Babu Seya/Papii Nguza kweli walibaka? Tukielekea kureview kesi yao oct 30

Kwa wale wasioamini kwamba Babu seya alionewa, kwa kawaida kila binadamu kaumbiwa nafsi ya kukiri kosa (Guilty Conscious) ndio maana kwa mfano mtu akishikwa ugoni hawezi kujibu mashambulizi kutoka kwa huyo aliyemfumania hata kama angekuwa anamzidi nguvu, hii ni kutokana na kwamba nafsi inamwambia ni kweli umekosa. Lakini hata kibaka hwa anakubali kichapo pale anapobambwa akikwapua tofauti na pale anapokuwa amesingiziwa atapambana kweli kujitetea.
Babu Seya licha ya kutoa walaka kupitia gazeti pendwa muda nmfupi kabla ya hukumu yake akielezea hatima ya kesi hiyo, tunaona tangu kutiwa hatiani ameendeleza mapambano kupinga hiyo hukumu, hii ndio namna ya mfungwa kuuelezea umma yanayomsibu kwakuwa hana uwezo wa kuitisha press conference.

Huu ndio uwe msukumo wa kutufanya kuamini kwamba alionewa, alibambikiwa kesi kama ilivyo jadi ya vyombo vya dola kutumiwa hovyo na wakubwa na itabakia kuwa anatumikia personal vendetta kwa huyo aliyemzulia kesi hii.
 
Ndio hivo tena nasikia ishapigwa tena kalenda..
 
NGUZA, KOCHA KUSOTA: Wakili wa Babu Seya, Papii Kocha aomba ushahidi ufutwe, waachiwe. Serikali yapinga. Korti ya Rufaa haijafanya uamuzi leo, yawapiga kalenda.

Mpaka lini tena.
 
Jelaaaaaaaa,,,,jela ni mbayaaaa

jelaaaaaaaaaa,,,jela ni matesooo..

Wanaokwenda jela sio wote wenye hatia


naamini mwenyezi mungu sio binadamu,,,,lolote linaweza kutokea katika hii kesi,,tuzidi kuwaombea
 
Qualified Dr hawezi ku testify nonsense. Procedure ya ku detect mtu aliyebaka au kulawiti ni on the spot au immediately after tendo sio wiki kadhaa baadae unakuta marks kwa mhanga halafu useme eti ni fulani! What if hao walio lay charge ndio waliwabaka hao watoto na kisha kupeleka michubuko kama ushahidi na wala sio sperms au other smears kutoka kwa mtuhumiwa babu seya?! Lakini niungane na aliyejiuliza swali hapo mwanzo kwamba baba na wanae wanachangia kulawiti watoto chumba kimoja sehemu moja kwa wakati mmoja je hayo ni maadili ya kiafrika kweli? je kama lilikuwa agizo la mganga wao wa kienyeji labda,je walipofikia sasa si wangekuwa wameshamtaja ili aungane nao katika kutumikia adhabu? kwanini hawafanyi hivyo na badala yake wanahangaika kuachiwa huru?!

Ninivyofahamu Dsm kuna kundi kubwa la wanawake wapenzi sana wa wanamziki wa bendi yaani ni waumini haswa wa wanamziki ndio maana kuna wanamziki baadhi wanalelewa kwa kupewa kila hitaji na wanawake fulani fulani hapa mjini, kwa babu seya na wanawe hawawezi kukosa bahati hiyo kiasi kwamba tusema ukame na udomo zege ndio uliwafanya kuparamia vitoto hivyo vilivyokuwa vinahongwa pipi na shilingi mia mbili kwa mujibu wa waendesha mashitaka na mashahidi wao.

