Baba wa Mwimbaji wa Injili aliyeimba "Mnatuona Nyani tu" ahukumiwa miaka 3 jela kwa kuendesha Kanisa bila kibali

Mchungaji Mwakipesile ambaye mtoto wake Sifa Bujune alikamatwa kwa kosa la kusambaza uongo kwa kuimba wimbo wa "Mnatuona Nyani tu" amehukumiwa miaka mitatu jela kwa kosa la kuendesha kanisa bila ya kuwa na kibali...
Kumbe naye mwovu licha ya kumtetea mwovu wake
 

Wakili msomi Mwabukusi azungumzia hukumu ya mchungaji Mbarikiwa Dixon Mwakipesile


View: https://m.youtube.com/watch?v=a1-EYritijY
 
Kwenye siasa lazima utumie akili hili jambo litakuza udini. Uhamsho walifungwa na Kikwete, muislamu mwenzao. Sasa sa100 muislamu anaanza vita na RC mara anafunga mchungaji lazima wakristo wengi wakasirike hata kama hawatasema. Huu ni kama ule ujinga wa Mkapa na Mwembe Chai. Vitu vya dini ni sensitive.
 
Saafiii afungwe kabisa Hana adabu na anakazi zakipepo sana... Anatafutaga umaarufu kipumbafu sana sijui anavutaga mibange
 
Mamlaka ni watu na Tanzania watu wengi wana dini. Hamna kiongozi Tanzania anaweza kushinda vita ya dini ni muhimu tusifike huko. Sa100 lazima ajue Tanganyika siyo Zanzibar
 
Sheria na mahakama za Afrika zipo kwa ajili ya kuonea wanyonge na Maskini.

Wabadhirifu wa mabilioni ya fedha za umma wana achwa watambe.

Ila mnyonge anaye jaribu kuendesha ibada tu, anatafutiwa angle ya kushtakiwa.

Uafrika hasa utanzania ni laana.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Serikali imeshasajili makanisa mangapi mpaka sasa??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…