Babu wa Loliondo afungiwa kwa muda kutoa huduma...

Babu wa Loliondo afungiwa kwa muda kutoa huduma...

Hali hii ilitegemewa na wengi. Baada ya viongozi wengi kupata huduma ya uponyaji akiwepo Askofu Laizer na Askofu Shao ambao wamekiri kupokea uponyaji sasa viongozi wetu wameona ni wakati wa wanyonge wa nchi kufa. Utafiti wao unaweza kufanyika wakati watu wakiendelea kupata dawa. Mimi nafikiri wangechukua wagonjwa wa magonjwa kadhaa yanayotibiwa na mchungaji huyu wawachukue vipimo kabla ya tiba ya mchungaji halafu wawafanyie vipimo baada ya kupata dawa. Wakirudia vipimo hivyo mara kadhaa wangeweza kujiridhisha. Pia tuelewe tiba ni imani ya mtu pia. Hakuna mwenyeuamuzi na maisha ya mtu binafsi kunapohitajika utabibu. Juzi nilibahatika kumwona mzee mmoja akitokwa na machozi pale watoto wake walipokuwa wanamshauri aende kwenye clinic yake ya kawaida pale Dar . Mzee alisisitiza kuwa anataka kwenda Loliondo na sio Dar. Jitihada za watoto kumshauri zilikwama na zaidi walipoona machozi ya baba. Mzee alipelekwa na sasa anajiona ahueni. Sisemi kuwa serikali haihusiki na maisha ya watu wake, la hasha ila kuishi pia ni uhuru wa mhusika. Linapokuwa ni suala la kuishi ni muhimu zaidi. Sioni sababu ya kukataza dawa hata kidogo labda iwe kunahusisha sumu ingawa dawa zote ni sumu kama zitatumika ndivyo sivyo. Ukija upande wa pili utakuta kuwa wanakataza ili waweze kupeleka ndugu zao. Fikiria unakutana na waziri wako ama hata kiongozi mkuu unategemea ataonaje aibu. Yaani wengine wanafikiria kuwa kuugua ni aibu. Tuache fitna tuangalie ukweli!
 
Serikali imefanya vyema. Hizi local beliefs zinarudisha nyuma maendeleo. Cha ajabu hatujasikia watu waliopata kupona kutokana na dawa hii. Kwa hili nasema Serikali mmefanya la mbolea. Dawa inapashwa kuchunguzwa na kujua kama inafaa kwa mwili wa mwanadamu sio kugawa dawa kama peremende. Kikombe kimoja watu maelfu sasa kuna kupona kweli?
 
Mbona hawasitishi tiba za shehe Yahaya na kumwambia kwanza zithibitishwe?
 
Wameona wenyewe na familia zao wameshakunywa kikombe cha babu mnyakyusa huko Loliondo sasa wanabania wenzao, kweli wakubwa wana mambo.

mimi nilidhani jambo jema ni kwa wao kuweka utaratibu mzuri wa usafiri na huduma za kijamii kama maji na vyoo na sio kuingilia namna ya kutibu.,

mbona hawawingilii washirikina wao wanowachanja chale na kuwapa hirizi ili wapate madaraka na kua na ulinzi wa kishetani?? Kwa hapo serikali imevuka mpaka.
 
Nilihoji hii kitu asubuhi!!! Inakuwaje mtu anaachiwa kugawa dawa kwa wananchi ambayo wala haijachunguzwa ubora na madhara yake. Nikashauri wasimamishe na kuomba watalaam wa WHO waichunguze.

Kwa vile inasemekana inaponya, naona itakuwa ngoma kwelikweli kuwakatisha watu ambao wana imani nayo tayari!!

Kula tano,mwanangu.Pointi za msingi sana hizo
 
pamoja na nia nzuri ya serikali, na uharaka wa tiba ambayo wananchi wanaitaka kwa hali yoyote ile, serikali ingeweka kambi huko kwa babu na kufanya naye kazi bega kwa bega huku yenyewe inajiridhisha na wananchi wanapata ujumbe haraka sana.
Kwa vile wananchi wamefumuka kwa wingi, basi serikali wangeamrisha watu wa red cross na watoa huduma wote wa afya ya binadamu kuwa karibu na watu na kuhakikisha wanazuia au kulinda madhara tofauti na magonjwa ambayo watu wamefuatia tiba. Vitu vya msingi kama mahema, madawa nk vingepelekwa kama tahadhari, kama walivyofanya polisi mkoa wa Arusha katika kulinda usalama wa raia.
Research ifanywe huko huko na siyo Dar, na uthibitisho au matokeo yatoke huko huko ambako watu wapo. Tusikurupuke kutoa maamuzi ambayo baadae watu watalazimika kutumia njia za panya kufika huko. WARIDHISHENI WATU KWA MAJIBU SAHIHI.
 
