Kuna kitu huwa tunashindwa kuelewa kuhusu dini, maranyingi Wakristo wamekuwa wakiwakebehi Waislam wasemapo kwamba manabii ama mitume fulani waliokuwepo miaka mingi nyuma kabla ya Uislam ni Waislam. Hamtakiwi kukebehi kuhusu hili maana ndio imani yao na vitabu vyao vimeandika hivi.
Kinachofurahisha Wakristo wao hujiona wako sahihi kusema Manabii hao wlikuwa upande wao wakati Ukristo umekuja baadae sana.
Iko hivi: Wayahudi wanaamini maandiko yao matakatifu (Torah). Wakristo wameandika katika biblia yao takatifu kuhusu Moses na maandiko yake lakini hii haiwezi kuwashawishi Wayahudi waamini kwamba Ukristo ulikuwepo tangu kipindi cha Musa. Vivyo hivyo kwa Waislam, Quran imeandika kuhusu Musa na hata Yesu lakini hiyo haitawafanya Wakristo waamini kwamba Uislam ulikuwepo kabla ya Yesu.
Mkijua hili wala hakuna haja ya kumsema mwenzako wakati hata wewe umefata mfumo huo huo. Wakristo wanaamini Wayahudi walimkataa Yesu na walijutia kwa hilo baada ya kumuua lakini ukweli hadi leo hii Wayahudi hawamuamini Yesu kama messiah. Waislam wanaamini Muhammad ni muendelezo wa mpango wa Mungu kuwaleta wasaidizi wake kueleza utukufu wake lakini Wakristo hawaamini katika hilo.
Anayewaita wenzake wafia dini yeye keshaoza katika dini yake[emoji23]