Babu Seya: Ufafanuzi juu ya uvumi unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii

Babu Seya: Ufafanuzi juu ya uvumi unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii

Joined
Jul 19, 2013
Posts
38
Reaction score
21
habari nilizozipata ivi punde zinasema babu seya kaachiliwa huru
naomba usibitisho jamani

==========

TAHADHARI:
UVUMI SI WA KWELI

Picha inayosambazwa kwenye mitandao ni ya Oktoba 2013 wakati wakitoka Mahakamani pia tetesi hizi si za kweli.

Kilichosambazwa na blogs nyingi ni mipango yao wakifika uraiani kama watatoka kwa msamaha wa Raisi ikiwa na kichwa cha habari kisichoakisi maelezo ya ndani kuvutia wasomaji


IMG_0161.JPG


Untitled.jpg

Hivi sasa kuna taarifa zimesambaa kupitia Ujumbe mfupi wa simu (SMS) na mitandao ya kijamii zikihusisha kuachiliwa huru kwa wafungwa wawili wanaotumikia Kifungo cha Maisha gerezani. Wafungwa hao wanaotajwa ni Nguza Vicking(Maarufu kwa jina Babu Seya) na Johnson Nguza(Maarufu kwa jina la Papii Kocha).

Napenda kuufahamisha Umma wa Watanzania kuwa taarifa hizo zote zilizotolewa kupitia njia hizo ni za Uongo na uzushi mkubwa na zinalenga kuipotosha jamii kwani wafungwa hao wapo gerezani na wanaendelea kutumikia adhabu ya kifungo cha Maisha gerezani kwa mujibu wa Sheria.

Jeshi la Magereza nchini linatoa onyo kali kwa watu kujiepusha na uhalifu huo na linawataka wale wote wanaotumiwa ujumbe wa aina hiyo waepuke kuusambaza ujumbe huo kwa wengine bali waufute, kwani kuendelea kuusambaza ni kosa kisheria.

Aidha, Jeshi la Magereza linaendelea na uchunguzi wa kina ili kuwabaini wanaosambaza ujumbe huo likishirikiana na Vyombo vingine muhimu kwa lengo la kuwakamata wahalifu hao ili mkondo wa Sheria uchukue nafasi yake.

Imetolewa na;

Lucas Mboje, Mkaguzi wa Magereza,

Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,

Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,

DAR ES SALAAM.

Septemba 8, 2014.


 
JK ndio kaanza kuaga kwa style hiyo kama hii habari ni ya kweli.
 
Huenda anataka kujisafisha katika jamii,lakini kasafiri mpaka anajishtukia hivi sasa,huenda hajui hali ilivyo tight huku kitaa,amesafiri mpka Singapole,ni nini tumepata kutokana na safari zake za kiuj.........
 
Nikirudi saa 10 jioni nikakuta uzi huu upo nitajua ni kweli!
 
Acha upumbavu wewe story za global waachie kina shigongo na wadaku wake usilete humu.. :angry::angry::angry::angry::angry:
 
Back
Top Bottom