Acheni unafiki... babu tale anachofanya ni sahihi.. hana tofauti na mtu mwingine anaetafuta kazi maana hata kipindi cha msiba.. kuna watu wanaenda kwenye interview za kazi..
Babu tale kamuuguza mkewe, amemzika vizuri, ila watu hamridhiki.. baada ya msiba baba si anaenda kazini.. kipindi cha matanga kikifika anashiriki kama kawaida.. babu tale ni mtu makini sana...japo hajasoma sana ila amelea familia yake vizuri tena kwa ustaarabu.. watu wengi wenye kazi kama zake za kusimamia wasaniii ndoa zimewashinda... ila babu tale na uislam wake ameoa mke mmoja na wameishi vizuri bila skendo mpaka kifo kimewatengenisha...
Ameshamzika mke wake.. mwacheni akatafute kazi kwa ajili ya watoto wake awalee vizuri
Maana mnamponda humu huku hamumsaidii kutunza familia... akikaa nyumbani mtamlisha nyinyi na kumlipia ada..
Ubunge una maandalizi yake.. huupati kwa zima moto... watia nia wote kipindi hiki wapo majimboni wanapiga figisu figisu... why mnataka babu tale achelewe akute wenzake wameshamtangulia na kumwacha mbali kwenye figisu... kuwahi muhimu