Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mchawi na mshirikina ni huyo Mwanamke mwenzio asiyekua na akili aliyeaamua kutekeleza Watoto wake wa kuwazaa mwenyewe kwa Baba wa kufikia asiyejitambua!!Mchawi mshirikina huyo.
hivi kwanini hii tabia wanayo wazee???kuanzia 55+Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mara imemuhukumu kwenda jela miaka saba Msirari Muhere (60) mkazi wa Wilaya ya Tarime baada ya kupatikana na hatia ya kumuambukiza ugonjwa wa Ukimwi mtoto wa miaka sita kwa makusudi.
Hukumu hiyo imetolewa mjini hapa leo Mei 31, 2023 na Hakimu Mkazi Mkuu mwenye mamlaka ya ziada ya kusikiliza mashauri ya Mahakama Kuu, Timoth Swai baada ya kuridhishwa na ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo.
Awali kesi hiyo ya jinai namba 7/2023 ilifunguliwa katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime Juni 2021 na kutolewa humu Novemba 2022 ambapo hakimu wa mahakama hiyo ya Tarime aliamuru mshtakiwa huyo kulipa faini ya Sh200,000 au kwenda jela miaka mitano katika kesi hiyo iliyosajiliwa kwenye mahakama hiyo kwa namba 186/2021.
Kufuatia hukumu hiyo mshtakiwa huyo alilipa faini na kisha kuwa huru.
Hakimu Swai amesema kuwa kutokana na hukumu hiyo, Jamhuri ilikata rufaa Mahakama Kuu baada ya kutokuridhishwa na hukumu kwa maelezo ilikuwa kinyume cha Sheria ya Kuzuia Maambukizi ya Ukimwi namba 28 ya mwaka 2008.
"Sheria hii inatamka kuwa mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya kusambaza Ukimwi kwa makusudi hukumu yake ni kifungo cha kati ya miaka mitano hadi 10 jela na hakuna chaguo la faini,"amesema.
Akitoa maelezo ya tukio hilo, hakimu Swai amesema kuwa mwaka 2018 Muhere alioa mke wa pili ambaye alikuwa na watoto watatu ambao aliamua kuishi nao pamoja na mama yao.
Amefafanua kuwa baadaye wanandoa hao waligombana hali iliyopelekea kutengana huku mwanamke huyo akiwaacha watoto wake watatu na baba yao huyo wa kufikia.
Ameongeza kuwa baadaye wanandoa hao walimaliza tofauti zao na kuanza kuishi tena pamoja kama mke na mume na kwamba baada ya muda mwanamke huyo aligundua kuwa mume wake aliwaambukiza watoto wake Ukimwi kwa makusudi.
"Ushahidi umeonyesha kuwa Muhere alichukua sindano na kunyonya damu kutoka kwa mtoto wa mke wake mkubwa ambaye alikuwa ameathirika kisha kuanza kuwadunga watoto wawili wa huyu mke wake wa pili na uchunguzi wa kitabibu umebaini kuwa kati ya hao watoto wawili mmoja wa kiume ameambukizwa ugonjwa wa Ukimwi," amesema.
"Muhere na mke wake mkubwa ni waathirika wa Ukimwi na binti yao alizaliwa na ugonjwa huo kwa hiyo baada ya kutofautiana na mke mdogo aliamua kumkomesha kwa kuwaambukiza watoto wake Ukimwi labda kwasababu hawakuwa wa kwake (Muhere) wa kuzaa," ameongeza.
Katika kesi ya awali jumla ya mashahidi sita walitoa ushahidi wao akiwemo mama pamoja na mtoto ambapo katika rufaa hiyo upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Mawakili wa Serikali, Felix Mshama na Joyce Matimbwi.
MWANANCHI
Kwa hiyo hii Katiba ya Sasa ndiyo inaruhusu ujinga huo!!? Kama kweli ndiyo hiyvo basi bora Katiba mpya ije faster!!Katiba mpya muhimu
Hii Kanda ya ziwa Ina matatizo, nasisitiza tu, hii Kanda Ina ukatili wa Hali ya juu yaani utu haupo kabsaaaMahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mara imemuhukumu kwenda jela miaka saba Msirari Muhere (60) mkazi wa Wilaya ya Tarime baada ya kupatikana na hatia ya kumuambukiza ugonjwa wa Ukimwi mtoto wa miaka sita kwa makusudi.
