Baba wa marehemu Shukran Amos Said akataa mwili kuzikwa mpaka mahari ya TSh 1,500,000 ilipwe

Ajabu zaidi mwenyewe anakili
Uyo Mtoto wake Marehemu kubadilisha Dini mwenyewe!!

Lkn sasa anataka kupewa pesa au atamzika kwa Dini yake ya zamani hii Kiboko 😛

japo kama anadai pesa za mahari Angesema atamzika yeye kwao lkn mambo ya Iman katisha zaidi 😀
 
Naona watu walio jitia uzungu uchwara wanajifanya kumpinga na kumkejeli Mzee eti sijui umasikini.
Kwa Mila na desturi za kiafirika na kidini iwe ukristo au uislamu mwanaume hana mamlaka wala haki yeyote Kwa mwanamke,au Kwa watoto alio wazaa Kwa mwanamke ambaye hajamtolea mahali.

Mzee Yuko sawa kabisa ,alafu huyu jamaa aliye muuwa mke wake naye chenga alikuwa analalamika kunyimwa uchumba kumbe hata mahari alikuwa hajalipa.
 
Mahari huwa haimalizwi yote usikute alitoa 500k au 2m au 5m au 3.5m kikawa kimebakia kiasi cha sh. 1.5m
Sio kweli Kwa mujibu wa uislamu ambayo ndo dini ya huyo mwanaume mahari ni kitu cha lazima na ni deni ni lazima ilipwe yote.
 
Baba wa marehemu Shukran Amos Said, mwanamke anayedaiwa kuuawa na mwanaume aliyefahamika kwa jina la Khatibu Mfaume katika eneo la Maili Mbili, jijini Dodoma, amekataa kuruhusu mwili wa binti yake kuzikwa na familia ya mume wake wa zamani kutokana na mgogoro wa mahari.

Inadaiwa kuwa baada ya tukio hilo, Khatibu Mfaume alijisalimisha kwa Jeshi la Polisi. Wakati familia zikianza kujipanga kwa ajili ya mazishi, familia ya mume wa zamani wa marehemu, ambaye alizaa naye watoto wawili, iliamua kushughulikia msiba huo na taratibu za mazishi.

Hata hivyo, hatua hiyo imekumbana na pingamizi kutoka kwa baba wa marehemu, Amos Said, ambaye amesema hataruhusu mwili wa binti yake kuzikwa na familia hiyo hadi suala la mahari litakapopatiwa ufumbuzi.

Akieleza msimamo wake, mzee Amos Said amesema binti yake alizaa watoto wawili na mume wake wa zamani, lakini hadi wakati huo hakukuwa na malipo ya mahari yaliyokamilishwa kwa familia yake.

Amesema yuko tayari kuruhusu familia ya mume wa zamani wa binti yake kuendelea na mazishi endapo italipa shilingi milioni moja na laki tano (TSh 1,500,000), kiasi ambacho amesema ni mahari inayodaiwa.

Aidha, amesema iwapo familia hiyo itashindwa kulipa kiasi hicho, atachukua jukumu la kumzika binti yake kwa taratibu za Kikristo, licha ya kuwa marehemu alibadili dini baada ya kuolewa na mume wake wa kwanza.

Mgogoro huo umeibuka wakati familia zikiwa katika kipindi cha majonzi kufuatia kifo cha Shukran Amos Said, ambaye kifo chake kinadaiwa kuhusishwa na mwanaume aliyekuwa katika uhusiano naye
Hiyo inaitwa nitoke vp
 
Wakamzike mtoto wao.
 
Huku usukumani ni kawaida tu hayo, tena hiyo 1500k ni cha mtoto yani wamemuonea huruma tu
Hao wasukuma ndio washenzi wanaozesha vitoto vyenye umri wa miaka 12 wanapomaliza la saba wanatafuta kwa kwenda kuchukua ng'ombe 25.

Mtoto wa miaka 12? Mahari ni mila ya hovyo I epitaph na wakati
 
Back
Top Bottom