Baba wa Mwimbaji wa Injili aliyeimba "Mnatuona Nyani tu" ahukumiwa miaka 3 jela kwa kuendesha Kanisa bila kibali

Baba wa Mwimbaji wa Injili aliyeimba "Mnatuona Nyani tu" ahukumiwa miaka 3 jela kwa kuendesha Kanisa bila kibali

Wale wanaohubiri masokoni na stendi na kwenye mabasi waache mara moja. Rungu hili litawashukia.
 
Hizi madhehebu ya kishenzi zisipodhibitiwa zitatupeleka walikofika Wakenya na Shakahola.

Hongera Serikali kwa hatua THABITI, mungecheka na nyani tungepata ya Kibwetere. Maana Mbarikiwa Mwakipesile na wafuasi wake wote wameshakuwa INDOCTRINATED vibaya
Ukiipa serikali mamlaka ya kudhibiti madhehebu unayoyaita ya kishenzi, halafu serikali ikasema hizi dini zote ni ushenzi wa kigeni, makanisa yote na misikiti yote ni ukoloni wa kiutamaduni, futa yote, kuanzia leo marufuku.

Utakubali? Utafurahia?
 
"samiah mama yangu,unainajisi ardhi ya TANZANIA KWA hayo,nani KWA kwambia hao HUWA wananyamazishwa hivyo!!?

Unapambana na nani mama yangu"!?

Unafikiri unapambana nae huyo anaefungwa!!?unapambana na aliekuumba Mama"

Nakuonya tu mwachie!!

Mungu ibariki Tanzania nchi yetu niipendayo sana
Pole mkuu naona umeandika Kwa majonzi Sana,

Lakini Ally ndio Yuko nyuma ya mambo yote, mwezake hakuwa hivi,
 
Kama hana kibali funga hata miaka kumi
Tumia Akili wewe hilo komwe lichezeshe leo ndio wamegundua kua hajasajili hiyo taasisi ?
hii inaonesha namna gani serikali imejaza mazezeta yasiyowajibika haiwezekani Mwakipesile afanye hiyo huduma for long time na wasajili wapo tu wamekalisha makalio kwenye viti na kulipwa mishahara ambayo hawaifanyii kazi
hapo serikali imeamua kujivua chupi hadharani
shame! shame! shame!
 
Tumia Akili wewe hilo komwe lichezeshe leo ndio wamegundua kua hajasajili hiyo taasisi ?
hii inaonesha namna gani serikali imejaza mazezeta yasiyowajibika haiwezekani Mwakipesile afanye hiyo huduma for long time na wasajili wapo tu wamekalisha makalio kwenye viti na kulipwa mishahara ambayo hawaifanyii kazi
hapo serikali imeamua kujivua chupi hadharani
shame! shame! shame!
Tii sheria bila shuruti ... Kutokujua sheria sio uchochoro wa kuendelea kuvunja sheria afunge huyo mtu hata 15 years wengine iwe fundisho kwao
 
Huyu mshenzi tu ninamfahamu, DG wa TISS anawezaje kumuua mtoto wa Mwakipesile? Tatizo la hizi YouTube, mtu anaongea ujinga wake kwenye microphone na nyinyi mnamuamini. Yule ni mwehu tu. Hakuna kanisa wala nini pale. Hawa ni typical akina Kibwetere au Mackenzie. Nakubali nilimpinga Magufuli kwa unyama wake wakati ule.

Ila kwa hili la Serikali kudhibiti madhehebu ya kishenzi yanayochipuka Mbeya kila siku, NAIPONGEZA Serikali.
Mkuu,

Hata hao kina Mackenzie na Kibwetere kama kweli ni washenzi tu cult leaders, njia ya kuwadhibiti ni kuwaelimisha wananchi wajue kuchambua wenyewe mbivu na mbichi.

Unaweza kutandika busati dunia nzima ili mguu wako usikanyage mchanga wa ardhi, au unaweza kuvaa viatu tu na ukafikia lengo lile lile, wewe unataka kutandika busati dunia nzima badala ya kuvaa viatu tu.

Ukiwafunga na kuwanyima vibali hawa wachungaji unawazidishia umaarufu tu, wanakuweka katika narrative yao kwamba hata Biblia ilitabiri kutakuja mpinga Kristo, na hii serikali inayowafungia ndiyo mkono wa huyo mpinga Kristo.

Tushaanza kuona hayo maneno hata kwenye thread hii tayari.

Dini ina nguvu sana, walioweka sheria za kuheshimu uhuru wa ibada hawakuwa wajinga. Waliona mengi sana.

Yani kifupi kuwafungia ndiyo kutakuwa kunawazidishia umaarufu, na ukifanya hivyo watatumia huruma ya watu kujipatia wafuasi zaidi. Wataenda underground usiwaone kabisa.

