Baba yetu amefariki lakini hakuacha wosia wowote

Mambo ya familia huwa yanajadiliwa nyumbani siyo jamii forums wewe ulilelewa wapi wewe ?
 
Pole sana Mkuu, maswali yako nitajitahidi kukujibu kwa mfumo wa maswali pia:

1. Baba yenu alikuwa anafuata mfumo gani wa maisha?, Nakuuliza hivi kwa sababu kwenye murathi kuna aina tatu za mfumo wa maisha ambayo ni:-

A. Mfumo wa kimila
B. Kikristu
C. Kiislamu

Sasa kama alifuata mfumo wa kimila mali zake zitagawanywa kwa mfumo au taratibu za kabila lenu, ila hapa kuna swala la ndia, sasa je alioa kimila?, na je ndoa zilisajiliwa?, na je alimtalaki mama yako?
Haya maswali muhimu kuyajibu ili tuelewe uelekeo wa kimfumo utaegemea bado hapa

Kama alifuata mfumo wa maisha ya kikristu, hapa ni kama alibatizwa/aliokoka na kuishi kwenye misingi ya dini za kikristu, huu mfumo utaleta utata kwenye hizi ndoa mbili endapo ta awali haikuwa na talaka. Ikumbukwe pia mfumo wa kikristu ndio mfumo unaoangaliana zaidi na sheria za kiserikali, sasa hapa ndoa ni ya mke mmoja, na hazifuatani mbili labda pawepo talaka, je talaka ipo?

Kama alifuata mfumo wa kiislamu, hapa utafuatwa ule utaratibu wa mgawanyo ulioelekezwa kwenye quorani, hapa ndoa zinaruhusiwa hadi nne hivyo kama hamna talaka na alioa kidini haitasumbua sana.

SASA, tuendelee hapo kwenye swala la mali kama wanaweza kuuza na kuja kuishi hapo kijijini.

Ipo hivi jambo muhimu kwanza ni kufanya vikao vya ukoo/familia ili mteue msimamizi wa mirathi hapo mtayajadili yote kwa maslahi ya watoto, hakikisheni mnajua nani atakuwa na jukumu la kuwalea hao watoto hii itategemea taratibu zenu inawezekana nyie wakubwa mkawaangalia wadogo zenu.

Msimamizi wa mirathi atafanya maombi mahakama ya mwanzo, kusipokuwa na mgogoro ni ahueni, ila hakikisheni mnajali maslahi ya watoto kwenye kikao maoema kabisa.

Swala la kuuza mali haliwezi kuamuliwa juu juu bila kuwepo msimamizi wa mirathi aliyeizinishwa na mahakama, mkiuza kiholela baadae mtapata migogoro ndugu.

Pia kila mtoto anayo haki ya kurithi mali za baba yake, swala ni kuzitambua mali za marehemu baba yenu ni zipi na hivyo kuzigawanya kwa taratibu sahihi.

Kila la kheri Mkuu. Ukiwa na swali usisite kuniuliza.
Karibu.
 
Naomba nikuulize, wewe unahitaji chochote kwenye hizo mali au una uwezo wako, unataka kuwasaidia wadogo zako?
Upande wangu sihitaji chochote lakini natamani mali za marehemu baba yangu zikiendelezwa na mpaka sasa mimi nina maisha yangu .
 
Waafrika mna matatizo sana,hao ni ndugu zenu tena damu mmoja unaposema wasirudi huko kijijini sijui una manisha nini yani unataka Historian yao ifutike kabisa.
Haya Matatizo yote sababu ya umasikini.
Mtoto wa mama mdogo na mtoto wa dada ndo una uhakika kwamba ni damu moja. Mtoto wa kaka na wa mama wa kambo huna uhakika yawezekana shemeji au mama wa kambo alichepuka. Ni ndugu kwa imani.
 
Nyie kama kaka wakubwa watunzeni wadogo Zenu,ila muwe makini sana katika mali zilichomwa na mama mdogo wenu,kama itabidi ziuzwe kuwasaidia Hawa wadogo Zenu,ni bora jambo hili lifsnyike kwa ushirikano na hao wadogo Zenu,na wajomba na mama zao wadogo na wakubwa bila hivyo,itaonekana mnataka kujinufaisha na hizo mali,
Mali huwa zinaleta changamoto sana,hata kama itabidi mgawane nguo za marehemu,gawaneni kwa usawa.
 
Upande wangu sihitaji chochote lakini natamani mali za marehemu baba yangu zikiendelezwa na mpaka sasa mimi nina maisha yangu .
Kaka fanyeni kikao cha ukoo/familia mteue msimamizi wa mirathi, ila pia muweke majukumu vizuri. Kisha mfanye maombi ya kumuizinisha msimamizi wa mirathi mahakamani.

Tofauti na hapo mtafanya ndivyo sivyo Mkuu.
 
Hicho kiwanja waachieni wadogo zenu maana baba yenu alichuma na mama yao na sio mama Yenu
Ukikaa kwenye nafasi ya huyu bwana, huwezi kufikiri hivi aisee. Najua anayopitia, tuna kesi ya namna hii iko mahakamani tangu 2015, hukumu inatoka, inapingwa, inatoka, inapingwa, mnasogezwa juu na juu zaidi, wapi! Watu wanaanza kupoteza maisha, mvurugano moja kwa yote.

