Usichoelewa ni kwamba, biashara haina protection kama ya "separation of state and religion".
Hao wahandisi, matabibu, waganga wa kienyeji, wanasheria, wahasibu etc, wote hawana protection ya "separation of state and religion"
Dini ina hiyo protection.
Ndiyo maana biashara inatozwa kodi, dini haitozwi kodi.
Nyerere alikuwa anaelezea hoja ya serikali kujua idadi ya Watanzania kwa mujibu wa dini zao, akasema serikali haihitaji kujua watu kwa dini zao, kama mtu anataka kujua idaid hiyo aende kwenye nyumba za ibada.
Alielewa separation of state and religion.
Sasa, hatuoni hizi habari za kusajili nyumba za ibada ni kurudi kule kule alikokataa Nyerere kwenye habari ya serikali kujiingiza katika dini?
Kwa nini serikali ilazimishe kusajili nyumba za ibada?