Babu Tale: P Diddy alituita chumbani kwake tukaangalie runinga, Swizz Beatz akatukataza na tukaondoka bila kuaga

Babu Tale: P Diddy alituita chumbani kwake tukaangalie runinga, Swizz Beatz akatukataza na tukaondoka bila kuaga

Mbunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano la Tanzania Mhe Tale amesema walikwenda nyumbani kwa Diddy na waliitwa chumbani kwake kwenda kuangalia filamu lakini mtayarishaji wa muziki kutoka Marekani (aliyekuwa mwenyeji wao), Swizz Beatz alikataa wasiende.

Kufuatia tuhuma zinazomkabili mkali wa Hip hop kutoka Marekani Diddy, Sean ‘Diddy’ Comb huku baadhi ya mastaa mbalimbali kuhusishwa kwenye kesi zake, meneja wa msanii wa Bongo Fleva, Diamond, Babu Tale amefunguka yaliyotokea baada ya kutembelea nyumbani kwa staa huyo.
Hapa tunahitaji ushahidi wa kutosha beyond a reasonable/ shadow of doubt!!
 
Jamaa msosi walitafuna na msosi wakafagia ila chumbani wakatoka nduki,

Swali, Kama mwenyeji wao Swizz Beat alizijua tabia za Didy aliwapeleka kufanya Nini?

Je, ni kula tu msosi?

Je, ni wakati Gani waliitiwa huo msosi?
Hapa tunahitaji ushahidi wa kutosha beyond a reasonable/ shadow of doubt!!
 
Ila Diddy baradhuli sana😂😂😂.

Na kwa Tale kuachwa salama nakataa. Likiongea tu linarembua na kuweka madoido. Yani hata kama siku hiyo Diddy alikuwa hana hamu lazima alimtamani Mheshimiwa na kumpaka Baby Oil😂

1727325442269.png
 
Mbunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano la Tanzania Mhe Tale amesema walikwenda nyumbani kwa Diddy na waliitwa chumbani kwake kwenda kuangalia filamu lakini mtayarishaji wa muziki kutoka Marekani (aliyekuwa mwenyeji wao), Swizz Beatz alikataa wasiende.

Kufuatia tuhuma zinazomkabili mkali wa Hip hop kutoka Marekani Diddy, Sean ‘Diddy’ Comb huku baadhi ya mastaa mbalimbali kuhusishwa kwenye kesi zake, meneja wa msanii wa Bongo Fleva, Diamond, Babu Tale amefunguka yaliyotokea baada ya kutembelea nyumbani kwa staa huyo.

Akizungumza na Rick Media, Babu Tale amesema walikwenda nyumbani kwa Diddy na waliitwa chumbani kwake kwenda kuangalia filamu lakini mtayarishaji wa muziki kutoka Marekani (aliyekuwa mwenyeji wao), Swizz Beatz alikataa wasiende.

“Sisi tulienda kama tulivyotoa taarifa hapo awali na tulitoka salama, jana ndiyo nimejua kwamba Swizz Beatz alikuwa akitulinda kinoma, kwanza tulipofika tulikaa nje.

"Diddy akatangulia chumbani juu anaangalia movie wafanyakazi wake wawili wakaja kutuchukua kwenda kula, baada ya muda akawatuma twende chumbani kwa Diddy tukaangalie movie lakini Swizz akawa mkali na tukaondoka bila kuaga kwa hiyo sisi tukawa tunajua kuwa brother (Swizz Beatz) ametubania, kumbe alikuwa anatulinda,” amesema Babu Tale.

Babu Tale ametoa ufafanuzi huo baada ya minong’ono kusambaa kuhusu safari yao nyumbani kwa Diddy, baada ya kipande cha video kikimuonyesha Diamond akifanyiwa mahojiano akisema kuwa baadhi ya mambo yaliyofanyika nyumbani kwa staa huyo sio ya kuwekwa kwenye vyombo vya habari.

“Ni kweli tulienda kwa Diddy nafikiri ilikuwa siku moja kabla ya uhuru wa Marekani, tulienda kwa Diddy usiku tukakaa kuna vitu tukafanya sema yaliyofanyika yalikuwa siyo ya kuposti kwa sababu yana mambo yajayo mbele,” alisema Diamond kwenye moja ya mahojiano yake aliyowahi kufanya.

