Babu wa Loliondo afungiwa kwa muda kutoa huduma...

Babu wa Loliondo afungiwa kwa muda kutoa huduma...

Serikali haikuhiji uhalali wa dawa? Wamemsimamisha sababu ya mazingira anayotolea huduma hayakidhi uwepo wa umati huo wa watu

Mbaya zaidi dawa ya babu hatibu magonjwa ya mlipuko e.g kipindupindu
 
Baada ya waziri wa afya kutoa tamko la kusitisha huduma kwa maelfu ya wagonjwa wanaosubiri kupewa dozi na mchungaji, kuna uwezekano mkubwa kwa wagonjwa hao kupuuza agizo hilo la serikali na kusema wataendelea kusubiri hadi wapate hiyo dawa, hivyo liwalo na liwe!
 
Mmmh isijekuwa ni ya kupunguza watu ila wakubwa waende kwa kujinafasi na baadae tutangaziwa hivi:-"Uchunguzi wa kimaabara umeonyesha kuwa dawa ya babu haina madhara kiafya. Aidha, utafiti wa kisayansi umeshindwa kuthibitisha kama kweli dawa hiyo ina uwezo wa kutibu magonjwa yanayosadikiwa kutibika kwa dawa hiyo. Hata hivyo, kwa kuwa suala lenyewe linahusu imani zaidi, Serikali haina kipingamizi".
 
Ilitakiwa Babu asidiwe, red cross wangeenda kuhakikisha tempo toilet na usafi in general. Hizo ni nguvu za Mungi period!.
 
Wanakataza baada ya vigogo kama sio magogo yote kupata kikombe cha dawa
 
Jamani, tukumbuke pia kuwa watu wanaokwenda huko ni wengi mno. Sidhani km serikali ina nia mbaya. Ni kiasi cha kujiridhisha kuwa dawa ipo salama.
 
Hii ndo sababu ,baada ya kuwaponya wagonjwa kadahaa, Yule Masihi Yesu alikuwa akiwaambia waliopona msimwambie mtu.

Serikali haijali maisha ya kila simu ya Mtanzania kwamba anakula nini anakunywa nini.
Watu kila uchao, ikiwa ni pamoja na Elite wa serikali, wanafakamia lita kwa Mamilioni za dawa za kienyeji kila kona ya Tanzania kwa imani zao za kishirikina sijasikia serikali ikitoa walau tahadhari tu.

Nahisi wanamshitukia Babu asijekuwa anatoa dawa ya kuzingua Ushirikina wao kwa ulaini.
 
Ndugu yangu amerudi leo kutoka kwa Babu kupata dawa, amenipa hali halisi kuwa Babu yupo kwa ajili moja tu kusaidia watu na hapati hata senti tano. Ni kuwa mpaka sasa ana wasaidizi sita ambao wote ni wachungaji wanaomsaidia kutoa dawa na kwa siku anahudumia magari yapatayo elfu moja. Na mchanganuo wake kwa kila Tsh 500 inayotolewa ni kuwa; Tsh 300 inakwenda kwenye huduma za kanisa yote kama ilivyo bila kupungua hata senti na Tsh 200 wanachukua hawa wasaidizi wake sita kwa kazi ngumu wanayoifanya. Hivyo yeye hapati hata mbuni. :-(
Hata na mimi sasa hivi natoka kuongea kwa simu na ndugu yangu aliyekwenda huko ili kupata matibabu, amesema hivyi hivyo.
 
Ningeshangaa sana kama serikali ingeacha mambo yaende kama yalivyokuwa yanakwenda. Kwa hali ilivyokuwa tulikuwa tunaelekea kutengeneza maafa mengine. Cha msingi serikali ikamilisha hizo tafiti zake mapema na iwape wananchi mwelekeo haraka iwezekanavyo.
 
Mmmh isijekuwa ni ya kupunguza watu ila wakubwa waende kwa kujinafasi na baadae tutangaziwa hivi:-"Uchunguzi wa kimaabara umeonyesha kuwa dawa ya babu haina madhara kiafya. Aidha, utafiti wa kisayansi umeshindwa kuthibitisha kama kweli dawa hiyo ina uwezo wa kutibu magonjwa yanayosadikiwa kutibika kwa dawa hiyo. Hata hivyo, kwa kuwa suala lenyewe linahusu imani zaidi, Serikali haina kipingamizi".

Ou avez vous cherche cette information, monsieur? (Si tu ne cherche pas quelquechose, c'est quelquechose qui te cherchera!!)
 
jamani mie nimeshatoka Mombasa nipo Mto wa Mbu itakuwaje tena? kuweni serious jamani
 
Kukurukupa tu, si ndo hao walileta Chloroquine, baadae wakasema haifai, so do Fansidar na SP. Siku si nyingi nikasikia wameleta ARV feki kutoka Afrika Kusini... Aagh, waache watu wapone bwana!
 
waziri asiyetumia akili hata kidogo. Je anajua ni watz wangapi wamepona kwa muujiza huu wa Mungu. Chezeni na akina Makamba msicheze na Mungu.
 
Pole sana wadau, hivi hata walikwisha fika huko LOLIONDO wanarudi bila dawa au serikali inaweka Road Block kusema haindi tena mtu huko?
 
Tanzania bwana mbona hawajazipima za sheikh Yahya au za Dr Ndodi hapo tayari mkono wa mtu umeshaingizwa hapo wangeacha anayeamini aende asiyetaka abaki na ngoma yake vigogo wameshakunywa halafu wanawazibia wengine
 
Mambo ya imani hayafanyiwi utafiti wa kipumbavu kiasi hicho.Wamwache mzee afanye huduma yake.
 
Back
Top Bottom