Baba yake Mbowe kusaidia kudai Uhuru sio defence ya Mbowe kutofanya uhalifu, tutumie busara kujenga hoja

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2020
Posts
3,315
Reaction score
5,058
Mzee AIKAELI MBOWE na mkewe BI AISHI, na huyo dogo hapo mbele katikati yao ndiye FREEMAN MBOWE. Mzee AIKAELI alipambana Sana wakati wa kutafuta Uhuru wa TANGANYIKA na alimsaidia Sana NYERERE katika HARAKATI zao za Kudai UHURU wa NCHI hii,Leo UTAWALA wa mama umempa kesi ya UGAIDI https://t.co/6b6d55U0OA
 
Kuna Wengine Baba zetu wameifanyia makubwa Tanzania hii tena mpaka Kujitoa Mhanga kabisa kwa kuhatarisha Maisha yao Kiusalama kwa Kushirikiana na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ili Tanzania isimame kama ilivyosimama sasa lakini wala hatujisifu na hata Mzazi Mwenyewe nae hataki Sifa ( Kujikweza ) kama wengineo.

Kinachonishangaza kila nikimuuliza Mzee wangu ni kwanini hataki Kujionyesha na Kujisifu Hadharani kama wafanyavyo Wengine jibu ambalo huwa ananipa ni moja tu kuwa anaipenda Tanzania kuliko ajipendavyo Yeye na anajiona ni mwenye Faraja Kubwa mno Kushirikiana na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere katika Kuipambania Tanzania hii na nchi nyingi za Afrika Kiukombozi.

Na si Mzazi wangu tu pekee ila nina uhakika wapo pia Wazazi wa Watanzania Wengine wameifanyia makubwa na ya Kushukuriwa Tanzania hii kuliko hata huyu Baba yake Freeman Mbowe, lakini wala hawana Shobo na hawataki Kutukuzwa au Kuogopeka.

Halafu Uhalifu / Makosa ya Mbowe yanahusiana vipi na Mafanikio ya Baba katika Kuchangia Kuipambania Tanzania hii katika Ukombozi na Uhuru wake? Nilidhani kwa Heshima ya Baba yake Mbowe basi ndiyo angekuwa Raia mwema Tanzania ili awe mfano Bora kwa Kizazi hiki cha sasa ila imekuwa ni Kinyume.

Tanzania ni Kubwa kuliko Mbowe wenu.
 
Jamii haikosei. Sauti ya jamii ni sauti ya Mungu. Sauti hiyo inasema na sauti hiyo inamnyanyua Mbowe kwasababu ya matendo ya baba yake sauti hiyo hiyo inasema "Mbowe sio gaidi". Unajipa ukituko kupingana nayo na kujikweza kwako kusukojulikana weye na mzazi wako asiyejulikana na jamii hiyo hiyo
 
Kesi ya Ugaidi kaitafuta yeye Mwenyewe Mbowe.
Mbona viongozi wenzake kina;
John Mnyika, Mrema, Benson kigaila, n.k "hawakupewa " kesi ya ugaidi?
Mbowe anavuna alicho kipanda mwenyewe.
Kama wazazi wake walisaidia kupigania Uhuru wa nchi hii basi yeye alipaswa kuwa mfano mzuri na mwema kwa nchi yake, alipaswa awe mzalendo wa kweli kwa nchi yake.
badala yake amekuwa msaliti na muovu dhidi ya Taifa lake mwenyewe,
amekuwa akiichonganisha nchi na mataifa mengine, amekuwa akihamasisha uvunjifu wa amani, amekuwa akiwahamasisha wafuasi wake kufanya vurugu na kuigomea Serikali, n.k.
Anawakosea sana hata wazazi wake ambao pia wanamchango wa kuijenga nchi hii.

Mkurugenzi wa Mawasiliano John Mrema alisema wazi kabisa alipo kuwa akizungumza na vyombo vya habari kuwa;
"huenda mwenyekiti alikuwa na mambo yake ya kisiri ambayo sisi wengine hatukuyajua....pengine alikuwa na handaki la silaha huko nyumbani kwake machame......sisi hatujui........" .
Mrema aliongea kiutu uzima sana na huku akizingatia kuwa Mbowe ni binaadamu sio malaika hivyo aliamini inawezekana Mbowe kutenda uhalifu bila wao kujua.
 
Sasa hata kama hataki sifa wewe tu ungemtaja huyo baba yako hata kwa jina tu, kutokumtaja jina na kuongea bila evidence unataka tu kumdhalilisha tu Freeman Mbowe na wivu wako.
 
Gaidi Hamza Ni zao la CCM na matunda yake tumeyaona wote.
 
Mkuu huwa hauna utaratibu wa kutumia akili zako kwa uzuri.
Could you kindly keep quiet?
 
Sema babako alihatarisha maisha yake kukutafuta wewe na sio hizi porojo ulizoandika hapa
 
Nyerere alisaidiwa na watu wengi tu kuna wengine walimasaidia mpaka sehemu ya kulala na kula mpaka nguo za kuvaa sasa unataka Mbowe apambane na rais aachwe kisa baba yake alikuwa anajuana la Nyerere
 
Nyerere alisaidiwa na watu wengi tu kuna wengine walimasaidia mpaka sehemu ya kulala na kula mpaka nguo za kuvaa sasa unataka Mbowe apambane na rais aachwe kisa baba yake alikuwa anajuana la Nyerere
Ndio maana nawaambia wenzangu wawe na busara kujenga hoja.
 
Duh..K
 
Hii historia inayo mtaja babake Mbowe kwenye Uhuru imeandikwa wapi?
Nani ali verify?
 
Hoja yako ni nini sasa?kweni baba yake kupigania uhulu wa nchi kunazuia tamaa za mtoto wake dhidi ya madaraka na pesa?

WaTananzania wengi hua mna ukichaa
 
Hii historia feki ya baba wa mbowe kupigania uhuru imetokea wapi?
 
Kamanda mchovu,kwako wewe mawazo yako unaona ndio busara yako,kalale uchovu ukiisha urudi.
 
Mkuu, kuna mahali Mbowe amejisifu?! Baba wa taifa anasifiwa sana, mama Maria akiulizwa kumhusu mumewe ataelezea, na maelezo yoyote atakayotoa ni sifa tupende tusipende, watoto na watu waliokuwa karibu na Nyerere wakimuongelea ni sifa tayari hata kama hatupendi!
Binafsi sijui ni lini Mbowe alijisifu au kumsifia baba yake japo siyo kosa kufanya hivyo kama isivyo kosa kwa wewe ulivyomsifia mzazi wako hapa.
Pamoja na hivyo....kwa nini mnamuongelea Mbowe kama mwenye hatia tayari?! Huo ndio wema wenu mnaojisifia?!
 
Upo sahihi Mbowe hana tabia za kijinga hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…