Baba yangu kachomwa nusu kaputi Jumatano hajazinduka mpaka leo, bado yupo ICU

Alikuwa na tatizo la pressure kabla ya operation? Je alipimwa ufanyaji kazi wa figo zake kabla? Na majibu ya vipimo hivo yalikuwa aje? Hali ya baba ako kabla ya operation hiyo ipoje? Na alikuwa anafanyiwa upasuaji wa kitu gani?
 
Pole sana mkuu mgonjwa wake hakupimwa vizuri kabla ya hiyo,
Kwa hiyo anaweza kufa au laaah cha msingi kama bado ananafasi ya kuishi ataishi
Lakin kama nafasi imeisha atakufa.
Kwa hiyo uwe na matokeo mawili
Ila kwa uekewa wangu kama ameekaa siku zote hizo
Huenda akapona
 
Nakumbuka vannesa mdee alihojiwa akasema Baba yake alikufa sababu ya uzembe wa madaktari kumpiga sindano za ganzi bila vipimo wakati akifanyiwa operation ndogo tena hapohapo KCMC. Same shida imemtokea Baba yako
 
Mwenyezi Mungu ampe shifa.
Hatuwezi jua labda walizidisha dozi, au alipatwa na pressure kabla ya sindano.

Tumuombee tu Mungu
 
Nakumbuka vannesa mdee alihojiwa akasema Baba yake alikufa sababu ya uzembe wa madaktari kumpiga sindano za ganzi bila vipimo wakati akifanyiwa operation ndogo tena hapohapo KCMC. Same shida imemtokea Baba yako
Ni kawaida; ndugu wa mgonjwa siku zote hakubali kuwa mauti ni haki ya mwanadamu. Kila kifo ndugu wa mgonjwa huwa hawakosi pa kusukumia lawama zao. Utasikia mara overdose, mara hakupewa huduma haraka, mara hivi mara vile ili mradi tu hakosi sababu ya kusingizia. Kifo ni kifo tu, usipokufa leo utakufa kesho!
 
Nakumbuka vannesa mdee alihojiwa akasema Baba yake alikufa sababu ya uzembe wa madaktari kumpiga sindano za ganzi bila vipimo wakati akifanyiwa operation ndogo tena hapohapo KCMC. Same shida imemtokea Baba yako
Wangekuwa Ulaya au Marekani lawsuit ya medical malpractice hapo ni mamilioni ya dola. Lakini hapa kwetu daktari anakuulia ndugu yako hivi hivi na huna la kufanya. Huyo anesthesiologist ana kesi ya kujibu!
 
Kuna uwezekano hamkutoa maelezo sahihi ya magonjwa aliyonayo hasa pressure maana niliwahi kushuhudia mtu kachomwa hiyo sindano akazimia kwa siku tatu after then akazinduka na alitibiwa akapona hadi leo yupo.
 

Hoja ya kizembe kabisa hii. Ndiyo tunajua kuwa sote tutakufa lakini hatukubali vifo ambayo vinatokana na uzembe na vinavyoweza kuzuilika. Dereva aendeshe kiholela aue abiria halafu tukae tu na kusema kifo ni kifo tu? Hii ndiyo tofauti yetu na wazungu na waasia. Wenzetu wanajitahidi sana katika kuzuia kwa sababu wanajua kwa vitendo kuwa kuzuia ni bora kuliko kuponya. Leo hii acha tetemeko la ardhi la 7.5 litokee Haiti na Japan halafu kaa uangalie idadi ya vifo. Haiti watakufa laki saba lakini Japan pengine watakufa 200 pamoja na kuwa na population kubwa. Kwa nini? Kifo ni kifo tu my foot!
 
ALLAH atamfanyia ahueni inshaallah atapata nafuu kwa uwezo wake jalia
 
ma dr wana siri yaan wanaweza Kuku aka ms wewe ambae sio dr ukaona makosa ni yao. anyway pole bwana yesu anaweza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…