Babu wa Loliondo afungiwa kwa muda kutoa huduma...

Babu wa Loliondo afungiwa kwa muda kutoa huduma...

hii imekaa poa,kupimaaaa kupimaaaaaa, sisi tunataka dawa tupone full stop.
Babu is not looking for fame anafanya aliyoagizwa, wanamdistract tuu na sayansi hapa, waende hukoo...:hand:
kwani wamespend how many years na dawa ya UKIMWI/KANSA/SICKLE CELL hawajazipata leo babu wanataka kumpima, ebo!! huo ni ushankunaku:hand:

Babu amekwambia anatibu kwa dawa ya mti aliooteshwa pamoja na maombi. Sasa unaweza kuyapima maombi kwa kisayansi!
 
Ni vizuri kuwa na mashaka lakini ni bora kuelewa kuwa katika mambo haya imani ndiyo inatakiwa kutangulizwa. Kwani imeandikwa "heri aaminiye bila kuona."

Lakini huwezi tu kuelewa for the sake of kuelewa. Lazima wote tujiulize maswali na siyo kukubali kila kitu tuambiwacho kama watoto. Hata kama ni swala la imani still... as long as we haven't actually talked to God himself, we have to ask questions maana kuna miungu wengi sana duniani. Na manabii wa uongo wako kila kona
 
hii imekaa poa,kupimaaaa kupimaaaaaa, sisi tunataka dawa tupone full stop.
Babu is not looking for fame anafanya aliyoagizwa, wanamdistract tuu na sayansi hapa, waende hukoo...:hand:
kwani wamespend how many years na dawa ya UKIMWI/KANSA/SICKLE CELL hawajazipata leo babu wanataka kumpima, ebo!! huo ni ushankunaku:hand:

Akishawaponya, then what?
 
Ukiachilia mbali ukweli kuwa dawa ya babu inamaombi pia, ambayo TFDA hawawezi kuyapima, Hivi TFDA wamethibitisha ubora wa dawa za wamasai na waganga wengine hadi wahitaji kuipima ya babu ?
 
kama maombi mungu yupo popote akikuombea utapona. na kama ni mitishamba basi ukinywea popote unapona. vp babu ang'anga'nie huko. mleteni mjini arusha kama ataki ujue tapeli huyo tena ni mtandao mkubwa tu. wanafanya b'ness ya vyakula, usafir,vinywaji, na fee. maaana kwa siku watu 2000 mara sh 500= 1,000,000/= aisee kwa mwezi 30,000,000 jumlisha na usafiri, 100,000 kwa kila mtu atakae tumia usafiri wa wajanja fulani. nasikia kuna madalali huko. Mleteni Arusha aumbuke huyo babu
 
kwa nini tusiombe invisible atuwekee ngumi kwenye keyboard ili mtu akikuboa unampa kitu inauma.....nadhani tungeheshimiana

hii ingewezekana nadhani member wa jf wote wangekuwa wanavaa helment
 
tupo zama gani tanzania
hivi watanzania tupo zama gani ? na hapa tupo na serikali au ndo siasa za kuogopana kama .....

... Thanks brother. Kila siku najiuliza maswali haya. Majibu yatokanayo ni pamoja na kubobea kwenye ... MAMBO YA HOVYO HOVYO... katika kila nyanja. TUPO NA SERIKALI?? The rule of law and order havipo kabisa. Watu wanajiamulia tu kutoka nje ya mstari bila impunity. Leo hii unaweza fungua mgahawa katikati ya barabara. Magari yatakupisha tu. Wateja kibao utawanasa na thubutu ingilia hapo. Hakuna tofauti na ya Loliondo. Ishu za tiba katika dunia ya leo si dhihaka. Ndio maana sambamba na masuala ya dawa kunajitihada kubwa za kupamabana na yale madawa FEKI. Hili lipo! Sasa tukiachana na hayo, nilikuwa DaresSalaam last week. Leo hii najiuliza, jiji kubwa lenye idadi ya watu karibu millioni tano. Garbage collection inafanywa na mikokoteni! Sewerage system usiseme. Migari ya mamillioni ya shillingi kibao. Sitaki kujadili niwaonao ndani ya hiyo migari ila nitumie neno kichefuchefu. Hivi kwa Tanzania SERIKALI inamaanisha nini?
 
Wameona wao wameshaenda wote sasa wanazuia walalahoi. Kama kawaida yao nchi hii mlalahoi hathaminiwi. Mbona hawakuzuia tulipokutana huko na Kandoro, IGP mstaafu Mahita, Ndesamburo and the rest?? Au wanataka tuweke list yao wote hapa tuliokutana nao?
 
Hukuelewa mkuu na madai mengine ni kwamba dawa zake hazijasajiliwa na maji atumiayo ni machafu

Laki we kweli unategemea Loliondo utapata maji safi na salama ya kuweza kunywesha makumi elfu ya watu kwa siku...kila siku?! Hapo bado vyoo vya kujisaidia...Ingezuka 'kipindu pindu' pale ni serikali hii hii ingelaumiwa! Ndio, si sahihi kuzuia watu kupata dawa kwa magonjwa yao (ni kosa la kisheria kama dawa ina uthibitissho wa kisayansi kuwa inatibu halafu mgonjwa akazuiwa hasiipate) lakini pia ni muhimu kuzingatia uwezekano wa matatizo mengine kuibuka kama hilo la magonjwa ya mlipuko.
 
