Kesi ya Ugaidi kaitafuta yeye Mwenyewe Mbowe.
Mbona viongozi wenzake kina;
John Mnyika, Mrema, Benson kigaila, n.k "hawakupewa " kesi ya ugaidi?
Mbowe anavuna alicho kipanda mwenyewe.
Kama wazazi wake walisaidia kupigania Uhuru wa nchi hii basi yeye alipaswa kuwa mfano mzuri na mwema kwa nchi yake, alipaswa awe mzalendo wa kweli kwa nchi yake.
badala yake amekuwa msaliti na muovu dhidi ya Taifa lake mwenyewe,
amekuwa akiichonganisha nchi na mataifa mengine, amekuwa akihamasisha uvunjifu wa amani, amekuwa akiwahamasisha wafuasi wake kufanya vurugu na kuigomea Serikali, n.k.
Anawakosea sana hata wazazi wake ambao pia wanamchango wa kuijenga nchi hii.
Mkurugenzi wa Mawasiliano John Mrema alisema wazi kabisa alipo kuwa akizungumza na vyombo vya habari kuwa;
"huenda mwenyekiti alikuwa na mambo yake ya kisiri ambayo sisi wengine hatukuyajua....pengine alikuwa na handaki la silaha huko nyumbani kwake machame......sisi hatujui........" .
Mrema aliongea kiutu uzima sana na huku akizingatia kuwa Mbowe ni binaadamu sio malaika hivyo aliamini inawezekana Mbowe kutenda uhalifu bila wao kujua.