Baba wa Taifa na Mizengwe - Makala ya Askofu Bagonza

Baba wa Taifa na Mizengwe - Makala ya Askofu Bagonza

Informer

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,606
Reaction score
6,672
Mizengwe na fitna havikuanza baada ya Baba wa Taifa kuondoka madarakani. Hata wakati wake, wapo waliojaribu kuanzisha mizengwe na fitna za kisiasa. Tofauti ya wakati ule na huu wetu ni moja tu. Wakati wa Baba wa Taifa, mizengwe na fitna ilianzishwa na wapambe na makanda bila kumhusisha. Alipoigundua, aliikemea na kuikomesha. Wakati fulani alimwajibisha kada wake kipenzi (Sozigwa) alipogundua kuwa anawalazimisha watu kuchangia harambee ya ujenzi wa kanisa fulani huko Dodoma kwa kisingizio cha kumuunga mkono Baba wa Taifa.

Wakati wetu, wapanga mizengwe na fitna wanadiriki ama kuwahusisha wakuu wa mihimili au wanaanzisha mizengwe na fitna na hawawajibishwi. Mizengwe na fitna hizo, vinawachonganisha wakuu wetu na wananchi au hata kuwachafua kuwa wakuu ndio wamewatuma hao wafanya mizengwe na fitna. Imewapasa wakuu wetu kukemea mizengwe na fitna kwa namna ambayo haiachi mashaka kuwa wanahusika na mizengwe hiyo. "Mtu akiwatazama usoni ajue kuwa wanamaanisha wanachokikemea". Hii ni kwa sababu baadhi ya mizengwe na fitna ina sura ya kijinai, mingine inavunja katiba, na mingine inapungua viwango vya kimaadili. Kibaya zaidi, baadhi ya mizengwe na fitna vinafanyika ndani vyombo vyenye utakatifu wa taifa letu.

Katika kukemea na kujitenga na mizengwe hiyo, Baba wa Taifa daima alizingatia mambo matano:

1. Ikulu ni mahali patakatifu. Utakatifu wa Ikulu haukutokana na utakatifu wa Baba wa Taifa bali msimamo wa wazi kuwa yeyote atumikaye Ikulu na aendaye ikulu atatenda na kutendewa haki, si pungufu ya haki. Kwa muda mrefu na kwa nyakati tofauti wakati wa Mwalimu, Mzee Timothy Apiyo na John Rupia walikuwa kama makuhani wa madhabahu ya Ikulu. Chochote kinyonge na kisicho cha nuru hakikuhusishwa na Ikulu. Waliofuata waliiga mfano huu isipokuwa hawakuwa waangalifu katika uteuzi wa "makuhani".

2. Chama kilikuwa kisafi kuliko serikali na Mwalimu alilalamika kuwa matendo ya serikali yalikuwa yanakichafua chama. Msimamo wa kutenganisha chama na serikali ulilenga kukifanya chama kuwa mfano na kielelezo kwa serikali. Kivukoni, JKT na madarasa ya itikadi vililenga kutatua kasoro hii.

3. Pamoja na uwepo wa washauri wa rais, Mwalimu alipata ushauri wake wa msingi kutoka kwa watu wa kawaida. Aliwauliza wapishi, wafagiaji, wakulima shambani, wacheza bao, madereva, wanafunzi na waumini wa kawaida kanisani Butiama ikiwa waliuelewa ujamaa na Azimio la Arusha. Nyakati fulani alimwuliza hata mama yake mzazi. Hekima ya kweli imesheheni katika watu wa kawaida na ndio maana Mungu ameumba wengi mno. Jilindeni na chachu ya watu kutoka Jalalani hata kama elimu yao ni muhimu pia.

4. Mwalimu aliwasikiliza washauri wake rasmi kwa kila sekta bila yeye kuwashauri. Wakati mwingine alifanya kama utani na kukaa na kuwaita waje kumshauri na aliwasikiliza na kuwauliza maswali magumu baada ya kuwasikiliza. Matokeo yake, washauri wake walilazimika kuandika ripoti zao na kumpa mapema azisome. Alizisoma na kuzichafua kwa kalamu ili kuwaonyesha alipokuwa na mashaka.

