pamoja na nia nzuri ya serikali, na uharaka wa tiba ambayo wananchi wanaitaka kwa hali yoyote ile, serikali ingeweka kambi huko kwa babu na kufanya naye kazi bega kwa bega huku yenyewe inajiridhisha na wananchi wanapata ujumbe haraka sana.
Kwa vile wananchi wamefumuka kwa wingi, basi serikali wangeamrisha watu wa red cross na watoa huduma wote wa afya ya binadamu kuwa karibu na watu na kuhakikisha wanazuia au kulinda madhara tofauti na magonjwa ambayo watu wamefuatia tiba. Vitu vya msingi kama mahema, madawa nk vingepelekwa kama tahadhari, kama walivyofanya polisi mkoa wa Arusha katika kulinda usalama wa raia.
Research ifanywe huko huko na siyo Dar, na uthibitisho au matokeo yatoke huko huko ambako watu wapo. Tusikurupuke kutoa maamuzi ambayo baadae watu watalazimika kutumia njia za panya kufika huko. WARIDHISHENI WATU KWA MAJIBU SAHIHI.