Baba wa Kambo acheni kuchapa watoto wadogo wa wake zenu mnajidhalilisha

Peleka mtoto kwa baba yake akaharibu mali za baba yake hukoo
 
UKiona mpaka umemchapa mtoto ujue michezo yake ni hatari kwake
Watoto wangu nawachapa vizuri tu
Tena sihitaji kuwa baba wa kambo, huyu mama ana bahati sio jirani yangu maana kama mwanane nimemkuta anafanya mambo ya ajabu anakula fimbo za kutosha tutakutana serikali za mitaa
 
Yule dada etu mtoto wa ba mkubwa alikua anatuambia eti mtoto wake akikosea AAMBIWE YEYE NDIO AMUADHIBU MAANA SISI HATUJUI PA KUPIGA ☺️😁
 
Mtoto wangu mwenyewe nachapa sembuse huyo sperm ya mwingine!! halafu usichokijua watoto wanaelewa kila kitu ila wanafanya makusudi ili kuona reaction ya mzazi,sasa hapo mzazi ukimchekea kuna siku atakufanyia tukio mpaka upate kizunguzungu
 
Hili jibu angelitoa mwanamke ikiwa mtoto sio wake dunia ingemshukia balaa🤔🤔
Nikwambie kitu rafiki saivi kuna uzembe wa wazazi wote ke na me yaani wanapeana mimba bila hata kujali hawaongei tofauti zao zikaisha wote watemi kuachana poa tu mmoja ke ndio anabeba mtoto au watoto kwa tumaini la kupendwa na ua lake! Mwanaume nae hesabu zake ziko palepale atapata bwana watoto watakuwa! Nani akulelee starehe zako? Maana kwenye kukojoa sperm na raha sana matokeo yake wengine ndio wakapambane nayo. Ok usinielewe vibaya mwanamke aliyefiwa na mzazi mwenzie nina huruma nae sana lakini kama mzazi mwenzie anapumua na kifua kikubwa kama mkwe wa rais! Sikubali sikubali.
 
Ni kweli kabisa uzembe upo pande zote. Lakini likishatokea basi hakuna namna zaidi ya kulibeba tu. Kumbuka huyo mtoto akiwa kwa baba yake, naye mama wa kambo atatoa kauli kama hiyo hiyo yako. Matokeo yake sasa🙆‍♂️🙆‍♂️

Kwahiyo mkuu inamaana inabidi kila mtoto apelekwe kwa baba yake, je hao akina baba nao wasioe wabakie mabachela walee watoto wao tu?🙆‍♂️
 
Kuwa sehemu ya maisha ya mtoto ambaye huenda kuna upande haukubaliani na malezi yake ni shida sana.

Ubinafsi wa wazazi unawaingiza watoto kwenye makuzi ya manyanyaso sana. Mtu anaweza kutoa adhabu ya kawaida tu, ila kwa vile sio damu yake unaona ananyanyaswa, akiletewa biscuits unaona analelewa vizuri....

Sidhauri watu watengane, iwe jwa sababu maalumu sana. Ona watoto wanavyotaabika.

Hata hivyo, kulea mtoto ambaye mzazi wake anafurahia maisha huko ni kujitafutia msongo tu, wapewe heshima wazazi wanaolewa watoto wasio wao.
 
Samaki mkunje angali mbichi....imeisha hiyo usipo mkazia bado mdogo akikuwa atasumbua jamii kwa tabia za hovyo hovyo.
 
Utabarikiwa kwa kulea watoto wa wanaume wenzako vizuri? Hili naliona hapa, labda useme huyo mwanaume ni marehemu, ila jamaa limekaa bar na malaya mimi nibarikiwe kwa kumsaidia malezi?
Ma single mother,wanachukukulua vitu simpo simpo tu, usikute Kuna watu wanaamini kulea mtoto wa kambo ni baraka
 
Hahahaha Kila MTU alee BAO lake,ila una hoja upewe nafasi ya kusikilizwa
 
Mbona umewasema mababa tu ao wamama hujawaona?

Aisee usiombe watoto wako walelewe na mama wa kambo ni watu ambao wanajali watoto wao tu roho mbaya kama zote
 
Tofautisha kumchapa mtoto na kumshambulia mtoto. Kumchapa mtoto kwa desturi zetu kumchapa mtoto ni njia ya kumkanya na kumrudisha mtoto kwenye mstari. Ila kumshambulia ndiyo uhesanika kama ukatili, yaani kumpa kipigo kisicho endana na umri ama kosa.

Sasa mtoa mada unapinga vyote ama unazungumzia kumshambulia? Kama kumshambulia naungana na wewe ila kumchapa utakuwa umezingua pakubwa maana mtoto asiyekanywa hupotea.

Labda kama single mother mlikubaliana kuwa hata watoto wenu hamtaki waguswe kabisa na step fathers. Kama ni hivyo inabidi mwandike barua kwenda kwa mwenyekiti wa chama cha step fathers.
 
Mkitaka haya mambo yasitokee hebu acheni kutengana na mliozaa nao ishi na baba wa mtoto au mama wa mtoto aiseee sio kutetea tu mambo ya baba wa kambo mara mama wa kambo,kama hamna mpango wa kuzaa na mnaodinyana nao si mmwagiane nje wakuu....hebu wewe single mother rudi kwa aliyekuzalisha oveeeeeeeer
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…