Mi naona aibu kwenda coz ni mtu mzito sana halafu kwenda natamani sasa nifanyeje?

Mkuu kwani una kila ngapi? kwenye red hapo umesema ni mzito sana. Mi nakushauri upungue uzito then utaweza kwenda
 
Kwa ujinga ujinga tu watanzania wanauua hii kitu, si muda tutasikia huu mti umegundulika na mmarakani miaka ya 90

Lakini mti haufanyi kazi mpaka babu afanye makarateka yake. Ukisikia ukoloni mamboleo ndo huu, wanaendelea kuukumbatia UKIMWI kwa manufaa yao!
 
Dawa hii inaambatana na suala la imani. Nina wasiwasi na hivyo vipimo/utafiti wanaotaka kuufanya kama utaleta matokeo sahihi hasa ukizingati watu waliojichotea dawa na wakapata madhara.

Serikali yetu imelala usingizi, tena usingizi wa Pono. Tungekuwa na watu sharp, leo hii tungekuwa tunazungumzia juu ya kuimarisha miundombinu katika eneo hilo, tungekuwa kama nchi kufanya jitihada za makusudi ili kuwafanyia utafiti wagonjwa waliokwisha pona ili kujiridhisha.
Hii ingekuwa oportunity nzuri kwa serikali yetu kujitangaza kimataifa ambako hata utalii wetu umeshindwa kulitangaza Taifa letu kwa kiwango stahili. Watu wangapi wataingia nchini tukifanya hivyo? guess pesa ngapi zitakusanywa nchini kutokana na kodi/ada mbalimbali? Serikali msaidieni huyo Mchungaji kwa mambo ya msingi ikiwa ni pamoja na kuratibu zoezi zima la watu kufika kule badala ya kuleta blabla za kitaalamu magharibi hapa. Watu tunataka kunywa dawa, tunataka kupona fullstop.
HIVI TUNATAKA MUNGU ATUBEBE NAMNA GANI?
 
Ndugu wapendwa
akuna asiejua hawa viongozi wa afya walivyo jilimbikizia ma duka ya dawa mbalia mbali na
hospital za vichochoroni ziisizo na idadi huku wakijumuika na jamaa wa madawa
kuwaibia watanzania..leo hii watanzania wengi wananunua dawa zinazoaminika kupewa bure
ukienda muhimbili dawa za tb ukimwi bure lakn mpaka upate umege kidogo ndio wanakukumbuka

sasa leo ameshuka NABII WA MBEYA awa mashetan wanaona awapati fedha kama zamani wanataka turudi kwenye ma kemikal yao nasema babu tutakulinda mpaka kufa na loliondo tutakuja else waweke uzio kati ya babu na sisi

ALUTA LOLIONDO
 
Jamani hii ikoje? Waislamu wenye siasa kali hupenda sana kuwakataza waislamu wenzao wasishirikiane na Wakristu maana wakristu ni makafiri wasio na dini. lakini cha ajabu ni kwamba mpaka sasa sijasikia kukatazwa waislamu kwenda kwa BABU anayetibu kwa kutumia imani ya kikristu!! Nilitegemea kwa mfano Radio Imani ya Morogoro ingekuwa imetoa tamko la kuwakataza waislamu wasijihusishe na huyo BABU. Ikoje hii??

Nawasilisha
 
Serikali kupitia wazara yake ya afya inge anza kwanza na dawa za isaac wa ndoodi ( yule tapeli anayejitangaza kwenye ma TV) kabla haijaanza kuweka mizengwe kwenye dawa za babu, au kwa vile babu ajakata 'kitu kidogo' kama akina ndoodi
 
Huwa unasikiliza radio Imani? Kama siyo, huna haki ya kusema usemayo. Sijui hata kama post zingine huwa unasoma.Tafadhali siku nyingine usikurupuke kama leo.JUBU:Waislam wanajua sheria zinazowaongoza na wapo pia wengi tu hawajui.Radio imani tayari wamezungumza maranyingi tu.
 
Kama wamezungumza hiyo ni dhahiri kumbe huwa hawasikilizwi na waumini wao maana tumeshuhudia wengi wakienda kupona.
 
Umaskini ni mbaya,na inapofikia hatua watu wanakosa imani na hospitali zao chochote wataamini
 
Huwa unasikiliza radio Imani? Kama siyo, huna haki ya kusema usemayo. Sijui hata kama post zingine huwa unasoma.Tafadhali siku nyingine usikurupuke kama leo.JUBU:Waislam wanajua sheria zinazowaongoza na wapo pia wengi tu hawajui.Radio imani tayari wamezungumza maranyingi tu.

Wamesemaje? Umeguswa nini kaka? Wewe ni juma na umekwenda kwa BABU??
 
Kaka ugonjwa hauna dini na wala usiwazuie viumbe wa Mungu kwenda kupokea uponyaji kwa jina la MPONYAJI WA AJABU.
 
Back
Top Bottom