Baba yetu amefariki lakini hakuacha wosia wowote

ashomile

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
2,739
Reaction score
2,697
Historia kwa ufupi.

Mzee wangu alioa mke wa kwanza na alikuwa amejenga nyumba kubwa na ndogo na akabahatika kuzaa nae watoto wanne wote wakiume (04).

Baada ya hapo waliaachana na mama yangu mzazi kwa sababu mama yangu aliugua sana akamtibisha bila kupata auhueni.

Ilipofika mwaka 2002 alioa mke wapili wakaishi nae hapa kijijini kwetu kwa muda mfupi na baada ya hapo walihamia mjini na huko mjini waliondoka tayari mtoto wakwanza akiwa ashazaliwa tayari , walipoenda mjini walinunua kiwanja na kubahatika kuzaa nae watoto sita (6)wote kwa ujumla upande wa mama mdogo, wakike wanne (04) na wakiume wawili (02).

Huko mjini walinunua kiwanja na wakajenga nyumba ya kuishi , pia wkt wa uhai wao walijenga msingi wa nyumba kubwana ipo mjini katikati .

Ilipofika tarehe 13.07.2021 nilipata taarifa baba yangu katangulia mbele za haki kwa ajali ya moto na mama mdogo pia yuko khali mbaya sana naye ilipofika tarehe 17.07.2021 akafariki pia.

Kibaya zaidi mzee wangu hakuacha usia wa aina yoyote.

Pia wakati tumeweka majadiliano ya kuwalea watoto wadogo waliobakia tulisema shina la watoto wote wa marehemu ni hapa kijijini.

Je wale watoto wa Ma. Mdogo wana uwezo wakusema kiwanja cha kule mjini kiuzwe kwa ajili ya kuwasaidia? Na Je wakiuza wanaruhusiwa kuja kwenye nyumba aliyojenga baba yetu kijijini enzi yupo na mke wa kwanza ?

Pia naombeni ushauri wenu wakisheria zaidi.
 
Majibu ya maswali yako yote yanatakiwa yatolewe na mahakama.
Hata kisheria nikifahamu itapendeza zaidi , mimi na wadogo zangu sina makuu nao , kama sheria itaruhusu wauze kule mjini kwa sababu wamezaliwa kule na wakaishi kule mpaka kifo cha wazazi ,wala haina shida na sisi wa kwa upande wa mke wa kwanza tubakie na kiwanja cha kijijini na nyumba zakijijini siyo vibaya kikubwa tu wasijaribu kuja kuishi huku wala kuomba kiwanja maana watakuwa wameweka utengano.
 
Kwa nini unataka wauze eneo la kuishi?Wao wataishi wapi?
 
Fanyeni hivi Mali za mjini jadilianeni kwa pamoja ..
Watoto Wana haki na mali zote za Baba Yao
But Mama yako yuko hai??
Mimi ni mtoto kwa upande wa mke wa kwanza , mama yangu yupo hai lakini ni mgonjwa mpaka sasa. Ila kama nilivyoeleza hapo juu kwenye Uzi upande wa wadogo zetu na mama yao nae katangulia mbele za haki.
 
Kama baba yako na mama yako waliachana kwa talaka manake mali za mjini hazimhusu kaka hawakuachana kwa talaka nadhani kuna majadiliano ila hili jambo linahitaji mwanasheria chukua hela uende kwa mwanasheria ukapate ushauri wa kitaalam nenda kwa wanasheria hata wawili tofauti tofauti ili uwe na uhakika
 
Poleni saana kwa majanga ila kwa manufaa ya sasa na kizazi kijacho hili swala ungelipeleka mahakamani wataalamu waliamue kwa utaalamu wa juu na kuliweka kwenye documents za kudumu ili hata ao watoto wakija kukua wasijeleta Taharuki kwamba walidhurumiwa
 
Kwanini muuze kiwanja mjini, nyie watoto hamnazo kweli kweri
Hatujaelewana nadhani , maana yangu ni kwamba wale watoto wa mke wapili wakishawishiwa kuuzwa kiwanja chao je , sisi kama watoto wa wakubwa wa marehemu tuna pingamizi? Binafsi nilitamani tupaendeleze mjini ikiwezekana tuwe wamoja mwenye pesa apaendeleze kwa kujenga nyumba lkn iwe asset yakuwasaidia ambao bado ni watoto wadogo .
 
Mimi ni mtoto kwa upande wa mke wa kwanza , mama yangu yupo hai lakini ni mgonjwa mpaka sasa. Ila kama nilivyoeleza hapo juu kwenye Uzi upande wa wadogo zetu na mama yao nae katangulia mbele za haki.
Hicho kiwanja waachieni wadogo zenu maana baba yenu alichuma na mama yao na sio mama Yenu
 
Hata kisheria nikifahamu itapendeza zaidi , mimi na wadogo zangu sina makuu nao , kama sheria itaruhusu wauze kule mjini kwa sababu wamezaliwa kule na wakaishi kule mpaka kifo cha wazazi ,wala haina shida na sisi wa kwa upande wa mke wa kwanza tubakie na kiwanja cha kijijini na nyumba zakijijini siyo vibaya kikubwa tu wasijaribu kuja kuishi huku wala kuomba kiwanja maana watakuwa wameweka utengano.
Waafrika mna matatizo sana,hao ni ndugu zenu tena damu mmoja unaposema wasirudi huko kijijini sijui una manisha nini yani unataka Historian yao ifutike kabisa.
Haya Matatizo yote sababu ya umasikini.
 
Hatujaelewana nadhani , maana yangu ni kwamba wale watoto wa mke wapili wakishawishiwa kuuzwa kiwanja chao je , sisi kama watoto wa wakubwa wa marehemu tuna pingamizi? Binafsi nilitamani tupaendeleze mjini ikiwezekana tuwe wamoja mwenye pesa apaendeleze kwa kujenga nyumba lkn iwe asset yakuwasaidia ambao bado ni watoto wadogo .
Kwahyo hao wanataka kuuza hicho kiwanja?
Na Wana umri gani hao watoto?
 
Kama baba yako na mama yako waliachana kwa talaka manake mali za mjini hazimhusu kaka hawakuachana kwa talaka nadhani kuna majadiliano ila hili jambo linahitaji mwanasheria chukua hela uende kwa mwanasheria ukapate ushauri wa kitaalam nenda kwa wanasheria hata wawili tofauti tofauti ili uwe na uhakika
Hakuna talaka iliyotolewa , kama nilivyosema aliugua mama yangu na wakaachana nae .
 
Hicho kiwanja waachieni wadogo zenu maana baba yenu alichuma na mama yao na sio mama Yenu
Ukisema hivo tukiwaachia kiwanja wakauza alafu mwisho wasiku wakaja kuomba hifadhi huku kwetu itakuwaje ?

Maana bado wadogo sana na tukiwakubalia wauze lkn huku kwetu wasahau kabisa itawekana ?

Pia tambua baba yetu wakati anaoa mke wa pili chanzo kilianzia kwetu unalitambua hilo ?
 
Back
Top Bottom