Baba yangu hakuwa anawaamini watu. Alianza kunijengea tabia ya ubinafsi na kujitenga, nashukuru nilistuka mapema

Mimi nimelelewa hivo huwa sina rafiki aisee. Nikiwa naye ni mmoja tu. Kwenye relation nipo hivo kama wewe huwa siachiki kirahisi, pia nimelea wanangu hivo. Hakuna marafiki, hakuna kuzurura sababu na mimi nililelewa geti kali
 
Hiyo ilikuwa hatari sana. Watoto wa kubanwa sana wanakuja kuharibika ukubwani wakipata uhuru. Inasikitisha kijana kuja kuharibikia Chuo. Unoko uliopitiliza sio mzuri.
Inatakiwa umbane mtoto kwa akili.Chezea akili yake ili aelewe unacholisha akili yake.Uhuru ukizidi ni hatari.Familia ni kama nchi.Unapaswa uitawale.
 
Watoto wa Uswahilini
Hiyo ilikuwa hatari sana. Watoto wa kubanwa sana wanakuja kuharibika ukubwani wakipata uhuru. Inasikitisha kijana kuja kuharibikia Chuo. Unoko uliopitiliza sio mzuri.
Tuliishi gud tym sana ile kujichanganya na watoto mtaa wa pili mara kucheza chandimu ,mara kuwinda ndege porini , Dah michezo mingine ilikuwa ni ya hatari sana,

Lakini ndio hivyo Mungu alitulinda, getinkali ngumu sana kuelewa hizo pigo😁
 
Mimi nimelelewa hivo huwa sina rafiki aisee. Nikiwa naye ni mmoja tu. Kwenye relation nipo hivo kama wewe huwa siachiki kirahisi, pia nimelea wanangu hivo. Hakuna marafiki, hakuna kuzurura sababu na mimi nililelewa geti kali
Watu ndio wametuzunguka na mambo mengi tunawategemea watu, kumbana mtoto asijue namna ya kuishi na watu ni mbaya. Ni watu hawa hawa ambao ukiishi nao vizuri hata kama si marafiki unaweza kupewa connection za kazi au biashara, kusaidiwa kwenye matatizo, n.k.

Lakini unapombana mtoto pia inakuwa kazi kwake kuujua upande negative wa watu na jinsi ya kujua namna ya kudeal nao, mfano marafiki feki, wanafki, waongo n.k. hawa ni muhimu kujua tabia zao ili kuwagundua mapema na kujua namna ya kuishi nao na kuwakwepa.
 
Mzazi anaweza kuwa sahihi lakini makosa mengi ya wazazi wengine ni kuwa
Wanawakataza kutoka au kuwa na marafiki bila kutoa sababu na hiyo inamchanganya mtoto

Mzazi lazima amuambie ukweli mtoto bila kupepesa macho kuwa huko nje Kuna watoto watukutu jihadhari nao wasikufundishe mambo ya kijinga au yasiokuwa ya kimaadili

Wengi wanaanza kujaribu vitu vingi wakiwa watoto wadogo sana tena hata chini ya miaka 10 wanaanza kuvuta sigara, na kuanza hata ngono na bangi

Wakiendelea kuwa na marafiki wa hivyo mwisho wanaanza na pombe na kama ni visichana na umalaya juu

Mzazi lazima ajue anamuelekeza njia sahihi mtoto kwa kumfundisha mema tu na kumkataza maovu

Wazazi wengi wanajua kupiga tu badala ya kuwaweka karibu watoto
Mzazi anaingia nyumbani unajua adui kaingia sio baba

Baba humuoni anatembea na wanae akiwa mapumziko
Mungu atusaidie kuna mengi sana ya kuwafundisha watoto na sio kuwazuia tu
 
Mzee wako alikuwa sahihi , kwenye maisha usipende kuzoea zoea watu kiboya
kwenye maisha ni muhimu kujua kuishi na watu. ukijua tabia za mtu mnafki, feki, muongo unakaa nae pembeni lakini ili uweze kufanya hivyo inabidi uwe unawajua watu.

Pia kwenye maisha ni watu hawa hawa ukijua namna ya kuishi nao wapo wanaoweza kuwa msaada kwako kwenye kukupa connection za kukupa michongo na kukutoa kwenye shida. hata polisi unaweza usiwe rafiki nae ila ile kujuana tu hata kwa mbali anaweza kukusaidia kwa kiasi chake kuliko kama hamjuani hata kidogo.
 
Now day Sina rafiki hata mmoja lkn wa kupiga nao stori mbili tatu hao wapo! Pia sipendi kujichanganya changanya na watu!

Kipindi Cha nyuma kidogo nilikua na rafiki tulie shibana sana lkn jamaa alikua akitongoza mademu zangu kwa Siri na wengine kupita nao kbs ( hiyo nilikua secondary)
Pengine sikuona athali kubwa kwenye hayo alokua akinifanyia rafiki yangu kwa sababu nilikua Bado mdogo. Now day waga nayafikilia sana matukio hayo na yanifanya nisiwe interested na marafiki.

Haya rafiki mwingine tulikutana ukubwani tu ktk hangaika ya maisha hapa mjini ( tumetoka sehemu Moja huko mkoani)

Mimi nikiwa na familia tayari lkn jamaa alikua mwaka wa mwisho chuo flani. Basi tukawa marafiki wa kushibana! Lkn end of the story jamaa alinitapeli pesa yangu na kutokomea baada ya kumkopesha ili nae akaanzishe biashara.

Hua najiuliza kama jamaa aliweza kunizulumu pesa zangu hivi angeshindwa kutembea na mke wangu kweli? Na hatimae kunivulugia familia? Mtu wa namna hiyo anashindwa kukumaliza kweli ili apate pesa?

So kwa matukio kama hayo yalionipata mm mwenyewe na mengine nayoyasikia na kuyashudia kwa wengine kuhusu kuwaamini watu na kuwafanya marafiki najikuta sitaki kuzoeana na mtu!
Salamu sawa! Stori mbili tatu imeisha hiyo.

Japo kwa wanangu siwezi kuwazuia kuwa na marafiki au kucheza na wenzao, ila wakishajielewa lazima niwape ABC za walimwengu ili wachukue tahathali nao.
 
matunda gani uliyoanza kuyaona
-kufata ya mzee
-au kufata ya kwako
 
Babako amegraduate chuo kikuu cha maisha, Watu wanaokuibia, kukusaliti, kikuumiza, kukutapeli na hata wanaweza kukuua ni marafiki. Binafsi sinaga marafiki and i love it.

Usiiruhusu watu wakujue sana. Kuna jamaa kaibiwa naishi nae kwenye compound moja alimwambia rafiki yake wa damu anasafiri, akampigia boda (rafiki mwingine) aje amfuate alfajiri ili akapande bus anarudi anakuta nyumba nyeupe kaibiwa kila kitu. Mimi nasafiri hata miezi hakuna mtu anajua nipo au sipo na hakuna anesogea hata kuchungulia kwangu.

Epuka marafiki ni hatari.
 
Sasa mkuu ndo uwabane kabisa watoto hata wasicheze na watoto wenzao kufurahia utoto na kuwabana kiasi hata cha kukosa hata watu (si lazima marafiki) wa kupiga nao story ?

Yani hata wakikwama huko njiani hawana hata skills za ku interract na watu kuomba kupata msaada.
 

Ikawaje [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Watoto hawana shida hawajui bado maisha ni nini lakini ni muhimu kuwa- alert wanapokuwa watu wazima.
 
Still bado huja ijua dunia ilivyo na walimwengu wake,utajua baadae your father was correctly right
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…