Kwa sasa Diddy amezuiliwa katika gereza la ‘The Metropolitan Detention Center (MDC) kwa tuhuma za ulaghai wa kingono na usafirishaji wa binadamu ili kujihusisha na biashara hiyo ya ngono, huku zaidi ya chupa 1,000 za mafuta na vilainishi vikikutwa katika nyumba yake ya Miami na New York.

Mwananchi
Lukamba anasema sijui alitaka ampake nan hilo wese kati ya babu tale, mondi, na yeye🤗🤗🤣🤣🤣
 
Akihojiwa na Rick Media, Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki ambaye pia ni Meneja wa msanii nguli Diamond Platnumz, Mh. Hamis Taletale au kwa jina maarufu Babu Tale amekiri walipoenda kumtembelea msanii P.Diddy, alionesha viashiria ambavyo wao hawakujua maana yake.

Mojawapo ya tukio la ajabu ni pale Diddy alipowakaribisha juu ghorofani wakaangalie runinga. Lakini mwenyeji wao waliyeenda naye, Produza Swizz Beatz aliwakataza kata kata. Na hata wakati wanaondoka hawakuagana na P Diddy.

Pia soma: Kitendo cha Diamond Platnums kwenda nyumbani kwa P. Diddy kimemlipa

Kesho yake Swizz alikuwa na party pia, walienda kushiriki na baada ya kumaliza Swizz aliwaonya tena wasije wakajaribu kwenda nyumbani kwa Diddy, Swizz aliwakabidhi kwa dereva awarudishe hotelini, huku akimpa maonyo makali dereva asije akajaribu kuwapeleka mahali popote.

Maelezo ya Tale yamekuwa tofauti na maelezo aliyotoa Nassib hapo awali, japo wote wanazungumzia safari ileile ya kwenda nyumbani kwa Diddy.

Awali, tuliambiwa Nassib kuwa, kuna mambo walifanya kwa Diddy ambayo hayawezi kuwekwa hadharani, lakini Tale anasema waliitwa kula chakula.

Na anaongeza, waliitwa chumbani na Diddy ila Swizz Beatz akawakataza, wakaondoka. So vitu walivyofanya na haviwezi kuwekwa hadharani ni kula chakula?

Maelezo ya Tale yanaonesha kuwa, wao walikula chakula tu kwa Diddy, kwamba hayo ndiyo mambo ambayo walifanya nyumbani kwa Diddy na hayawezi kupostiwa kama Nassib alivyosema?

Hawa bado hawajasema, kama wakiulizwa vizuri watasema tu.

Ova
 
Tunamshukuru Mh rais kwa jambo la mbunge wao kuwawakilisha Wana CCM katika nyanja za kimataifa hakika mama anaupiga mwingi.
 
Akihojiwa na Rick Media, Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki ambaye pia ni Meneja wa msanii nguli Diamond Platnumz, Mh. Hamis Taletale au kwa jina maarufu Babu Tale amekiri walipoenda kumtembelea msanii P.Diddy, alionesha viashiria ambavyo wao hawakujua maana yake.

Mojawapo ya tukio la ajabu ni pale Diddy alipowakaribisha juu ghorofani wakaangalie runinga. Lakini mwenyeji wao waliyeenda naye, Produza Swizz Beatz aliwakataza kata kata. Na hata wakati wanaondoka hawakuagana na P Diddy.

Pia soma: Kitendo cha Diamond Platnums kwenda nyumbani kwa P. Diddy kimemlipa

Kesho yake Swizz alikuwa na party pia, walienda kushiriki na baada ya kumaliza Swizz aliwaonya tena wasije wakajaribu kwenda nyumbani kwa Diddy, Swizz aliwakabidhi kwa dereva awarudishe hotelini, huku akimpa maonyo makali dereva asije akajaribu kuwapeleka mahali popote.

Kwa kuwakataza na kuwaonya bila kusikiliza hisia zao, Swizz hakuwatendea haki wawili hao. Vipi kama labda wao walihitaji zaidi kuangalia TV kwa Diddy kuliko kuhudhuria party ya Swizz?
 
Back
Top Bottom