Baba wa Mwimbaji wa Injili aliyeimba "Mnatuona Nyani tu" ahukumiwa miaka 3 jela kwa kuendesha Kanisa bila kibali

Baba wa Mwimbaji wa Injili aliyeimba "Mnatuona Nyani tu" ahukumiwa miaka 3 jela kwa kuendesha Kanisa bila kibali

Vita ya Dini haitoweza kutokea, unajua kwanini?

Huu mchangamano wa Dini mbili kuishi ktk familia moja bila tatizo na kila mtu akaabudu anavyotaka ndio imesaidia haya.

Mwisho wa siku unakuta Baba Mkristo Mama muislam. Vita inaanzia wapi? Watu psychology zao tyr wameshaona hakua uadui between hizi Dini.

Ishu ni moja ambayo mbaya ni UKABILA. hiyo ndio Kansa mbaya zaidi. Em fatilia vuguvugu la UZANZIBAR na UTANGANYIKA alafu linganisha na Vuguvugu la UISLAM na Ukristo. Utaona wapi pakianza kutokota kunateka hisia za wengi.

Ukabila na Ukanda ndio utaleta shida hasa huu MUUNGANO hautavunjika kirahisi.. huwenda Bendera zikawa na ka rangi kekundu.
Hii Nchi ina udini sana fungua macho yako.
 
Mchungaji Mwakipesile ambaye mtoto wake Sifa Bujune alikamatwa kwa kosa la kusambaza uongo kwa kuimba wimbo wa "Mnatuona Nyani tu" amehukumiwa miaka mitatu jela kwa kosa la kuendesha kanisa bila ya kuwa na kibali.

View attachment 2766355

================== ==================
Mchungaji Mbarikiwa Mwakipesile (39), baba mzazi wa Sifa Bujune, Muimbaji wa Injili anayetuhumiwa kusambaza uongo kutokana na Wimbo wake wa “Mnatuona Nyani tu”, amehukumiwa kifungo hicho na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa kosa la kuendesha huduma ya kiroho bila kibali.

Akizungumza na JamiForums, Wakili Boniphace Mwabukusi amesema “Kweli amehukumiwa lakini Mchungaji alifuata machakato wa kuomba vibali japo Serikali ndio ilikuwa ikichelewesha ukamilishwaji, pia Sheria inasema mtu ambaye yupo katika mchakato wa maombi hawezi kushtakiwa."

Ameongeza "Adhabu aliyofungwa nayo ina faini na kifungo, Hakimu ametoa adhabu ya kifungo bila faini, tunatarajia kukata rufaa Jumatatu (Oktoba 2, 2023)."

=================​
Pia soma: 'Mbeya: Msanii wa Nyimbo za Injili, Sifa Bujune ashikiliwa kwa tuhuma za kuimba wimbo wenye maudhui ya uchochezi' Mbeya: Msanii wa Nyimbo za Injili, Sifa Bujune ashikiliwa kwa tuhuma za kuimba wimbo wenye maudhui ya uchochezi
Huyu HAYAWANI muache aende jela pengine akili itamkaa sawa.

Mtu anaizushia Uwongo Serikali kuwa imeua mtoto wake ili apate forum ya kutukana.
 
Huyu HAYAWANI muache aende jela pengine akili itamkaa sawa.

Mtu anaizushia Uwongo Serikali kuwa imeua mtoto wake ili apate forum ya kutukana.
Mkuu akizushia serikali uongo si anapaswa kushtakiwa kwa uongo? Akishindwa kuthibitisha atiwe ndani.

Haya mambo Stuxnet uliyapinga enzi za Awamu ya Tano ila sasa naona na weww umeyaunga mkono?

Je ni kwa sababu sasa hivi ni zamu yenu? Au kumbe mlikuwa mkikosoa maovu kwa wivu tu sio kwa sababu ya Uhalisia?

Nilidhani jambo Baya mtu kama Stuxnet ataendelea kusimamia Ukweli bila kujali nyakati.

Aidha hii ndio sababu Watu wakipata madaraka wanaamua kujitoa fahamu na kukandamiza wanavyotaka maana wanaamini hata nyinyi mkiyapata mtafanya hivyo hivyo.

Umetoa comment mbaya sana kwa Mtu kama Wewe
 
Kwa nini nyumba ya ibada iwe na usajili serikalini katika nchi inayotoa uhuru wa kuabudu kikatiba kwa kila mtu?

Serikali hata kodi haikusanyi kutoka nyumba za ibada, sasa zinasajiliwa kwa nini?

