Babu Seya: Ufafanuzi juu ya uvumi unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii

hatimae mwanamziki maarufu nguza viking na mwanae waachiwa huru

MUHIMU: Sasa unaweza kutuma picha za matukio/habari kupitia WhatsApp 0765 600009. Namba hii ni ya WhatsApp tu.
 
kuna uzi mwingine unao toa ufafanuzi juu ya jambo hilo humu ndani!! Ufafanuzi unadai jambo hilo ni uvumi tu!!
 
Ndugu wanajamvi habari zilizonifikia hivi punde kutoka chombo kimoja cha habari zinasema kuwa ndugu zetu papii Kocha na Babu Seya wako huru kwa kutokana na rufaa yao waliokata wakitetewa na Wakili Maarufu nchini MABERE MARANDO!! Naomba update zaidi wakuu?

Wewe jinga soma uzi wako pumba.vu
 
Kwa watu ambao hawakuwai kufatilia mwenendo wa hii case ndio anaweza kuamini hii habari!
Kwanza hiyo picha ina sign ya GPL sasa tunaomba mtwambie ni gazeti gani la Leo la GPL limetoa hiyo habari!
 
habari nilizozipata ivi punde zinasema babu seya kaachiliwa huru
naomba usibitisho jamani

==========
UVUMI SI WA KWELI
Picha inayosambazwa kwenye mitandao ni ya October wakati wakitoka Mahakamani pia tetesi hizi si za kweli.

Kilichosambazwa na blogs nyingi ni mipango yao wakifika uraiani kama watatoka kwa msamaha wa Raisi ikiwa na kichwa cha habari kisichoakisi maelezo ya ndani kuvutia wasomaji
 
Ww godfrey unachobisha n nn na unafahamu nn kuhusu msamaha

Katika orodha ya makosa yanayo weza kupata msamaha kosa lao halipo kabisa! Hii rufani ilikatwa tena lini? Kwa sababu zipi? Ilianza kusikilizwa lini?
 
habari nilizozipata ivi punde zinasema babu seya kaachiliwa huru
naomba usibitisho jamani

==========
UVUMI SI WA KWELI
Picha inayosambazwa kwenye mitandao ni ya October wakati wakitoka Mahakamani pia tetesi hizi si za kweli.

Kilichosambazwa na blogs nyingi ni mipango yao wakifika uraiani kama watatoka kwa msamaha wa Raisi ikiwa na kichwa cha habari kisichoakisi maelezo ya ndani kuvutia wasomaji

Kosa lao halina msamaha! Ni kifo tuu ndio kita watenganisha na gereza!
 
Hivi sasa kuna taarifa zimesambaa kupitia Ujumbe mfupi wa simu (SMS) na mitandao ya kijamii zikihusisha kuachiliwa huru kwa wafungwa wawili wanaotumikia Kifungo cha Maisha gerezani. Wafungwa hao wanaotajwa ni Nguza Vicking(Maarufu kwa jina Babu Seya) na Johnson Nguza(Maarufu kwa jina la Papii Kocha).

Napenda kuufahamisha Umma wa Watanzania kuwa taarifa hizo zote zilizotolewa kupitia njia hizo ni za Uongo na uzushi mkubwa na zinalenga kuipotosha jamii kwani wafungwa hao wapo gerezani na wanaendelea kutumikia adhabu ya kifungo cha Maisha gerezani kwa mujibu wa Sheria.

Jeshi la Magereza nchini linatoa onyo kali kwa watu kujiepusha na uhalifu huo na linawataka wale wote wanaotumiwa ujumbe wa aina hiyo waepuke kuusambaza ujumbe huo kwa wengine bali waufute, kwani kuendelea kuusambaza ni kosa kisheria.

Aidha, Jeshi la Magereza linaendelea na uchunguzi wa kina ili kuwabaini wanaosambaza ujumbe huo likishirikiana na Vyombo vingine muhimu kwa lengo la kuwakamata wahalifu hao ili mkondo wa Sheria uchukue nafasi yake.

Imetolewa na; Lucas Mboje, Mkaguzi wa Magereza, Afisa Habari wa Jeshi la Magereza, Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, DAR ES SALAAM. Septemba 8, 2014.
 
Hakuna kosa lisilosameheka duniani ni mangapi tunayomkosea Mungu na tukiomba tunasamehewa ? Mtoa hukumu n Muumba ila binaadamu tumejitwalia mamlaka zisizokuwa zetu kwa imeandika lililofungwa duniani na mbinguni limefungwa sasa binadamu ni nani hata ushindwe kusamehe? Ila kama wamesingiziwa malipo ni hapahapa duniani na chozi la mnyonge linalipwa na Mungu yetu macho.
 
Mimi nongea kutokana na sheria za nchi sio maswala ya kiroho!
Nimegundua Mimi nawe tuna ongea lugha tofauti! Wewe unaongea kihisia zaidi!
 
Hivi sasa kuna taarifa zimesambaa kupitia Ujumbe mfupi wa simu (SMS) na mitandao ya kijamii zikihusisha kuachiliwa huru kwa wafungwa wawili wanaotumikia Kifungo cha Maisha gerezani. Wafungwa hao wanaotajwa ni Nguza Vicking(Maarufu kwa jina Babu Seya) na Johnson Nguza(Maarufu kwa jina la Papii Kocha).

Napenda kuufahamisha Umma wa Watanzania kuwa taarifa hizo zote zilizotolewa kupitia njia hizo ni za Uongo na uzushi mkubwa na zinalenga kuipotosha jamii kwani wafungwa hao wapo gerezani na wanaendelea kutumikia adhabu ya kifungo cha Maisha gerezani kwa mujibu wa Sheria.

Jeshi la Magereza nchini linatoa onyo kali kwa watu kujiepusha na uhalifu huo na linawataka wale wote wanaotumiwa ujumbe wa aina hiyo waepuke kuusambaza ujumbe huo kwa wengine bali waufute, kwani kuendelea kuusambaza ni kosa kisheria.

Aidha, Jeshi la Magereza linaendelea na uchunguzi wa kina ili kuwabaini wanaosambaza ujumbe huo likishirikiana na Vyombo vingine muhimu kwa lengo la kuwakamata wahalifu hao ili mkondo wa Sheria uchukue nafasi yake.

Imetolewa na; Lucas Mboje, Mkaguzi wa Magereza, Afisa Habari wa Jeshi la Magereza, Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, DAR ES SALAAM. Septemba 8, 2014.

Hii ni taarifa kutoka kwa mtu mjinga, kupeleleza na kukamata ni kazi ya Polisi. Hii ndio shida ya kuwapa vilaza madaraka.
 
Back
Top Bottom