nisengekuwa mtu romantic kwake.

Umejitahidi kudumu katika ndoa kwa miaka hiyo yote, tujitahidi kuepuka zinaa na tusiwe tunaweka wazi mambo yetu maovu ya nyuma isipokuwa ikipatikana haja na kiasi cha haja , mwisho tuwe wenye kutubia mara kwa mara na kuomba thabati .

Allaah atuongoze ,atuhiadhi na atujaalie mwisho mwema aamiyn.
 
Ni sahihi kabisa kuhusu Tabia wote Mashallah wamejaaliwa.....lkn hivi vitu vinaenda pamoja....kwamaana Tabia na mvuto wa mtu husika au ndio kupenda huko....siamini Nakadori kama wewe binafsi unaweza kuwa na mtu ktk mahusiano kwasababu Tu ana Tabia nzuri? Lazima utavutiwa nae Kwa mwonekano wake....

Na UZURI WA mtu upo Kwa Yule anayependa....na hapa hatuangalii zile sifa kubwa za kidunia sijui mshepu mkubwa au kalio kubwa na mambo kama hayo....muhimu ni nini kile kinakuvutia Kwa mpenzi wako....baada ya hapo sasa ndo unacheki je na Tabia unaipenda?

Lakini lazima kuwe na mvuto Kwanza.
Kweli kabisa hata ,Mimi In shaa Allaah nitatafuta Mzuri(anayanivutia) kati ya wale Wenye Tabia njema , kama uwezekano wa kupata mzuri na Wenye Tabia njema upo why mtu ujitese eti tabia kwanza ? nakuunga mkono kauli yako kuwa "Lazima kuwe na mvuto kwanza"
 
Back
Top Bottom