Nikisema hii habari ya kusajili nyumba za ibada serikalini ni namna ya serikali kudhibiti ibada na kuingilia uhuru wa kikatiba wa kuabudu nitakuwa nakosea?
Hizi madhehebu ya kishenzi zisipodhibitiwa zitatupeleka walikofika Wakenya na Shakahola.

Hongera Serikali kwa hatua THABITI, mungecheka na nyani tungepata ya Kibwetere. Maana Mbarikiwa Mwakipesile na wafuasi wake wote wameshakuwa INDOCTRINATED vibaya
 
Hii Nchi ina udini sana fungua macho yako.
Hauna Makali, hawapo strict.
Unalewa na Muislam unalewa na mkristo. Pembeni kuna kitimoto huyu mmoja hali mwingine anakula. And sometimes wote wanakula kitimoto.

Utasema kuna wafia Dini hii nchi..?
Nenda huko Afrika ya kati uone kama wanaishi hivyo.
 
Hehehee
 
Mkuu akizushia serikali uongo si anapaswa kushtakiwa kwa uongo? Akishindwa kuthibitisha atiwe ndani.

Haya mambo Stuxnet uliyapinga enzi za Awamu ya Tano ila sasa naona na weww umeyaunga mkono?

Je ni kwa sababu sasa hivi ni zamu yenu? Au kumbe mlikuwa mkikosoa maovu kwa wivu tu sio kwa sababu ya Uhalisia?

Nilidhani jambo Baya mtu kama Stuxnet ataendelea kusimamia Ukweli bila kujali nyakati.

Aidha hii ndio sababu Watu wakipata madaraka wanaamua kujitoa fahamu na kukandamiza wanavyotaka maana wanaamini hata nyinyi mkiyapata mtafanya hivyo hivyo.

Umetoa comment mbaya sana kwa Mtu kama Wewe
Huyu mshenzi tu ninamfahamu, DG wa TISS anawezaje kumuua mtoto wa Mwakipesile? Tatizo la hizi YouTube, mtu anaongea ujinga wake kwenye microphone na nyinyi mnamuamini. Yule ni mwehu tu. Hakuna kanisa wala nini pale. Hawa ni typical akina Kibwetere au Mackenzie. Nakubali nilimpinga Magufuli kwa unyama wake wakati ule.

Ila kwa hili la Serikali kudhibiti madhehebu ya kishenzi yanayochipuka Mbeya kila siku, NAIPONGEZA Serikali.
 
Wakati wa ukominist, ili upate kibali Cha kuanzisha kanisa Urusi lazima ukiri kwamba Mungu ana watoto wawili, Yesu na Lenin, ila Lenin ni mkuu zaidi ya Yesu, hapo utapata kibali, Imani tofauti na hiyo ni kifungo au kifo

Sijuii sifa za kusajili kanisa Tanzania linatakiwa kuamini nini, ili serikali ifurahi
 
Mamlaka ni watu na Tanzania watu wengi wana dini. Hamna kiongozi Tanzania anaweza kushinda vita ya dini ni muhimu tusifike huko. Sa100 lazima ajue Tanganyika siyo Zanzibar
Tutolee "ungeseeer" wako hapa....

Angekuwa ni "mpagani" ungeongea hivyo ?!!!

Kwa hiyo mtu akikosea asihukumiwe kwa kuwa ni mkristo ama muislam?!!![emoji15][emoji15]

Shule ulikwenda kusomea "ushoouuugeeer"?!!!
 
Wakati wa ukominist, ili upate kibali Cha kuanzisha kanisa Urusi lazima ukiri kwamba Mungu ana watoto wawili, Yesu na Lenin, ila Lenin ni mkuu zaidi ya Yesu, hapo utapata kibali, Imani tofauti na hiyo ni kifungo au kifo

Sijuii sifa za kusajili kanisa Tanzania linatakiwa kuamini nini, ili serikali ifurahi
Noma sana mwisho wa Siku Lenin aliacha dunia kanisa bado lipo.

Hawa watawala waoga ni shida.
 
Eti DG wa TISS amemuua mwanaye [emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]

Anastahili miaka 3 nyuma ya nondo.....

Shyyyyynzyyyyy tyyyppp
 
Hili linatosha kumuondoa Sa100 madarakani. Watanzania acheni uzombi. Mtafungwa wote.

Bebeni hata marungu muingie ikulu.
Tuache uzombi tutafungwa wote ? Kwani wewe M-Nyasa ? Kama uko Malawi hayakuhusu. Butt out.
 
Back
Top Bottom