Baba wa Mwimbaji wa Injili aliyeimba "Mnatuona Nyani tu" ahukumiwa miaka 3 jela kwa kuendesha Kanisa bila kibali

Wale wanaohubiri masokoni na stendi na kwenye mabasi waache mara moja. Rungu hili litawashukia.
 
Ukiipa serikali mamlaka ya kudhibiti madhehebu unayoyaita ya kishenzi, halafu serikali ikasema hizi dini zote ni ushenzi wa kigeni, makanisa yote na misikiti yote ni ukoloni wa kiutamaduni, futa yote, kuanzia leo marufuku.

Utakubali? Utafurahia?
 
Pole mkuu naona umeandika Kwa majonzi Sana,

Lakini Ally ndio Yuko nyuma ya mambo yote, mwezake hakuwa hivi,
 
Kama hana kibali funga hata miaka kumi
Tumia Akili wewe hilo komwe lichezeshe leo ndio wamegundua kua hajasajili hiyo taasisi ?
hii inaonesha namna gani serikali imejaza mazezeta yasiyowajibika haiwezekani Mwakipesile afanye hiyo huduma for long time na wasajili wapo tu wamekalisha makalio kwenye viti na kulipwa mishahara ambayo hawaifanyii kazi
hapo serikali imeamua kujivua chupi hadharani
shame! shame! shame!
 
Tii sheria bila shuruti ... Kutokujua sheria sio uchochoro wa kuendelea kuvunja sheria afunge huyo mtu hata 15 years wengine iwe fundisho kwao
 
Mkuu,

Hata hao kina Mackenzie na Kibwetere kama kweli ni washenzi tu cult leaders, njia ya kuwadhibiti ni kuwaelimisha wananchi wajue kuchambua wenyewe mbivu na mbichi.

Unaweza kutandika busati dunia nzima ili mguu wako usikanyage mchanga wa ardhi, au unaweza kuvaa viatu tu na ukafikia lengo lile lile, wewe unataka kutandika busati dunia nzima badala ya kuvaa viatu tu.

Ukiwafunga na kuwanyima vibali hawa wachungaji unawazidishia umaarufu tu, wanakuweka katika narrative yao kwamba hata Biblia ilitabiri kutakuja mpinga Kristo, na hii serikali inayowafungia ndiyo mkono wa huyo mpinga Kristo.

Tushaanza kuona hayo maneno hata kwenye thread hii tayari.

Dini ina nguvu sana, walioweka sheria za kuheshimu uhuru wa ibada hawakuwa wajinga. Waliona mengi sana.

Yani kifupi kuwafungia ndiyo kutakuwa kunawazidishia umaarufu, na ukifanya hivyo watatumia huruma ya watu kujipatia wafuasi zaidi. Wataenda underground usiwaone kabisa.

Kumbuka Ukristo ulianzia underground enzi za Warumi, umesha survive government persecution, unajua kutambaa chinichini sana. Utakachofanya ni kuwafanya waende underground usijue kabisa wanafanya nini.

Serikali inajikuta katika litu kinaitwa "The Law of Unintended Consequences".

Katika jitihada za kuwazima, ndiyo inawaongezea umaarufu.

Halafu watakuwa wanakutana kisiri, wanafanya mambo yao.
 
O
Tii sheria bila shuruti ... Kutokujua sheria sio uchochoro wa kuendelea kuvunja sheria afunge huyo mtu hata 15 years wengine iwe fundisho kwao
ok naona umefurahi kijana cheka sana omba yasikukute kumbuka Shetani hana rafiki

save my coment blood maneno yangu hua hayaendi bure!
 
Na wafungwe tu sababu hakuna namna.
Kwanza kueneza uchochezi, pili kuanzisha kanisa bila kibali lenye lengo la kutapeli waumini na si kuwapa mwongozo wa kiroho.
 
Wale wanaoimba matusi na kusupport ushg wanaachiwa

Ova
 
Kabisa.
 
Huyu si ndio yule mchungaji anayelalamika serikali ilimuua mwanae ili kumnyamazisha, wakamnyima kibaru kwa kuwa anakosoa sana hii serikali ya sa190
 
Acha wafungwe uko wa kambale huu usiokuwa na adabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…