Babu Tale kuweka kambi Morogoro Vijijini kwa ajili ya ubunge! Familia yagawanyika

Babu Tale kuweka kambi Morogoro Vijijini kwa ajili ya ubunge! Familia yagawanyika

Aisee mm mke wangu akifa itanichukua miaka 3 mpaka 4 kuja kukaa sawa kiakili na hii timu ya mpira ya watoto 6 nilio nayo mbn nitapagawa nitalia na kugalagala kama mtoto mdogo japo mke wangu anamapungufu Mengi mno lakini nitapagawa na kudata mno nitamkubuka kwa Mengi sana hasa nikiwa namuangakia uyu mtoto wa mwisho binti wa miaka 2 aisee nitadata mno yani nikiwa nakiangalia kitanda nitakuwa silala aisee nitakuwa

Nawaza nitamtania nani?,nitapikiwa na nani?,nitafuliwa nguo na nani,?nitanyolewa kipara changu cha kichwani na nani dongo,?nitanyolewa ndevu na nani mana nature ya kazi yangu ndevu kila wiki na nyoa tena zote na iyo kazi ya wife.,?nitakatwa kucha zangu na kusuguliwa miguu na nani.,?? Aisee ni Mengi sitachanganyikiwa mno
Acha kabisa kusu mke wewe wanatusumbua lakini wao ndo kila kitu ndani ya nyumba...MUNGU muweke mke wangu tuzeeke pamoja..

POLE babu tale kwa kipindi iki kigumu mke anauma mno...japo wanawake wapo wengi kumpata mtu sahihi ni ishu sana...

Mkuu,

Mula umenena maneno kuntu sana

Hilo lijamaa halina soni kabisa na yawezekana

maneno yanayosemwa hapa na wadau yakawa ya kweli.

Hivi kweli cheo kina thamani kushinda utu?

Ama kweli wonders shall never cease.
 
Unaona jamaa wala hata hajatulia kusubiri arobaini ya mkewe. Ubunge ndo priority yake. No wonder mkewe alimuomba Makonda amlelee wanae.
nilishangaa sana how come marehemu anawaomba watu wengine wamsaidie kulea wanae while baba wa watoto yupo hai.
 
Kwa hio mama akifariki.. baba asiende kutafuta kazi kwa ajili ya watoto wake waishi maisha mazuri?

Huyo huyo babu tale watoto wake wakikosa ada mtamsema mtandaoni..

Hujui ubunge unalipa sana... unajua watoto wa wabunge wanavyoishi maisha mazuri.. sasa babu tale kuwatafutia hayo maisha watoto wake mnamponda. Mnajifanya hamjui ubunge unapatikana kwa kugombea jimboni na sio kila siku kuna mda wake.. babu tale akichelewa aseme amlilie mkewe itambidi asubiri tena hadi 2025.. huku hio miaka mitano watoto wanasota maisha ya kubahatisha.. hadi diamond ampe posho
Nimewashangaa sana watanzania wenzangu.
Wana mawazo ya kimaskini maskini.Yani mipango ulopanga miaka 5 ilopita isimame kisa Mke aliyefariki?
Huu unafiki tu.Tena akiwa morogoro ndiyo vizuri awe karibu na kaburi la mkewe ajengee vizuri.Na ikiwezekana akimaliza maombolezo aoe haraka sana asiwe mpweke.
 
Halafu kwani watu before ubunge walikuwa wanaishije?
Maana majority ni raia wa kawaida kwani hatuishi, pesa zipo na zinataftwa tu lakini when ur loved one is gone atleast Kuna kipindi, flani hivi.
Is gone.
 
Kwa hili kama ilikuwa ni kweli basi jamaa alikuwa na shida kubwa na mkewe ingawa hikuwa rahisi sana kuigundua.
Aisee ogopa sana watu wenye tabasamu kama lote......kuna tabasamu flani hivi lilikuwepo kati yao halafu bidada alikuwa na kicheko flani mtu anayedeal na mambo ya councelling ni rahisi kudetect tatizo, alikuwa anacheka kama anamuendelezo wa kitu flani then anaongea anapiga stop na tabasam HATARI SANA.
 
Kwa hesabu za kawaida bado kuna mambo mazito yamezunguka juu ya saga zima hili.. wingu hilo zote kwa sasa itakuwa ni tafrani kwa upande wa pili. Yawezekana mke alishajua yeye ndio target na ndio maana alianza harakati mapema za kujikomboa(hii ni kwa mujibu wa post flani flani) sasa mbaya zaidi ni kule alikokimbilia ni moto utawaka. Maana ile laser guided missle ukishatumiwa na target iko locked ku intercept inatakiwa utaalam mkubwa. Sina shaka na mtaalam aliemkimbilia, ila tatizo ni life style ya muhusika! Life style inaua nguvu na karama na hata vipawa vya kutibu... alijaribu ila ndio hivyo kombora lilimuondoa mlengwa!

