Baba wa kambo jela kwa kumuambukiza mtoto UKIMWI kwa makusudi

Daah aisee matukio ya Watanzania ukiyasikia yanatisha sana wana Unyama huyo mnyama mwenyewe anasubiri mbali sana...
 
Sheria bado ni nyepesi mno.

Kwa muktadha huo atakaa gerezani kwa miaka minne na point. Wakati ukatili aliowafanyia watoto ni wa maisha.

Sheria inabidi iongezewe meno. 30 years at least.

Hata hiyo 30 bado ni midogo. Hapo irekebishwe iwe kifungo cha maisha, na itapendeza zaidi ikiwa ni kunyongwa mpaka kufa. Maana kafanya kwa makusudi.
 
Aiseee,
Hivi huwaga ni magonjwa ya Akili au Ukatili wa namna gani???

Mtoto wa miaka 6 kweli ????
Umaskini/ufukara,ujinga,hapa lazima ubongo ushindwe kufanya kazi vzr,unakuwa mtu asiyejielewa,
Unakuta tamaa,unakuwa katili,unaona kila mtu ndio kakusababishia hiyo hari,
Kwa wale tuliowahi kuvamiwa na vibaka,Hawa madogo Huwa hawana huruma,macho yao Huwa yamejaa chuki,kutokana na maumivu ya umaskini,kupoteza mwelekeo wa maisha,
Unakuta wameishakusaula kila kitu,cm,pochi,begi,viatu,lakini hawakuachi,unaachiwa ngeu!
Nikala mtama,tofauli likatua usoni,damu kibao,nikapata wenge,sauti haitoki,fahamu ziliporudi nilikimbia kama husein bolt!wakawa wananifata
 
Nitajie matukio ya kutumbukiza watoto chooni na kuchokonoa mimba nikutajie matukio yaliyofanywa na hiyo gender kwa mwezi mmoja tu.
Aliyeumiza au kuu kumi Vs 9 wote ni makatili na wauaji
 
Aaarrrgh!! 😫 What a nonsense!! Huyu mbuzi alistahili kifungo cha miaka 10, na siyo 7.
 
Nchi hii Kuna sheria nyingine zinatungwa mpaka unajiuliza hawa waliotunga walikuwa na akili kweli!?? Huyu anatakiwa kuhukumiwa kunyongwa kabisaa! Hivi huyo mtoto akikua akakutana na hii story halafu akalipa kisasi kwa kumuua huyu mhusika Kuna atakayekuja kumlaumu..!?? Huyu mtoto akikua atakuwa na Hasira mara 100 zaidi akimuona muhusika yupo nje. Tuna watunga sheria wa ajabu Sana nchi hii...
 
I wish ninge....
Unamnyofoa kiungo kimoja kimoja bila ganzi. Au unamtupa mbele ya fisi wenye njaaa wanamtafuna anajiona. Shetani ndani ya kiwili wili cha binadamu.
 
Ingewezekana angefungwa maisha, huwezi kumsababishia mtoto mdogo aanze kumeza ARVs kwa makusudi yake.

Huu ni uuwaji
 
Jamaa roho ya korosho
 
Akirudi uraiani ataendelea kuambukiza na wengine..

Hata huyo mama akapime...

Huyu Ni wa kumfunga maisha ..alime na kulala tu jela!
 
Lakini mama nae ana makosa na alaumiwe tena sana unaachaje watoto wadogo tena kwa baba wa kambi ihali mmegombana??
Baba mzazi tuu siwezi achia mtoto mdogo tukigombana sembuse baba wa kambo?? Kina mama tujitafakari pia
 
Huyo anafaa kunyongwa kabisa, hafai kuishi, hata huko gerezani anaweza kuwaqmbukiza wenzake kwa maksudi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…