Babu wa Loliondo afungiwa kwa muda kutoa huduma...

Babu wa Loliondo afungiwa kwa muda kutoa huduma...

watu wanywe dawa maadam ni miti ambayo ameumba mungu na hakuna maradhi yasio na dawa.kama kuna mgonjwa amepata reaction hapo lipo la kuchunguza.tena babu amekutajia mti anaotumia! Pamoja na yote pia inabidi kuwa waangalifu na tiba anayotoa na imani mbalimbali.
 
mimi sijui mwisho wa tiba na madhara ya loliondo. Lakini ukweli unabakia pale pale kuwa watu wanapona. Nilichokisikia jana ktk vyombo vya habari kuwa "babu " asimamishe huduma yake, binafsi naona si haki kwa kile serikali ilichoamua. Kujisajili si kitu muhimu wakati huu wa neema. kwani huduma za tiba zilikuwepo toka enzi na hazikuwa zimesajiliwa. TFDA ipo lakini jana tu gazeti moja limeandika uingizwaji wa dawa feki nyingi tu za malaria. Nawaomba mlioko huko Ar kachukueni form mpatieni Babu ilikwamba huduma iendelee. Na tunaokwenda huko tuenendeni na mchango wa Tshs.100 tu kwa ajili ya vyombo vya kazi. Mliopona mfungulieni akaunti ili chombo cha usafiri kipatikane. msiwe kama wale kenda. kwa serikali acheni unafiki wa kisiasa kwani angekuwa mzungu kavumbua mngempatia huduma zote tena kwa siku moja tu. mbona tunawashuhudia mkiparamia safari za nje kila leo kwa ajili ya semina zisizokwisha za magonjwa hayo sugu. ama kweli nabii kwao haku...
 
Sifa, heshima na utukufu vimrudie Mungu aliye juu, maana sasa watu watajua kwa jina la Yesu wagonjwa wote wanapona, maana pale kwa babu ni dawa na maombi. makabila yote ,mataifa yote,dini zote, wanapata huduma bila upendeleo.... ifikie mahali watu wote wajue kwa jina la YESU kila mtu anapokea uponyaji....
heshima kwa babu kwa kufanya kazi ya Mungu kwa uaminifu
 
mbona wamasai wengi mitaani wanapitisha kuuza mitishamba na hawaulizwi....? there is something fishy with this government
 
, mbona hospital nyingi mazingira machafu tu na zahanati za serikali lakini hazifungiwi? na ikienda kwenye maabara haitaonyesha maana ni swala la imani, watakuja na matokeo kwamba in kemikali za sumu, wanaipeleka ulaya wazungu wanaifungia maabara. babu ndo kwisha hivyo waliopona bahati yao, ila najua viongozi wa serikali wataenda kwa siri
 
waongo haoooooooo!! wanataka waanze kwenda wabunge na mawaziri hawana lolote!!
 
Kwa ufahamu wangu, babu kazuiliwa kwa muda kutoa huduma kutokana na wingi wa watu na mazingira magumu ya huduma za kijamii kama maji, choo, vyakula, barabara, malazi nk. Kazuiliwa kwa muda mpaka waliopo waishe ndio wengine waendelee kwenda.
 
thtz not fair at all respect...where is my Damn GUN?
 
tupo zama gani tanzania
hivi watanzania tupo zama gani ? na hapa tupo na serikali au ndo siasa za kuogopana kama tunaamini fortune teller si tungempatia ward hapa Kcmc au hospital yoyote ya taifa,au hatujui thamani ya roho za watu,wagonjwa wengi wanatoroshwa mahospitalini wakiwa na hali mbaya kupelekwa kwa babu loliondo na matokeo yake wanafia njiani kutokana na hali mbaya za kiafya mbaya zaidi na
watu waliopo kwa babu wakianza na magonjwa ya tumbo au milipuko ya kipindupindu huyu babu mganga wa loliondo atawamudu?embu tuamue kitu kimoja wajameni kama tumeamua kuamini mambo hayo basi aletwe arusha mjini hapo kutakua hakuna haja ya kutumia nauli kubwa kama ilivyo sasa na ni mjini hospitalini so inakua rahisi hata ikitokea milipuko jinsi ya kusolva sasa nambie mtu umeanzia kuhara toka loliondo kama ni kipindupindu usafirishwe kilometa 400 mpaka town si utafia njiani
 
