Baba yangu kachomwa nusu kaputi Jumatano hajazinduka mpaka leo, bado yupo ICU

Baba yangu kachomwa nusu kaputi Jumatano hajazinduka mpaka leo, bado yupo ICU

Pole sana Manka, Mungu amuweke mahali pema peponi baba yetu!
 
  • Thanks
Reactions: RWE
Oooh masikini pole my dia.May his soul rest in peace baba yetu mpendwa
 
Ndugu wanajamii forum baba yangu alikuwa afanyiwe upasuaji mdogo kwenye ziwa kulikuwa kuna uvimbe alipochomwa sindano ya nusu kaputi mapigo ya moyo yakasimama ghafla na akapoteza fahamu toka jumatano asubuhi yupo icu hajitambui anapumulia mashine!tukiwauliza madaktari hawana majibu sahihi!swali langu nikwamba atakuwa amepata tatizo gani?naombeni ushauri wenu kwayoyote anayejua ishu kama hii!natanguliza shukrani.
jamani pole mkuu nimekuja kuuliza vipi .. alale kwa amani
 
Wapendwa Mungu kampenda zaidi baba yangu
Pole sana ndugu...Mungu akutie moyo wa ujasiri ili uweze kupita salama kipindi hiki kigumu. Hiyo ndiyo njia yetu sote, tunapishana muda tu. Pole sana Manka.
 
Pole Sana Mkuu, umoja katika familia Ni muhimu sana kama Mzee alivyowalea kwa nguvu zake Basi bakieni wamoja daima.
 
pole sana mkuu may his soul rest in peace kikubwa usimlaumu sana madaktari kwa yaliyowakuta mpeni sifa na utukufu Mungu wetu
 
Kwake tumetoka na kwake ndio marejeo yetu,

Pole sana kwa msiba mzito Manka.
 
Mungu ndiye mwenye enzi yote na mamlaka, madaktari nao humtegemea yeye maana ndiye mponyaji mkuu
 
Pole sana ndugu. Umenikumbusha mbali sana, mzazi mwezangu nyuzi zilifumka akiwa na mwezi amefanyiwa operation ya uzazi, damu zilikuwa nyingi, nafika hospital Dr. anaagiza apelekwe ICU, aisee nilikuwa nikiagizwa kifaa sijui nilikuwa natembea kama jini kuwahisha mahitaji. Mungu ni mwema atazinduka tu.
 
Oh men, thats so sad. Pole sana naomba kwa dhati Mungu awe mfariji wenu na kuwapa tumaini pole Sana Manka
 
Back
Top Bottom