Watu walianza kuitumia bila ushauri au tangazo la serikali,so watu wataendelea tu kuitumia regardless of what the govement has said.Watu wanaimini dawa kuliko serikali
 
kweli wizara ya afya imefilisika dawa kibao feki zipo mitaani awazifanyii utafiti wala awaizuii ila babu kafunuliwa wanataka kufanya utafiti kwani mpaka wapime dawa kwanini wasipeleke wagonjwa husika wa kwao wakawafanyie utafiti kama wamepona au la
 
Serikali imesitisha kwa muda utoaji wa tiba (miracle cure) unaofanywa na Babu wa Loliondo mpaka uchunguzi wa dawa unaofanywa na wataalamu wa serikali utakapothibitisha kuwa tiba yenyewe inafanya kazi kweli.

Pia serikali inataka kujiridhisha kuwa dawa ya Babu ni safi na salama kunywa ili isilete magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu, typhoid, etc kwa wagonjwa.

Source: Clouds FM

Habari za kuaminika zinasema Mkulu, mkewe na vigogo wenzake wengi tu wamshatumia hiyo dawa na baadhi ya vogogo wame testify kuwa wamepata miujiza yao. Kama azma ya siri kali ni kusitisha huduma ya babu, inayoaminiwa na wengi kuwa ina upako wa pekee for selfish reason, Sii kali itapigwa kwa laana. Kama nia ya serikali ni nzuri na ya manufaa kwa wananchi waliochoka na huduma mbovu za hospitaly na ma NGO feki ya ukimwi, then it's ok!
 
Utafiti ni muhimu lakini kwa hili la imani haitawezekana,waachwe watu wapate huduma hiyo muhimu,mazingira yaboreshwe mzee aendelee na shughuli yake haraka ikiwezekana ndani ya siku 7.

Ni jukumu la serikali kujitutumua kuonyesha uwepo wake lakini haitakuwa busara kumfungia kabisa kutoa huduma hiyo.Huduma kama hiyo ingegunduliwa na mtu mweupe hakuna ambaye angefungua kinywa chake kukebehi,tuache kuendekeza fikra za kikoloni,kudharau vya kwetu.TUMUWEZESHE TIBA IENDELEE KUTOLEWA KWA UFANISI.Watu wanajifanya kuponda dawa za waganga wa jadi wakati ndio vinara wa kujiganga na kuroga wenzao makazini wapate vyeo na wakati wa kampeni za siasa,tuache unafiki.
 
Serikali imesitisha kwa muda utoaji wa tiba (miracle cure) unaofanywa na Babu wa Loliondo mpaka uchunguzi wa dawa unaofanywa na wataalamu wa serikali utakapothibitisha kuwa tiba yenyewe inafanya kazi kweli.

Pia serikali inataka kujiridhisha kuwa dawa ya Babu ni safi na salama kunywa ili isilete magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu, typhoid, etc kwa wagonjwa.

Source: Clouds FM

Naiomba Serikali imkamate huyu Mganga wa Kienyeji kwa kusababisha vifo vingi vya Wagonjwa ktk wiki hii!! ni jana tu nimemzika Shangazi yangu aliyefariki huko Loliondo mara tu baada ya kunywa kikombe kimoja cha dawa ili kutibu gonjwa la kisukari!!! Marehemu Shangazi langu aliishi na ugonjwa huo zaidi ya miaka 20 lakini alipoambiwa kuna Mchungaji anatibu papohapo tulimpeleka Shangazi na kupewa hiyo dawa na tukiwa njiani kurudi nyumbani Shangazi aliaga dunia!!

Tunasikitika kumpoteza Shangazi wetu mpendwa na nimesikia kuna wagonjwa wengi waliofariki mara baada ya kunywa dawa za huyo Mchungaji na kunipa hofu na kukumbuka kisa cha Mchungaji mmoja huko Uganda miaka ya 90 alichoma Kanisa Moto na kuteketeza maelfu ya Waumini waliokuwa humo ndani kwa kudai alioteshwa na Mungu kuwa wakifia Kanisani kwa kujichoma moto basi wataenda mbinguni!!!

Naiomba Serikali imchukulie hatua kali huyu Mchungaji wa Loliondo kwani amesababisha madhara makubwa kwa Wananchi na hata kuharibu mazingira kwa kuwakusanya maelfu ya watu mahali finyu bila choo wala mahala pa kulala na pa kula!!

Familia yetu iko mbioni kushika wakili ili tumfungulie kesi kwa kusababisha kifo cha Shangazi wetu mpendwa!
Wananchi tuwe macho na hawa WACHUNGAJI NA MAPADRE wenye kudai kutibu maradhi baada ya kuoteshwa ndoto na Mungu wakiwa wamelala!!!!!!!!!
 
Wamesema hadi dawa hiyo isajiliwe kwanza. Kuna kazi !!!!!!!!!!
 
huyo shangazi yenu aliitwa na huyo babu?......
 
Back
Top Bottom