5. Kwa sababu za kihistoria, Mwalimu aliona maadui wengi nje kuliko ndani. Maadui wa nje aliona ni mabeberu/mabepari. Maadui wa ndani aliona ni viongozi/vibaraka. Alitumia muda mwingi na timu ya mambo ya nje kutafakari matishio ya nje kuliko ya ndani. Hii ilimsaidia kuwatania watanzania aliowaita "waswahili" ambao aliona wanasumbuliwa zaidi na ushamba, ujinga, maradhi na umaskini. Kundi la pili la maadui wa taifa aliona ni viongozi vibaraka kuliko "waswahili".

Sikumbuki wakati wowote Mwalimu alipoona wananchi ni tatizo na kuwatungia sheria ya kuwadhibiti. Aliwakomalia viongozi ambao daima aliona wanataka kutumia ujinga wa wananchi ili kuwanyonya na kuwakandamiza.

Kutokana na misimamo hii ya Mwalimu, yafuatayo yalitokea:

1. Kuna watu walikufa wakaandika urithi wa mali zao kwa serikali au kwa chama tawala. Serikali na chama vilikuwa na hadhi sawa na dini.

2. Watu waliwekesha mali zao serikalini na kwenye chama. Watu walilaza magari yao kwenye viwanja na ofisi za TANU/CCM kuliko kuyalaza kanisani au msikitini.

3. Watu walipeleka mashauri yao TANU/CCM kuliko kuyapeleka mahakamani.

4. Kadi ya TANU/CCM ilikuwa na uzito kuliko passport au degree ya chuo kikuu.

5. Tulifuta ujinga kitaifa tukiwa na chuo kikuu kimoja, lakini hivi sasa tuna vyuo vikuu zaidi ya 50 ila tuna wajinga wengi!

Ukiona wazee kama mimi tuna kumbukumbu nyingi kuliko ndoto za kesho, ujue kuwa kuna jambo lisilo sawa. Kutukanwa ni halali yangu maana nimepitwa na wakati. Nikiitwa mzee mzima ovyo nitakuwa nimependelewa.

What went wrong? Nini kilienda mrama?
 
Amenena Baba Askofu Dr Benson Bagonza ambaye ni mkuu wa Dayosisi ya KKKT Karagwe.

Kama una maswali, manung'uniko, mapovu, maoni, shukurani, nk - elekeza kwake Baba Askofu mwenyewe atakuhudumia kwa kadri ya mahitaji yako.

Shukurani nyingi sana kwako Baba Askofu Bagonza kwa mafundisho yako yenye upako wa kuponya roho na nafsi.


20200613_195113.jpg
 
Kwa hiyo anataka turudie kadi ya CCM yenye uzito kuliko Pasipoti?

Low IQ!
 
Sana Mkuu miaka mingine 5 ndiyo basi tena ndiyo sababu hata Mkapa akataka Tume huru ya uchaguzi kwa kujua hachomoki kwenye uchaguzi huru na wa haki. Dikteta kajifanya kama hakumsikia Mkapa yuko busy kupiitisha miswaada yake ya kidikteta kwenye Bunge lake.

ndani ya miaka 5 tu tumekuwa reduced into some piece of trash.
inaumiza sana kuona hata eti Wamalawi wanatudharau....
 
Kweli kabisa aisee. Ni aibu sana umenikumbusha rafiki yangu mmoja mbongo. Siku moja akaniambia akisikia jina la Tanzania anakasirika na kukosa amani moyoni kwa jinsi anavyochukia uovu unaozidi kushamiri Nchini.

Sometimes kusema ww ni mtanzania ukiwa mbele ya mataifa mbali mbali ni aibu sana..Ujinga umepitiliza ,ona yanayoendelea saivi na kidikiteta kinavotuendesha afu watu wako bungeni talking sh*t passing through sheria za kipuuzi puuzi
 
Back
Top Bottom