Kupima ufanisi wa kitu kuna njia nyngi: mfano, ufanisi wa mkandarasi unaweza kupimwa kwa kupima ubora wa jengo au barabara aliyojenga na si kukagua vyeti vyake au zana alizotumia. Nawashauri wapime wagonjwa kama wamepona au la.

Ndugu yangu kupima ufanisi na kupima kilichopelekea ufanisi ni vitu viwili tofauti
Kwa mifano uliyotoa, ile sementi, nondo n.k navyo vilipimwa kama vinaweza kufanya ujenzi huo ndiyo maana kuna TBS kwa hapa TZ
Mkandarasi anapimwa ufanisi kama amevitumia vipelekea ufanisi kisahihi ambavyo hupelekea uimara wa ujenzi huo
Wizara inachotaka kupima ni je hii dawa ni kitulizo tuu ama ni ya kutibu kwa kudumu? Je endapo inavilaza virusi, bacteria n.k kwa miezi au miaka kadhaa tu na kurudi na mashambulizi itakuaje?
We real need to think about it very very carefully
 
Ni meshtushwa na kauli ya serikali kuwa sababu mojawapo ya kumfungia mchungaji ni kutojaregister dawa yake .

Serikali inashindwa kutoa ushirikiano na babu na kuhakikisha watu wanapata uponyaji kwa mpango mzuri na gharama nafuu.

Swali langu, serikali ni wivu au ninini kinacho wafanya wachukue hii hatua ya kumfungia babu?
Waganga wote wa kienyeji Tanzania wameregister dawa wanazo wapa watu?
Je babu atafungiwahadi lini? au ndio kama mgao wa umeme, hatima ya kufungiwa kwa babu haijulikani?

Mawazo yangu;

Serikali ingeangalia uwezekano wa kumsaidia babu kuweza kutoa hiyo huduma kwa kupeleka huduma zingine muhimu kama jeshi kwenda kujenga vyoo vya kutosha.

Kusaidia kuingiza watu wachache kijijini kwa kuhakikisha wanaingia kwa mpango wa wachawachache.

Pia kuweka hata huduma ya kwanza pale kwa babu.

Hawa wagonjwa na ndugu za wagonjwa wanao amini kuwa babu atawaponya wanaiangaliaje serikali na sijui kama serikali imejiuliza kuhusu hili, kwani hapo ni sawa na kumkatili mtu maisha.

Ombi langu serikali iiangalie ni vipi babu ataendelea na huduma mapema bila kuchelewa kuliko kufunga bila kutangaza the way forward.
 
Ah? Jibu ni rahisi sana. Hiyo ni influence toka nje, hasa kwenye HIV. Ukimwi ukimalizwa bongo haya mashirika yao yatakuwa hayana tena ishu, afu yataondoka, kitu ambacho serikali za magharibi hazitaki kusikia!
 
Duh!But same time unachozungumza ni ukwel ila huy Babu anavyosema hawez kutoka katik hilo eneo aliloambiwa na Mwenyezi MUNGU.
Source Raia Mwema
Tarehe 9-03-2011
 
serikali ina lake jambo kwani wanata kumuibia babu dawa ili wenyewe wajitangaze kuwa ndo waliogundua dawa ya ukimwi hapo wamegonga mwamba kwa babu kapewa hiyo dawa na mungu hawataweza heheeeeeeeeeeeeeeeeeee imekula kwaooooooooooooo
 
