Baba wa Taifa na tatizo la Udini

Belo,
Tunaweza tukafanya mjadala wa adabu na heshima bila ya kejeli na kebehi.

Mathalan ukishanisoma na ukaona kuna jambo una fikra tofauti na zangu ukaeleza.

Sasa hii "kulia," na maneno ya kukashifiana yanatoa ladha ya mjadala.
Shikamoo Mzee Said. Hongera kwa uandishi wako kwa njia ya vitabu na makala.

Hongera pia kwa kutetea usawa katika jamii.

Mzee Said nimekuwa mfanyakazi wa umma sehemu mbalimbali, kiukweli sijawahi ona sehemu ambayo ilifanyika makusudi na viongozi au sekretariati ya ajira kutoajiri mtu kwa sababu ya dini yake. Kikubwa ni sifa ya mtu wala sio dini. Ungesema kabila na ukanda hapo tungekuelewa kidogo maana kuna baadhi ya taasisi huko nyuma (sio enzi hizi za sekretariati ya ajira) zilijaa watu wa kabila au kanda fulani.

Udini kidogo umeanza kurise kuanzia 2000s tena kwa baadhi ya taasisi.

Huko nyuma ni kweli kulikuwa na gap kubwa kati ya mkristo na muislamu (sababu kubwa ilikuwa elimu, kuna upande uliwekeza zaidi elimu ya dini kuliko elimu dunia), ila kwa sasa wengi wa vijana na watoto wa kitanzania wamesoma bila kujali dini wala kabila....hata jamii za waokota matunda na mizizi pamoja na wafugaji wako wengi kwenye mfumo wa elimu na ajira.

Hivyo, Mzee wangu tambua hilo gap la elimu lilivyokuwa huko nyuma ukizingatia taasisi nyingi za elimu zilikuwa chini ya dini fulani.
 
Mkoloni hakuona kuwa muislamu au mwarabu hakuona huyu mkristu aliona wote waafrika weusi .
Sisi ndio tumechanganyikiwa tunaangalia kwa dini. Hamna sehemu walienda kugombea uhuru kuwa uhuru wapewe waislamu au uhuru wapewe wakristu . Uhuru uliombwa wapewe waafrika watanganyika.

Mtu mzima kuingiza dini katika mazungumzo ya waafrika kuhusu kuendesha nchi ni kuchanganyikiwa

nampongeza sana baba wataifa kuliona hili na kulizuia ila bado majinga yanachochea dini ukabila.

tuache ujinga ndugu zangu watanzania
 
Hii inaleta mantiki na inaonesha kweli unafuatilia kwa karibu. Kuna sababu ya kulalamika...lakini bado pia acknowledge some of the factors kwa baadhi ya positions
 
Hii inaleta mantiki na inaonesha kweli unafuatilia kwa karibu. Kuna sababu ya kulalamika...lakini bado pia acknowledge some of the factors kwa baadhi ya positions
Hii ndio maana wazee kama hawa nyerere aliwapiga chini na nina furahi mtu kama huyu anapima watanzania kwa jicho la dini hafai katika jamii
 
Nauliza swali moja tu. Nyerere alipokewa na wazee wa dar au waislamu.?
Ada...
Hilo swali jibu lake lipo katika hotuba ya Mwalimu aliyotoa Ukumbi wa Diamond.

Itafute hotuba hiyo uisikilize kasema ni nani walimpokea Dar es Salaam.
 
Hii ndio maana wazee kama hawa nyerere aliwapiga chini na nina furahi mtu kama huyu anapima watanzania kwa jicho la dini hafai katika jamii
Ed...
Unaona sawa kuwa na 20:80?
 
Soine,
Hujui.

Na kama hujui ndiyo hujui.
Utasema kile ukijuacho.

Mimi najua na naeleza nikijuacho.
Hakuna tatizo.
 
Hongera sana.
 
Soine,
Sasa nakufahamisha.

Hali ilivyo katika serikali ni hii:

Wakristo wamehodhi 80%
Waislam 20%

Ukitaka maelezo zaidi nifahamishe nikuwekee mchanganuo.

Hili ndilo tatizo linalotukabili ulilokuwa hujui.
 
Key...
Majibu si mepesi kama unavyodhania.
Wazee wetu wamepigania uhuru wa nchi hii kuondoa udhalili.

Soma historia ya Waislam katika Maji Maji hadi siasa za TANU unakuja na habari za Wapagani.

Kuna Wapagani waliokuwa katika kupigania uhuru wa Tanganyika?

Au una picha hata kipande ya wachungaji wamepiga na Nyerere wakati wa ukombozi wa nchi hii?

Huna unachokijua katika tatizo hili.
Wanaostahili kujibu wako kimya.

Jitulize soma historia hii kwanza uielewe.
 
Historia yako unataka ianzie lini na wapi ? Nikikwambia kwamba wazee wetu waliteseka na hata huo udhalimu kuja baada ya hizi dini kuja na Merikebu takuwa ninakosea ?

Au ni mangapi yamefanywa kwa jina la hizi Imani ambazo kwa pande hizi za dunia ni Alien ?, Au ndio yale yale kwamba utamaduni wa mababu zetu ulikuwa ni wa kipumbavu na hizi Imani zilizokuja ndio ustaarabu ? Ni ajabu sana watu wanaoamini Binadamu wote ni sawa kuanza kudai kwamba wao wana Hati Miliki zaidi ya wengine...

Na ni nani alikwambia kwamba kujua Historia ndio kujua Mema na Mabaya ? Yaani sababu Waarabu waliwachukua Mababu zangu utumwani ndio leo niwachukie wajukuu zao ? Au unamaanishi nini nisome historia ili nielewe....

Samahani kama sielewi ila sijawahi kuona watu wanajenga kwa kubomoa na kutenga; Kwangu Umoja ni Nguvu na Umoja huo utapatikana kwa kushikilia umoja wetu na sio kutofautiana kwetu (Hizo Imani zibakie kwenye Mahekalu na Makanisa huku Kitaa Binadamu wote ni Sawa)
 
Key...
Ikiwa unataka tujadili historia ya utumwa vyema niko tayari.

Tuanze na Transatlantic Slave Trade.

Kisha tuingie Belgian Congo Slave Trade.

Karibu.
 
Key...
Ikiwa unataka tujadili historia ya utumwa vyema niko tayari.

Tuanze na Transatlantic Slave Trade.

Kisha tuingie Belgian Congo Slave Trade.

Karibu.
Belgian Congo slave trade ni tofauti na Transatlantic slave trade?
 
Naona unanadi kitabu chako kwa gia ya uislam
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…