Baba wa marehemu Shukran Amos Said akataa mwili kuzikwa mpaka mahari ya TSh 1,500,000 ilipwe

Sio kweli Kwa mujibu wa uislamu ambayo ndo dini ya huyo mwanaume mahari ni kitu cha lazima na ni deni ni lazima ilipwe yote.
Mahari ni biashara ambayo wameificha katika kichaka cha zawadi.

Zawadi ya kulea? Kulea ni jukumu la nani? Unamshukuru mtu kwa kutimiza wajibu wake au majukumu yake?

Mila ya wake wengi, mila ya kuoa mahari na zingine zinazo tweza utu wa mtu au zinazoweza pelekea kuenea kwa magonjw nk ni zimepitwa na wakati
 
Kama ni mie sitoi mahari,akae na mwili wake🙌
Ni kama mila ya kugomboa mtoto.. ushenzi mtupu. Watoto wakikua wataenda kwa baba yao.

Ni ujinga ujinga tu.

Unakuta anayepigania mahari ni mwanamke ambaye hiyo mahari wala hanufaiki nayo zaidi muuzaji (baba na ndugu zake) ndio mnufaika mkuu na kuipagia cha kufanya kama anaongeza mke au kuhonga ni yeye na hakuna wakumuhoji.
 
Hii ya kugomboa mtoto ni ufala, anko wangu alizaa na binti,wakakaza amgomboe,dadeq akawa anahudumia bibi mtu anataka anko akajitambulishe,mbona mtoto wametuachia bila kutambulisha Wala kugomboa,na majina anatumia upande wetu na cheti nk,
 
Anyways Mila na Desturi zifatwe Tu kama hivyo ndivyo unapaswa kuwa
 
Cha kwanza Kwa mujibu wa uislamu mahali ni ya Mali ya mwanamke muolewaji na na si Mali ya mzazi wake ,na anatakiwa apewe yeye na ndio maana hata kiasi cha mahali linatakiwa kutamkwa na mwanamke.
 
Cha kwanza Kwa mujibu wa uislamu mahali ni ya Mali ya mwanamke muolewaji na na si Mali ya mzazi wake ,na anatakiwa apewe yeye na ndio maana hata kiasi cha mahali linatakiwa kutamkwa na mwanamke.
Kama hivo ni kweli; vipi kama mwanamke mwolewaji hawezi kutamka??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…