Hukumu hiyo imetolewa mjini hapa leo Mei 31, 2023 na Hakimu Mkazi Mkuu mwenye mamlaka ya ziada ya kusikiliza mashauri ya Mahakama Kuu, Timoth Swai baada ya kuridhishwa na ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo.
Awali kesi hiyo ya jinai namba 7/2023 ilifunguliwa katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime Juni 2021 na kutolewa humu Novemba 2022 ambapo hakimu wa mahakama hiyo ya Tarime aliamuru mshtakiwa huyo kulipa faini ya Sh200,000 au kwenda jela miaka mitano katika kesi hiyo iliyosajiliwa kwenye mahakama hiyo kwa namba 186/2021.
Kufuatia hukumu hiyo mshtakiwa huyo alilipa faini na kisha kuwa huru.
Hakimu Swai amesema kuwa kutokana na hukumu hiyo, Jamhuri ilikata rufaa Mahakama Kuu baada ya kutokuridhishwa na hukumu kwa maelezo ilikuwa kinyume cha Sheria ya Kuzuia Maambukizi ya Ukimwi namba 28 ya mwaka 2008.
"Sheria hii inatamka kuwa mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya kusambaza Ukimwi kwa makusudi hukumu yake ni kifungo cha kati ya miaka mitano hadi 10 jela na hakuna chaguo la faini,"amesema.
Akitoa maelezo ya tukio hilo, hakimu Swai amesema kuwa mwaka 2018 Muhere alioa mke wa pili ambaye alikuwa na watoto watatu ambao aliamua kuishi nao pamoja na mama yao.
Amefafanua kuwa baadaye wanandoa hao waligombana hali iliyopelekea kutengana huku mwanamke huyo akiwaacha watoto wake watatu na baba yao huyo wa kufikia.
Ameongeza kuwa baadaye wanandoa hao walimaliza tofauti zao na kuanza kuishi tena pamoja kama mke na mume na kwamba baada ya muda mwanamke huyo aligundua kuwa mume wake aliwaambukiza watoto wake Ukimwi kwa makusudi.
"Ushahidi umeonyesha kuwa Muhere alichukua sindano na kunyonya damu kutoka kwa mtoto wa mke wake mkubwa ambaye alikuwa ameathirika kisha kuanza kuwadunga watoto wawili wa huyu mke wake wa pili na uchunguzi wa kitabibu umebaini kuwa kati ya hao watoto wawili mmoja wa kiume ameambukizwa ugonjwa wa Ukimwi," amesema.
"Muhere na mke wake mkubwa ni waathirika wa Ukimwi na binti yao alizaliwa na ugonjwa huo kwa hiyo baada ya kutofautiana na mke mdogo aliamua kumkomesha kwa kuwaambukiza watoto wake Ukimwi labda kwasababu hawakuwa wa kwake (Muhere) wa kuzaa," ameongeza.
Katika kesi ya awali jumla ya mashahidi sita walitoa ushahidi wao akiwemo mama pamoja na mtoto ambapo katika rufaa hiyo upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Mawakili wa Serikali, Felix Mshama na Joyce Matimbwi.
MWANANCHI
Umesahau wizi ufisadi ujambaz utapeli rushwa daaah wanaume ni mateso lawama ushoga vita kazi ngumu full shidaaKila sehemu hiyo gender inafanya uharibifu, si kwa watoto, walemavu, wazee, wanawake, inatishaaa
Hayo aliyofanya mtuhumiwa ni mauaji alipaswa naye kuuawa..Sheri ya kijinga sana hio, adhabu ndogo mno
Afungwe miaka 30 kwa gharama za nani? Kwa zuri lipi alilolifanya hata akatunzwe kwa muda wote huo?30 michache sana, kama kweli amefanya hayo (hajasingiziwa), basi kifungo cha maisha jela ni haki yake.., yaani ingekuwa mimi huyo angekula shaba ya kichwa
Unatafuta kuhamisha mada kwa kuleta habari za gender?Nimekosa la kusema hii gender hii [emoji119]
Nitajie matukio ya kutumbukiza watoto chooni na kuchokonoa mimba nikutajie matukio yaliyofanywa na hiyo gender kwa mwezi mmoja tu.Unatafuta kuhamisha mada kwa kuleta habari za gender?
Kwani ni gender gani hutumbukiza watoto vyooni au huchokonoa mimba?