Tunaweza kuchambua mengi sana ya kuonesha ujinga wa waliokuwa wanaendesha kesi hii bila kujua kuwa watanzania wana upeo wa kuchambua mambo na kuujua ukweli! ( Kwa taarifa tu Wakili yeyote ni Court Official ) yuko pale kuhakikisha haki inatendeka na sio kupendelea hata kama ni mteja wake. Haujiulizi kwanini mpaka leo wakili wa babu seya bado anapambana kumtoa jela??
 
kwa kuwa kesi yao ilipikwa na magogoni na chama cha walimu. mwalimu aliyetoa ushahidi yuko kagera anakula maisha na katibu mkuu cwt sasa anapeta tume ya katiba. hii ndo Tanzania

haikuwa chama cha waalimu bali mwl wa mkuu wa shule ya Mapambano na baada ya hapo alikula bata la CWT na majuzi ndio nimeanza kumwona kwenye tume ya Katiba.

Nijuavyo mimi uongo waliosingiziwa watu hawa lazima laana yake iwatafune walioshiriki ima kwenye maamuzi, imma kwenye ushahidi, imma kwenye kushtaki.
 
hakia MUNGU hawa walionewa tu.Siri yooooote pale Ikulu hata Jk analijua hili 100%.
 
Kama ni kweli walisingiziwa, ni nani alilawiti wale watoto? Nani aliwafundisha wale malaika kutoa ushahidi wa uongo mahakamani?
Tanzania unamaswali mengi sana hujayajibu!
 

"IMMA" ni jina la kampuni dada yangu angalia wasikushitaki
 
Mkuu mbona kuna Blog wameandika ameshatoka tayari? Mwenye taarifa sahihi atujuze.
 

Tanzania mabush lawyer ni wengi sana
 

watoto zaidi ya sita wengi wao wakiwa chini ya miaka 7 , karibu wote wanaogeshwa, wanafuliwa, kweli isigundulike walibakwa wote , hadi walipoanza kutoka usaha, yaani watoto wote hawakuumia, hawakutoka damu on the spot.

mtu mzima akiingiliwa bila ridhaa yake anaumia, inawezekanaje mtoto wa miaka chini ya saba asichechemeee !?

mbona matukio yote yakubakwa watoto issue hustukiwa soon na wazazi ?
 

Mkuu katika system tunayofuata (adversarial system) haitafuti ukweli bali inaangalia upande unaoweza kuleta ushahidi wa kutosha kudhibitisha au kukanusha mashtaka.

Inawezekana wahusika walitenda hilo kosa na wanastahili kuhukumiwa lakini Jamhuri lazima idhibitishe bila shaka kuwa walitenda hilo kosa.

Kama wahusika wanaweza ku-dispute ushahidi wa Jamhuri au kama mahakama ikikuta kuwa ushahidi wa Jamhuri unajichanganya au haujitoshelezi, basi wanaweza kuwachiwa huru hata kama walitenda hilo kosa.

Hii kesi ime-drag on kwa muda mrefu, imerudi mahakamani zaidi ya mara moja na pia imevutia umma kwa sababu ambazo hazieleweki.


Kama wahusika wanajua wazi moyoni mwao kuwa walitenda hilo kosa halafu wanakuja kuomba kuachiwa, then bado watahukumiwa kikamilifu na aliyeko juu yao. Roho zao lazima ziwasute.

Lakini kama kuna watu wameitengeneza au kujihusisha kwa namna yoyote ile kutengeneza hii kesi kwa sababu wanazozijua wao wenyewe, nao watahukumiwa kikamilifu na aliye juu yao. Roho zao lazima ziwasute.


Hivi hao watoto walikuwa na wazazi? Kama walikuwa na wazazi, hao wazazi hawaku-note kitu chochote kuhusiana na kubwa kwa hao watoto? Hivi hao watoto wana umri gani kwa sasa?
 
dah! hii kesi ina utata sana lakini mwisho wa siku malipo ni hapahapa duniani.
 
nitapataje hii kiboko ya paulina? Tafadhali nisaidie
 
Hivi wakitoka leo, itabidi waanze kujifunza kutumia simu na upya.
Walifungwa kipindi cha Phillips na Siemens, sasa hivi kuna Galaxy na iPhones. Mweh.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…