Na bora hawa kwamba mali za baba alizochuma na mama wote. Watu wanagombea mpaka maeneo ya mke mkubwa ambayo alipewa na wazazi wake kabla ya ndoa, mke mdogo na watoto wake wanayataka hayo pia!

Mtoa mada, kuna vyeti vya ndoa kwa wake wote wawili? Wakati wapili anaolewa, zipi ni mali zilikuwepo? Na zipi ni mali zilizokuja baada ya ndoa ya pili?

Kulikuwa na maelewano mazuri baina ya watoto wote kabla ya mzee kufa?

Choreni mstari, kuna wakati haya mambo myamalize kindugu, kijamaa na kijamii, mahakama haziondoi kila mgogoro na zaidi zinavunja vingi!

Mwisho wa siku, kila kitu kinatafuta na kama kiko kwenye mkondo wako kitakuja tu! Kisicho ridhiki hakiriki.
 
Walipoachana na mama yako marehemu wote waliendelea kuishi na mtt wao kwenye nyumba ipi hapo kijijin??
Je mama yako na baba yako baada ya kutalikiana waligawana mali?
Mke mkubwa yupo hai km yupo hashai mali ya mjini hazimuhusu kwa kuwa hakushiriki kuzalisha au kuendeleza.
Mtoto ana haki ya kurithi mali za mzaz au wazazi wake.
Je kuna watoto wanosoma au wapo chini ya umri wa miaka 18
 
Mambo ya familia huwa yanajadiliwa nyumbani siyo jamii forums wewe ulilelewa wapi wewe ?
Hajaja kujadili kaja kuomba msaada wa kisheria. Wewe umejuaje kama kwao kuna mwanasheria, au nyie familia yenu ikipata changamoto ya kisheria mnakaa kikao kujadili solution wakati hakuna mtu hata mwenye certificate ya law
 
Hajaja kujadili kaja kuomba msaada wa kisheria. Wewe umejuaje kama kwao kuna mwanasheria, au nyie familia yenu ikipata changamoto ya kisheria mnakaa kikao kujadili solution wakati hakuna mtu hata mwenye certificate ya law
Hilo kwanza siyo suala la kisheria ni suala la kumaliza kwenye familia tu.

Suala dogo kama hilo unahitaji ushauri wa kisheria ?

Kwanini hakuenda kwenye ofisi ya wakili akapata ushauri mdogo tu ambao hauhitaji kuanika family affairs kwenye mitandao japokuwa anatumia fake identity ?
 
Kaka fanyeni kikao cha ukoo/familia mteue msimamizi wa mirathi, ila pia muweke majukumu vizuri. Kisha mfanye maombi ya kumuizinisha msimamizi wa mirathi mahakamani.

Tofauti na hapo mtafanya ndivyo sivyo Mkuu.
Mpaka sasa sielewi ila mkuu wa familia ndo kama msimamizi hakiwezi kufanyika chochote bila ya wao kuhusishwa.
 
Hapo ni ninyi wenyewe kukaa pamoja na kuelewana. Umeshasema hauna makuu basi busara itumike-waaachienj vyote alivyonunua au kujenga mzee wenu huko mjini akiwa na mke wake wa pili na ninyi mbaki kwenu na mali zenu kijijini. Hata haina haja ya kumsumbua mheshimiwa hakimu
 
Mnahangaika hivyo kwa sababu kama familia hamkutaka kuelewana kabla ya kwenda mahakamani huko.

Mirathi ni kitu kibaya sana unaweza kuzeeka unasumbuka na kesi ya mirathi na ukatumia gharama kubwa kuliko value ya kile unachokitafuta.

Mirathi lazima mkubaliane nyumbani tu vinginevyo endless kesi zisizo na maana zitawapotezea muda wa kufanya mambo mengine mwisho mnaishia kulogana na kukatana mapanga.
 
Mzee wangu alimuoa mama yangu kimila hivyo hakuna cheti cha ndoa ila kwa mke wa pili alifunga ndoa.

Kwa mke wa kwanza alikuwa tayari amejenga nyumba kubwa na ndogo .

Pamoja na viwanja vitatu .


Alipooa mke wa pili alinunua kiwanja vile vile na akajenga nyumba moja na msingi mmoja wa nyumba.

Pia sisi tulikuwa tunawatembelea wadogo zetu lkn wao kuja ilikuwa kwa msimu maana mama yao hakutaka watutembelee .
 
Walianzia kuishi hapa kijijini kwenye nyumba aliyojenga baba yangu na mama yangu mzazi baada ya hapo walihama wakiwa na mtoto mmoja tayari , hawakugawana mali .
 
Mpaka sasa sielewi ila mkuu wa familia ndo kama msimamizi hakiwezi kufanyika chochote bila ya wao kuhusishwa.
Mkuu, Msimamizi wa mirathi anaizinishwa na mahakama, na huyo msimamizi ni anachaguliwa tu na kikao cha ukoo)familia ila si lazima awe ni mzee wa ukoo/familia. Huyu anatakiwa kuwa tu mtu mzima anayejua maswala ya majukumu ya kifamilia.

Labda kama kuna ugomvi mwingine ambao upo kati yenu kaka ila kama haupo hichi kikao kinafanyika vizuri kabisa na ni lazima na muhimu.

Tofauti na hapo utaratibu mtakaofuata ni batili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…