Kumbuka Ukristo ulianzia underground enzi za Warumi, umesha survive government persecution, unajua kutambaa chinichini sana. Utakachofanya ni kuwafanya waende underground usijue kabisa wanafanya nini.

Serikali inajikuta katika litu kinaitwa "The Law of Unintended Consequences".

Katika jitihada za kuwazima, ndiyo inawaongezea umaarufu.

Halafu watakuwa wanakutana kisiri, wanafanya mambo yao.
 
O
Tii sheria bila shuruti ... Kutokujua sheria sio uchochoro wa kuendelea kuvunja sheria afunge huyo mtu hata 15 years wengine iwe fundisho kwao
ok naona umefurahi kijana cheka sana omba yasikukute kumbuka Shetani hana rafiki

save my coment blood maneno yangu hua hayaendi bure!
 
Na wafungwe tu sababu hakuna namna.
Kwanza kueneza uchochezi, pili kuanzisha kanisa bila kibali lenye lengo la kutapeli waumini na si kuwapa mwongozo wa kiroho.
 
Mtumishi wa mungu mwenye nyimbo nzuri za kuabudu za tenzi za rohoni mchungaji mbarikiwa mwakipesile leo amehukumiwa miaka 3 kwenda jela kwa kuanzisha kanisa bila kibali.

ikumbukwe kuwa awali mwanae alitunga nyimbo inayohusu mkataba mbovu wa bandari pamoja na kile kinachiendelea ngorongoro kuhusu matumizi ya nguvu yanayotumika kuhamisha wamasai aka kamatwa na jeshi la polisi na kupelekwa mahakamani kisha na kupata dhamana.

Nyimbo hiyo ilikuwa inaimbwa kuwa sisi tunaonekana nyani kuonesha kuwa sisi wananchi hakuna tunalolijuwa.leo mtumishi wa mungu na mwimbaji mashuhuri mchungaji mbarikiwa mwakipesile amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu kwa kauli zake za kukosoa serikali kigezo cha kusema ameanzisha kanisa bila kibali hakina mashiko mbele ya jamii.[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]

View attachment 2766381
Wale wanaoimba matusi na kusupport ushg wanaachiwa

Ova
 
Kwa nini nyumba ya ibada iwe na usajili serikalini katika nchi inayotoa uhuru wa kuabudu kikatiba kwa kila mtu?

Serikali hata kodi haikusanyi kutoka nyumba za ibada, sasa zinasajiliwa kwa nini?

Nikisema hii habari ya kusajili nyumba za ibada serikalini ni namna ya serikali kudhibiti ibada na kuingilia uhuru wa kikatiba wa kuabudu nitakuwa nakosea?
Kabisa.
 
Huyu si ndio yule mchungaji anayelalamika serikali ilimuua mwanae ili kumnyamazisha, wakamnyima kibaru kwa kuwa anakosoa sana hii serikali ya sa190
 
Mchungaji Mwakipesile ambaye mtoto wake Sifa Bujune alikamatwa kwa kosa la kusambaza uongo kwa kuimba wimbo wa "Mnatuona Nyani tu" amehukumiwa miaka mitatu jela kwa kosa la kuendesha kanisa bila ya kuwa na kibali.

View attachment 2766355


================== ==================
Mchungaji Mbarikiwa Mwakipesile (39), baba mzazi wa Sifa Bujune, Muimbaji wa Injili anayetuhumiwa kusambaza uongo kutokana na Wimbo wake wa “Mnatuona Nyani tu”, amehukumiwa kifungo hicho na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa kosa la kuendesha huduma ya kiroho bila kibali.

Akizungumza na JamiForums, Wakili Boniphace Mwabukusi amesema “Kweli amehukumiwa lakini Mchungaji alifuata machakato wa kuomba vibali japo Serikali ndio ilikuwa ikichelewesha ukamilishwaji, pia Sheria inasema mtu ambaye yupo katika mchakato wa maombi hawezi kushtakiwa."

Ameongeza "Adhabu aliyofungwa nayo ina faini na kifungo, Hakimu ametoa adhabu ya kifungo bila faini, tunatarajia kukata rufaa Jumatatu (Oktoba 2, 2023)."


=================​
Pia soma: 'Mbeya: Msanii wa Nyimbo za Injili, Sifa Bujune ashikiliwa kwa tuhuma za kuimba wimbo wenye maudhui ya uchochezi' Mbeya: Msanii wa Nyimbo za Injili, Sifa Bujune ashikiliwa kwa tuhuma za kuimba wimbo wenye maudhui ya uchochezi
Acha wafungwe uko wa kambale huu usiokuwa na adabu.
 
Back
Top Bottom