Ndugu yangu kupima ufanisi na kupima kilichopelekea ufanisi ni vitu viwili tofauti
Kwa mifano uliyotoa, ile sementi, nondo n.k navyo vilipimwa kama vinaweza kufanya ujenzi huo ndiyo maana kuna TBS kwa hapa TZ
Mkandarasi anapimwa ufanisi kama amevitumia vipelekea ufanisi kisahihi ambavyo hupelekea uimara wa ujenzi huo
Wizara inachotaka kupima ni je hii dawa ni kitulizo tuu ama ni ya kutibu kwa kudumu? Je endapo inavilaza virusi, bacteria n.k kwa miezi au miaka kadhaa tu na kurudi na mashambulizi itakuaje?
We real need to think about it very very carefully

babu anasema dawa hii utapona kama utaitumia na kuamini kwa imani yako kwamba umepona.... sasa unataka kuichunguza chunguza tuu ... hii ni dalili ya kutoiamini dawa hii kwa imani ya kisayansi (which you stand on) ..... this kind of healing is of its own and of the very recent century ..... aliyeigundua kwa uwezo aliopata kwa namna yeyote ndiye anayeweza kutupa options za kutoa uhakika zaidi na siyo intruders (government)
 
babu anasema dawa hii utapona kama utaitumia na kuamini kwa imani yako kwamba umepona.... sasa unataka kuichunguza chunguza tuu ... hii ni dalili ya kutoiamini dawa hii kwa imani ya kisayansi (which you stand on) ..... this kind of healing is of its own and of the very recent century ..... aliyeigundua kwa uwezo aliopata kwa namna yeyote ndiye anayeweza kutupa options za kutoa uhakika zaidi na siyo intruders (government)

SWALI: Je waliotumia wote na wakajiona wamepona wanaimani sawa zinazolingana ?????
 
SWALI: Je waliotumia wote na wakajiona wamepona wanaimani sawa zinazolingana ?????

mkuu ... mungu ni yule yule ...jinsi ya kumjua , kumheshimu na kumwomba ndiyo inayopelekea kuwa na imani tofauti ...... imani anayosema babu ni ya aina yeyote ile ....! wamepona watu wa imani mbalimbali na hakuna doubt ya imani fulani kwa babu ...
 
Ah? Jibu ni rahisi sana. Hiyo ni influence toka nje, hasa kwenye HIV. Ukimwi ukimalizwa bongo haya mashirika yao yatakuwa hayana tena ishu, afu yataondoka, kitu ambacho serikali za magharibi hazitaki kusikia!

Kwa ujinga ujinga tu watanzania wanauua hii kitu, si muda tutasikia huu mti umegundulika na mmarakani miaka ya 90
 
Mbona hayo maswali yako zaidi upande wa serikali kuliko Babu? kwani watalii wanapokuja kutembelea wanyama mbugani na Ngorongoro crater mbona hatulalamiki kuzihamishia Dar ambako kuna facilite zote? Kumbuka babu kapewa karama ya kutibu katoa utaratibu ambao mimi nauona wakimungu zaidi...uwe na imani, uwe mnyenyekevu (nipamoja na kukubali hadharani kwamba babu ndiye aliyekusaidia na ndoto yake) and na yeye ili aweze kuhold anointing utii ndo agizo pekee so yeye amsikilize nani? Ninyi walalamikaji ambao hamtaki ku facilitate utaratibu wa babu uendelee kufuatwa bila yeye kukosa utii au yeye awasikilize ninyi na hiyo anointing iondoke watu waendelee na shida zao kama mwanzo? Babu is not a panacea but a contributor to problem ruduction kwa magonjwa sugu kumtupia lawama ya watu wanaokufa is not fair wengine wanatakiwa wasaidie kuweka coordination office sehemu kama Arusha na wagonjwa waliozidiwa wapewe priority badala ya kujaza FFU kule basi watu wangeruhusiwa kwenda kumwona babu kama wanavyopanda Mt. Kilimanjaro..ili babu awe free na tuhuma zenu za rushwa kama mtapenda kuingiza rushwa kama ilivyo desturi yetu hapo nyumbani kwani amekataa hayo kufanyika?

