Baba yangu hakuwa anawaamini watu. Alianza kunijengea tabia ya ubinafsi na kujitenga, nashukuru nilistuka mapema

Baba yangu hakuwa anawaamini watu. Alianza kunijengea tabia ya ubinafsi na kujitenga, nashukuru nilistuka mapema

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Nahisi mzee aliwahi kufanyiwa matukio kadhaa ya usaliti na walio wahi kuwa marafiki zake ama ni yeye mwenyewe hakuwa anachagua marafiki sahihi na hivyo kutendwa na wenzake.

Sote tunajua kwamba watu wapo wazuri na wabaya lakini hii sio sababu ya kumbana mtoto kuwakwepa kabisa watu kwa kumkinga tu na wale wabaya, mtoto ni advantage kwake kujua hata namna ya kuishi na watu kupitia watoto wenzake ili hata ukubwani akianza kuishi mbali basi awajue watu wabaya wa kukwepa na wazuri wa kuwa nao.

Huu uoga wake ulioingia kwa watu ndio akataka kuanza kunijengea mazingira ya mimi kutokuwa na marafiki hasa utotoni.

  • Alikuwa anakazia sana sana sana nisiwaamini watu, watu ni wabaya nisijenge ukaribu nao yani hata watoto wa rika langu
  • Alinikataza kuingiza marafiki hata iwe tunacheza kibarazani
  • Nilikuwa getikali ndani tu, hata kusema niende kucheza mpira na majirani hakuna,

Hii hali ilitaka kuniathiri sana kisaikolojia na pengine ningekuwa introvert,

  • Kwangu ilikuwa ngumu sana kujenga urafiki, rafiki ni moja na ni shuleni, namganda sana maana hakuna zaidi yake. nilikuwa najihisi vibaya akiwa na marafiki zake wengine maana mimi sina marafiki wengine.
  • Nilikuwa naonewa kirahisi
  • Sikujua michezo mingi sana ya utotoni
  • Nikipata mwanya kutoka nje watoto wengine walikuwa wananikatalia kwenda kwao sababu kwetu hawaingii
  • Mtaani nilikuwa sina urafiki na watoto wengine,

lakini nashukuru nilipata akili ya kuona maisha nayofundishwa sio ya kawaida, mzee nilikuwa namgomea wazi kabisa na nilikuwa nakula stiki za kutosha tu ial matunda nilianza kuyaona.
 
Mimi nipo kama baba ako,sipendag urafik kabisa
Maana rafik hachelew kukukopa hela na asirudishe,au kukuomba kausafir kako na kwenda kukapiga chini,mazoea zoea ya kipuuz

Ila ukiwa kama mzazi mtoto hutakiw kumzuia asitoke ndani ni vibaya sana,niliwah kuona familia moja walikuwa na watoto wawili kwanza wale watoto walichelewa sana kujua kuzungumza pia walikuwa kama mazezeta kidogo walivyoanza kwenda shule kidogo ndo wakaanza kuwa poa ila sio sana
 
Ni vema kuwalinda watoto lakini usiwanyime fursa ya kujua namna ya kuishi na watu,

Mtu usipojua kuishi na watu ni ngumu sana, mtoto hatajua kuna watu wabaya na wazuri atapata wakati mgumu kujifunza ukubwani.
 
Baba yangu alikuaga anapenda kunikosoa sana alikua ananiona mi ni mzembe kwenye kila kitu huku akisema yeye hakua kama Mimi
siku moja aliniuliza nina miaka mingapi nikamjibu miaka 12 ye akaniambia "nikiwa na umri kama wako nilikua na miaka 13" ili tu nimuone ye yuko vizuri zaidi yangu
 
Baba yako alikuwa ni mtu na nusu.Mbele mbele yako zaidi ya mbele.😂😂😂😂
 
Huwezi kuelewa mpaka yakukute
ni heri kujifunza mapema namna ya kuishi na watu.

Iliniharibu sana kisaikolojia kiasi hata kujenga urafiki ilikuwa ngumu na nikiwa na rafiki namganda sana
 
Hiyo ilikuwa hatari sana. Watoto wa kubanwa sana wanakuja kuharibika ukubwani wakipata uhuru. Inasikitisha kijana kuja kuharibikia Chuo. Unoko uliopitiliza sio mzuri.
 
Back
Top Bottom