Baba yangu hakuwa anawaamini watu. Alianza kunijengea tabia ya ubinafsi na kujitenga, nashukuru nilistuka mapema

Baba yangu hakuwa anawaamini watu. Alianza kunijengea tabia ya ubinafsi na kujitenga, nashukuru nilistuka mapema

Ni vema kuwalinda watoto lakini usiwanyime fursa ya kujua namna ya kuishi na watu,

Mtu usipojua kuishi na watu ni ngumu sana, mtoto hatajua kuna watu wabaya na wazuri atapata wakati mgumu kujifunza ukubwani.
Watu hawakupi mafasi ya wewe kuyajua hayo. Just watch out, utaumizwa vibaya. Hapo unarushiwa mchele kuelekea kwenye tenga, ngoja wategue tenga likufunike ndipo utajua.
 
Nahisi mzee aliwahi kufanyiwa matukio kadhaa ya usaliti na walio wahi kuwa marafiki zake ama ni yeye mwenyewe hakuwa anachagua marafiki sahihi na hivyo kutendwa na wenzake.

Sote tunajua kwamba watu wapo wazuri na wabaya lakini hii sio sababu ya kumbana mtoto kuwakwepa kabisa watu kwa kumkinga tu na wale wabaya, mtoto ni advantage kwake kujua hata namna ya kuishi na watu kupitia watoto wenzake ili hata ukubwani akianza kuishi mbali basi awajue watu wabaya wa kukwepa na wazuri wa kuwa nao.

Huu uoga wake ulioingia kwa watu ndio akataka kuanza kunijengea mazingira ya mimi kutokuwa na marafiki hasa utotoni.

  • Alikuwa anakazia sana sana sana nisiwaamini watu, watu ni wabaya nisijenge ukaribu nao yani hata watoto wa rika langu
  • Alinikataza kuingiza marafiki hata iwe tunacheza kibarazani
  • Nilikuwa getikali ndani tu, hata kusema niende kucheza mpira na majirani hakuna,

Hii hali ilitaka kuniathiri sana kisaikolojia na pengine ningekuwa introvert,

  • Kwangu ilikuwa ngumu sana kujenga urafiki, rafiki ni moja na ni shuleni, namganda sana maana hakuna zaidi yake. nilikuwa najihisi vibaya akiwa na marafiki zake wengine maana mimi sina marafiki wengine.
  • Nilikuwa naonewa kirahisi
  • Sikujua michezo mingi sana ya utotoni
  • Nikipata mwanya kutoka nje watoto wengine walikuwa wananikatalia kwenda kwao sababu kwetu hawaingii
  • Mtaani nilikuwa sina urafiki na watoto wengine,

lakini nashukuru nilipata akili ya kuona maisha nayofundishwa sio ya kawaida, mzee nilikuwa namgomea wazi kabisa na nilikuwa nakula stiki za kutosha tu ial matunda nilianza kuyaona.
Hapo haujastuka wala nini, hapo umekaidi. Watu siyo wa kuwaamini, wengine wanakutia ubovu leo just uje ku sufffer 20 years later.
Watu ni ni wa kucheka nao kinafiki tu, siyo wa kula nao wala kulala nao.

Utakuja kumkumbuka baba yako.
 
ni heri kujifunza mapema namna ya kuishi na watu.

Iliniharibu sana kisaikolojia kiasi hata kujenga urafiki ilikuwa ngumu na nikiwa na rafiki namganda sana
Ninauhakika baba yako alikugundua mapema Kama asinge ku restrain Kama vile huenda ungepoteana mazima na kuharibikiwa kabisaaa,mzazi yeyote humoma mtt mapema kabisa ,Kuna watt Wana akili za kujitambua mapema mno yaani bado mtt tu lakini tayari ameahajitambua nn anapaswa kufanya na nn hapaswi kufanya ,yaani unakuta mtt humwambii ajisomee lkn unamkuta Yuko bize anajisomea ,humwambii adamke mapema kwenda shule lkn anadamka mapema na kujiandaa kwenda shule ,yaani hahitaji assistance ya kuambia nn Cha kufanya,lkn Kuna mtt mingine usipo ifuatilia umekula hasara,yaani atajichanganya na wahuni na mitabia ya ajabuajabu ,hivyo naamini baba yako alikugundua wewe ukipewa Uhuru utapotea mazima.so yr father was right.
 
Watoto wa Uswahilini

Tuliishi gud tym sana ile kujichanganya na watoto mtaa wa pili mara kucheza chandimu ,mara kuwinda ndege porini , Dah michezo mingine ilikuwa ni ya hatari sana,

Lakini ndio hivyo Mungu alitulinda, getinkali ngumu sana kuelewa hizo pigo😁
Yale ndo maisha bro. Ingawa vipigo kwa wazazi na shuleni ilikuwa karibu kila siku. Mimi hadi kanisani tukienda mafundisho jumamosi kuna padri alikuwa akitupa adhabu kama zote. Yaani hakuna sehemu ilikuwa salama.. lakini pamoja na yote nilifurahia sana utoto wangu. Nakumbuka kuna siku kwenye ile michezo ya kibaba na mama nikataka nifanye kweli nikaishia kufumwa na mama wa binti.. yule mama alinipa kipigo kitakatifu kiasi kwamba nakuja kuonja utamu wa papuchi niko chuo mwaka wa pili.
 
