Babu Tale: P Diddy alituita chumbani kwake tukaangalie runinga, Swizz Beatz akatukataza na tukaondoka bila kuaga

Babu Tale: P Diddy alituita chumbani kwake tukaangalie runinga, Swizz Beatz akatukataza na tukaondoka bila kuaga

Hali ya hewa imechafuka sana.
Mawimbi yanazoa watu wengi maarufu kila kona ya dunia kwenye biashara ya Muziki na Burudani.
Dhoruba yote imeanzia kwenye kasri la Bwana sijui niite Bi Sean Combs maarufu kama P. Diddy.
Zile tafrija za Freak Off zimerekodiwa.
.
Sasa ndugu zetu toka Tanzania wako walIo onekana wakiwa ktk hilo kasri. Tena walipiga picha za kwao za ushahidi kuonesha waliingia kwa mtinduaji.

Babu Tale na cameraman wa kundi hilo maarufu bongo wa wakati huo aitwae Rukamba/Lukamba wameongea kupitia vyombo vya habari kujitetea hawakufikiwa na tone la mafuta. Kwamba waliitwa chumbani kwa mtinduaji lakini mwenyeji wao 'Swiz Beat' 'akawagombelezea' yaani kawaokoa wasiende chumbani kwa mwamba.

Kwa sasa hatuamini kauli yoyote hadi kesi ya P Diddy iishe. Uzuri ni kwamba jamaa alifunga camera kila chochoro la kasri lake. FBI wameshapata hizo video tapes.
Tusubiri tuone hatima ya ndugu zetu. Kweli walitoka salama?

Hawakutindua watoto wadogo au hawakugusa wanawake waliolazimishwa ngono?

Nasikia bwana Ali K naye kaibuka anasema alipoenda kwa R KELLY hakutinduliwa. Ukumbuke huyo mtinduaji mwingine anatumikia kifungo kwa baadhi ya makosa yanayo fanana na ya P Diddy.

Umaarufu unapatikana kwa shida, ikibidi watu wanafuata cha uvunguni wanainama.

Matusi dhidi yangu hayatafuta kashifa hii. Yataonesha kweli kuna watu wameguswa na upako wa mafuta ya Diddy.

Nasemaje LATE THE VIDEO TAPES ROLL..😃
 
Hali ya hewa imechafuka sana.
Mawimbi yanazoa watu wengi maarufu kila kona ya dunia kwenye biashara ya Muziki na Burudani...
Ndugu mripoti ripoti yako imekamilika na imejieleza......kwa kifupi hili wimbi ni zito na kwa ukubwa na uzito wake kwa kila aliyepitiwa kusalimika ni ngumu Sana
 
Akihojiwa na Rick Media, Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki ambaye pia ni Meneja wa msanii nguli Diamond Platnumz, Mh. Hamis Taletale au kwa jina maarufu Babu Tale amekiri walipoenda kumtembelea msanii P.Diddy, alionesha viashiria ambavyo wao hawakujua maana yake...
Kuna mambo hawajazungumza bana et runinga mnatupanga kama watoto wadogo fungukeni
 
Naskari wakae na diamond kabla ya kujitetea

Diamond kasema wak
Akihojiwa na Rick Media, Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki ambaye pia ni Meneja wa msanii nguli Diamond Platnumz, Mh. Hamis Taletale au kwa jina maarufu Babu Tale amekiri walipoenda kumtembelea msanii P.Diddy, alionesha viashiria ambavyo wao hawakujua maana yake...
Ienda chumban

Huyu atujwenda

Nykkoooo

Mtasema yoteee
 
Akihojiwa na Rick Media, Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki ambaye pia ni Meneja wa msanii nguli Diamond Platnumz, Mh. Hamis Taletale au kwa jina maarufu Babu Tale amekiri walipoenda kumtembelea msanii P.Diddy, alionesha viashiria ambavyo wao hawakujua maana yake...
Mbona huu ufafanuzi hauna yale maelezo ya Diamond kuhusu mambo waliofanya ambayo hayawezi kuelezwa mbele ya vyombo vya habari?
 
Kipindi wametoka marekani walikataa kabisa kuongea walichoenda kufanya kwa "didi" kwakua imejulikana jamaa ni mla visamvu wa kimataifa ndio wanajaribu kujisafisha 🙄 hawa jamaa lazima na wenyewe walipatiwa utakaso wa mafuta ya moto 😃😃
 
IMG-20240926-WA0033(1).jpg

Mbunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano la Tanzania Mhe Tale amesema walikwenda nyumbani kwa Diddy na waliitwa chumbani kwake kwenda kuangalia filamu lakini mtayarishaji wa muziki kutoka Marekani (aliyekuwa mwenyeji wao), Swizz Beatz alikataa wasiende.

Kufuatia tuhuma zinazomkabili mkali wa Hip hop kutoka Marekani Diddy, Sean ‘Diddy’ Comb huku baadhi ya mastaa mbalimbali kuhusishwa kwenye kesi zake, meneja wa msanii wa Bongo Fleva, Diamond, Babu Tale amefunguka yaliyotokea baada ya kutembelea nyumbani kwa staa huyo.

Akizungumza na Rick Media, Babu Tale amesema walikwenda nyumbani kwa Diddy na waliitwa chumbani kwake kwenda kuangalia filamu lakini mtayarishaji wa muziki kutoka Marekani (aliyekuwa mwenyeji wao), Swizz Beatz alikataa wasiende.

“Sisi tulienda kama tulivyotoa taarifa hapo awali na tulitoka salama, jana ndiyo nimejua kwamba Swizz Beatz alikuwa akitulinda kinoma, kwanza tulipofika tulikaa nje.

"Diddy akatangulia chumbani juu anaangalia movie wafanyakazi wake wawili wakaja kutuchukua kwenda kula, baada ya muda akawatuma twende chumbani kwa Diddy tukaangalie movie lakini Swizz akawa mkali na tukaondoka bila kuaga kwa hiyo sisi tukawa tunajua kuwa brother (Swizz Beatz) ametubania, kumbe alikuwa anatulinda,” amesema Babu Tale.

Babu Tale ametoa ufafanuzi huo baada ya minong’ono kusambaa kuhusu safari yao nyumbani kwa Diddy, baada ya kipande cha video kikimuonyesha Diamond akifanyiwa mahojiano akisema kuwa baadhi ya mambo yaliyofanyika nyumbani kwa staa huyo sio ya kuwekwa kwenye vyombo vya habari.

“Ni kweli tulienda kwa Diddy nafikiri ilikuwa siku moja kabla ya uhuru wa Marekani, tulienda kwa Diddy usiku tukakaa kuna vitu tukafanya sema yaliyofanyika yalikuwa siyo ya kuposti kwa sababu yana mambo yajayo mbele,” alisema Diamond kwenye moja ya mahojiano yake aliyowahi kufanya.

Kwa sasa Diddy amezuiliwa katika gereza la ‘The Metropolitan Detention Center (MDC) kwa tuhuma za ulaghai wa kingono na usafirishaji wa binadamu ili kujihusisha na biashara hiyo ya ngono, huku zaidi ya chupa 1,000 za mafuta na vilainishi vikikutwa katika nyumba yake ya Miami na New York.

Mwananchi
 
Back
Top Bottom