I totally disagree. You cant compare wildlife safaris and this unbelievable thing ambayo huyu babu anafanya. First of all, huko mbugani kwa watalii kuna hotels and lodges na kuna first AID treatment kama kuna mtu atapata shida yoyote. For your information kuna mpaka private planes za kuwakimbiza hao watu mahospitali for further check ups kama watazidiwa. Now I know you will ask me what about the poor ones who cant afford and my reply is, wildlife safaris are luxuries so if you cant afford then DONT GO.

Back to our topic. Kwa nini babu wa Loliondo asikubali dawa zake kuchunguzwa if there is nothing wrong with it? Si anaclaim kuwa Mungu ndio aliyempa ndoto ya huo mti kwa nini asikubali wakauchunguza maana si watakuwa wanachunguza kazi ya Mungu na siyo ya kwake, sasa kwa nini aikatalie serikali? Mbona Yesu alivyoitwa kwa Herode hakukataa alienda na akawaeleza wazi kuwa MIMI NI MWANA WA MUNGU. Maana tunaambiwa katika Biblia kuwa vita yetu si ya mwili na siyo sisi tunaopigana bali ni Mungu ndani yetu, kinachomfanya huyo babu apigane vita ya Mungu ni nini? Tunaambiwa tiini mamlaka mliyopewa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu siyo? Yeye anaitii? What is he hiding???


My point of view: This thing is a BIG LIE. Why, because if God wanted to heal so much people at one time, he would have done it already. Why now? Because Tanzania is the perfect country of all? I have no doubt that God can choose someone to represent him but why choosing one person only? Huyu babu anasema kama utachukua the same dawa unywe mwenyewe haitafanya kazi ina maana huyu babu na sisi yeye ndiyo bora zaidi mbele za Mungu kiasi kwamba kupitia yeye tu ndio tupone? ndio maana nikakuuliza vipi kuhusu wagonjwa maskini ambao hawana uwezo wa kumfikia? Hawana means yoyote ya transportation ina maana hao hawatapona kama ni yeye pekee ndio anatoa dawa? Huoni kwamba Mungu atakuwa anapendelea wenye fedha tu, kama ni kweli huyu babu katumwa na Mungu?

What is his goal, huyu babu, what is his goal? Yes, huyu babu atatutibu tutapona, then what? Then we go back to our sinful life like always? Let me tell you something..... God is not interested in healing our bodies but he is interested in healing our hearts and mind, because he knows that our hearts are the MOST manipulating thing in human beings. God knows he has to heal our hearts first so we can change our stupid thoughts towards certain things in this world. Jesus healed people but his mission on earth wasn't to heal anyone, his mission was to preach the word of God so that people can know, understand and love his FATHER. He healed people because he saw the way wayahudi hawakumwamini so ilibidi atoe ishara ili waamini. It doesnt matter if you are blind, deaf, or HIV positive, to God you are the loving son if you will follow what he wants.

Watanzania especially christians, tutakufa kifo kibaya sana siku moja. Tena kitaitwa kifo cha kujitakia. Mkumbukeni Kibwetere wa Uganda, na yule mzungu aliyeenda Gayana kama sikosei miaka ya 70 (South America) akaua watu zaidi ya mia mbili kwa kuwahubiria neno la Mungu na baadae akawapa dawa akiwaambia itawatakasa dhambi zao. We have to be critical in things, and not being easy in accepting everything just because he said God sent him. Watu wa namna hii wamekuja na wamepita na wataendelea kuja.

NB: I work in one of the biggest HIV clinics in this country and so many patients have taken the dawa but not a single one amepona, most of them children so I REALLY WONDER!!!!!!
 
Back
Top Bottom