Mkuu, kuna mahali Mbowe amejisifu?! Baba wa taifa anasifiwa sana, mama Maria akiulizwa kumhusu mumewe ataelezea, na maelezo yoyote atakayotoa ni sifa tupende tusipende, watoto na watu waliokuwa karibu na Nyerere wakimuongelea ni sifa tayari hata kama hatupendi!
Binafsi sijui ni lini Mbowe alijisifu au kumsifia baba yake japo siyo kosa kufanya hivyo kama isivyo kosa kwa wewe ulivyomsifia mzazi wako hapa.
Pamoja na hivyo....kwa nini mnamuongelea Mbowe kama mwenye hatia tayari?! Huo ndio wema wenu mnaojisifia?!