Kazi kwa picha za msiba ule kule Moro, sanduku kuwekwa chini ardhini ndani ya nyumba na huku likiwa juu ya jamvi nusu mwili (Yani nusu juu ya jamvi na nusu juu ya ardhi) na mpangilio wa watu kuzunguka pale ni viashiria tosha kwamba chain ile imekuwa unbreakable..tutarajie uvunaji wa jamaa zaidi kwenye familia yake. Na kwa yule aliejaribu ku intercept lile kombora ndio atamezwa taaluma yake maana maziko yale yalizika vingi/mengi... ngoja tuone
Hata jinsi upande wa juu wa jeneza ulivyoelekea usawa wa dirisha lilikowa na pazia lenye Nembo.....Dah Maisha Bana.
 
Kile si kilio cha huzuni, hata mtoto mdogo angecheki angejua tuu
Hasa alipokuja Mh. flani ambaye ameachiwa jukumu la watoto na ambapo Mke alienda kule kuacha wosia basi kilio kikapandishwa weeeeeee.....lakini ukiendelea kuangalia picha na matukio unaona kabisa ni mapichapicha..................mbaya zaidi haya mambo hayajifichi SIJUI NI KWANINI
 
Nimewashangaa sana watanzania wenzangu.
Wana mawazo ya kimaskini maskini.Yani mipango ulopanga miaka 5 ilopita isimame kisa Mke aliyefariki?
Huu unafiki tu.Tena akiwa morogoro ndiyo vizuri awe karibu na kaburi la mkewe akengee vizuri.Na ikiwesezekana akimali,a maombolezo aoe haraka sana asiwe mpweke.
Hivi wee n mwanamke kweli? Lol
 
Wangeweka tu kigezo degree ujue bunge letu limekuwa kimbilio la wapuuzi wasio weza hata kutunga sera, yani imekuwa sehemu ya watu kwenda kupiga hela kiurahisi, iweje dereva wa mbunge awe na form four qualification, plus Veta training huku mbunge yeye ajue tu kusoma na kuandika huko ka si kurogwa Nini?
Aisee
 
Jinsia yangu inahusiana nini na mada?
Kwanza inakuhusu nini?Au mnachangia kulingana na jinsia ndugu mwana jamvi?
Nooope sijauliza kwa ubaya, ila wee kweli mwandani wako amekuacha sku 3 tu tangu mumpumzishe ktk nyumba yake ya milele, ndio uanze harakati za siasa, tena islamic hata 7 haijafika mmmmh, hapana kwa kweli
 
Mkuu,

Mula umenena maneno kuntu sana

Hilo lijamaa halina soni kabisa na yawezekana

maneno yanayosemwa hapa na wadau yakawa ya kweli.

Hivi kweli cheo kina thamani kushinda utu?

Ama kweli wonders shall never cease.
Aiseee hana son mke man dah.
 
Wasalaam

Meneja wa Diamond Platinumz ambaye amefiwa siku tatu zilizopita ,kuanzia leo ameanza mchakato na kuendelea na mchakato wa kugombea ubunge wa Morogoro vijijini tiketi ya CCM!

Pamoja na mpango huo ndugu zake wa karibu wamekuwa wakiweka shinikizo la kupinga ndugu yao kugombea ubunge hasa kipindi hiki ambacho amefiwa na mke wake na uchaguzi umekaribia....na bahati mbaya ni juzi ametoka kufiwa na mke wake hivyo haitaleta picha nzuri kwenye jamii kwani ubunge usimfanye akasahau utu na yeye ni mfiwa hata msiba hajapoa na hata udongo kwenye kaburi la mkewe haujashikana!

Lakini ushauri wa ndugu na watu wa karibu wa Tale umegonga mwamba kwani waki ijayo Babu Tale anatarajia kwenda kuweka kambi Morogoro kwaajili ya maandalizi ya kugombea ubunge wa Morogoro Mjini.
Ni hatari hata matanga bado hayajesha yeye ashaanza kampeni? Watu wakiconfirm hizo tuhuma za NGENDE atabisha?
 
Nooope sijauliza kwa ubaya, ila wee kweli mwandani wako amekuacha sku 3 tu tangu mumpumzishe ktk nyumba yake ya milele, ndio uanze harakati za siasa, tena islamic hata 7 haijafika mmmmh, hapana kwa kweli
Kwa hiyo mwenzangu maneno yote unayosoma mtandaoni unayabeba kama yalivyo?
Na inamaana hamjui Tale moro kwao,lazima tu angerudi sababu ya mambo ya msiba hata kama sio ubunge?
Na ni vema kama ameamua amalize maombolezo yake aunge na mambo mengine.
Its all good.Huu ni mtazamo wangu na maoni yangu.Hatupaswi kufanana.Duniani tunatofautiana sana kimtazamo.
 
Back
Top Bottom