Ninauhakika baba yako alikugundua mapema Kama asinge ku restrain Kama vile huenda ungepoteana mazima na kuharibikiwa kabisaaa,mzazi yeyote humoma mtt mapema kabisa ,Kuna watt Wana akili za kujitambua mapema mno yaani bado mtt tu lakini tayari ameahajitambua nn anapaswa kufanya na nn hapaswi kufanya ,yaani unakuta mtt humwambii ajisomee lkn unamkuta Yuko bize anajisomea ,humwambii adamke mapema kwenda shule lkn anadamka mapema na kujiandaa kwenda shule ,yaani hahitaji assistance ya kuambia nn Cha kufanya,lkn Kuna mtt mingine usipo ifuatilia umekula hasara,yaani atajichanganya na wahuni na mitabia ya ajabuajabu ,hivyo naamini baba yako alikugundua wewe ukipewa Uhuru utapotea mazima.so yr father was right.
nilikuwa najitambua vizuri tu wala sikuwa na shida.
 
Baada ya kupitia Baadhi ya comment nimegundua msimamo wngu sio mbaya, maana mwanzo nilikuwa na marafiki siku moja tumetulia maeneo Mara wazee wakatimba,tukaokotwa wote haibu mzee mpaka home, kumbe wenzetu wawiliwanajihusha na ujambazi Nami nikawa na Jina ilo kwa muda mrefu, nilisota kuizima iyo kesi, nilikoma
Matukio mengine ni kupigana mizinga kwamba atairudsha Anza kui dai Sasa uone rangi ya Rafik
Wengine unaheshimiana nao sana namuona kama ndugu ukisafiri tu basi ni kumtongoza, shemeji yao
Aya vipindi kama hivi vya mvua gari, inaharibika sana chini nikimaanisha zinagonga sana so sevis ni Mara kwa Mara mtu anafuruliza kuomba round akirudisha ni kesho asubui gari zinagonga balaa na pacha juu ndani ya gari Unakutana na mabak ya kike usiombe watoto ndo wameingia kuiangalia video ndani ya gari wa nakutana na chupi imefinyangwa pembeni ya siti,, sipendi hata kuendelea Kuya Ongea kwani ninayo andika ya ekwisha nitokea
Naapa nipo chumba tu mpaka nimeyazoe haaya maisha ya upweke
Ila pia kuna shida upande mwingine wa haya maisha nitaeleza siku nyingine
Lakini toka nijitenge nimepata maendeleo makubwa tofauti na kipindi kile pia kuna Amani ndani ya nyumba yangu
 
Now day Sina rafiki hata mmoja lkn wa kupiga nao stori mbili tatu hao wapo! Pia sipendi kujichanganya changanya na watu!

Kipindi Cha nyuma kidogo nilikua na rafiki tulie shibana sana lkn jamaa alikua akitongoza mademu zangu kwa Siri na wengine kupita nao kbs ( hiyo nilikua secondary)
Pengine sikuona athali kubwa kwenye hayo alokua akinifanyia rafiki yangu kwa sababu nilikua Bado mdogo. Now day waga nayafikilia sana matukio hayo na yanifanya nisiwe interested na marafiki.

Haya rafiki mwingine tulikutana ukubwani tu ktk hangaika ya maisha hapa mjini ( tumetoka sehemu Moja huko mkoani)

Mimi nikiwa na familia tayari lkn jamaa alikua mwaka wa mwisho chuo flani. Basi tukawa marafiki wa kushibana! Lkn end of the story jamaa alinitapeli pesa yangu na kutokomea baada ya kumkopesha ili nae akaanzishe biashara.

Hua najiuliza kama jamaa aliweza kunizulumu pesa zangu hivi angeshindwa kutembea na mke wangu kweli? Na hatimae kunivulugia familia? Mtu wa namna hiyo anashindwa kukumaliza kweli ili apate pesa?

So kwa matukio kama hayo yalionipata mm mwenyewe na mengine nayoyasikia na kuyashudia kwa wengine kuhusu kuwaamini watu na kuwafanya marafiki najikuta sitaki kuzoeana na mtu!
Salamu sawa! Stori mbili tatu imeisha hiyo.

Japo kwa wanangu siwezi kuwazuia kuwa na marafiki au kucheza na wenzao, ila wakishajielewa lazima niwape ABC za walimwengu ili wachukue tahathali nao.

Hivi huwa najiuliza mtu anaanzaje kuchukUa pesa ya mtu au kitu cha mtu alaf asirudishe alaf awe comfortable kabisa wakati mimi kuchukua tu kitu cha mtu na kukaa nacho tu nahisi kuumwa yan nafsi inasumbuka sana na kuhangaika kama nikikopa alaf nikadaiwa na mtu
 
We acha tu ndgu yangu wengine mishipa ya aibu ishakatika
 
Baba yangu alikuaga anapenda kunikosoa sana alikua ananiona mi ni mzembe kwenye kila kitu huku akisema yeye hakua kama Mimi
siku moja aliniuliza nina miaka mingapi nikamjibu miaka 12 ye akaniambia "nikiwa na umri kama wako nilikua na miaka 13" ili tu nimuone ye yuko vizuri zaidi yangu
😂😂😂😂
 
[emoji23][emoji1787]
 
Back
Top Bottom