Babu wa Loliondo afungiwa kwa muda kutoa huduma...

Babu wa Loliondo afungiwa kwa muda kutoa huduma...

Kama ingekuwa waislamu wanakataza waumini wao wasipewe tiba basi wangekatazwa hata kwenda kutibiwa kwenye hospital za Mission.
Mtoa mada tafadhali usijaribu kuleta udini.
 
Jamani hii ikoje? Waislamu wenye siasa kali hupenda sana kuwakataza waislamu wenzao wasishirikiane na Wakristu maana wakristu ni makafiri wasio na dini. lakini cha ajabu ni kwamba mpaka sasa sijasikia kukatazwa waislamu kwenda kwa BABU anayetibu kwa kutumia imani ya kikristu!! Nilitegemea kwa mfano Radio Imani ya Morogoro ingekuwa imetoa tamko la kuwakataza waislamu wasijihusishe na huyo BABU. Ikoje hii??

Nawasilisha

Non Sense. Udini mtupu
 
Kufuatia ujumbe uliotumwa na wizara ya afya na ustawi wa jamii kwenda Loliondo kwenda kuangalia uhalali wa matibabu yanayo tolewa na babu inasemekana babu hakuwa tayari kuruhusu wataalam hao kuipima dawa yake. ndugu wanajamii je hiyo imekaaje?

Wizara ya Afya ni wanafiki wakubwa. Kwanini wakapime dawa ya mtu wao kama wangekuwa wakweli basi wangefuatilia wagonjwa wanaotibiwa kutoka kwa babu na kujua maendeleo au hali zao compare na zamani.

Tusiongopeane hapa ni wanafiki wakubwa hao wanataka tu kumwibia tecknology yake
 
Ktk utafiti uliofanywa imeonekana kuwa tanzania ndio nchi ya mwanzo barani africa kwa kuamini mizimu, uchawi na ushirikina. Haya nendeni wajinga.

kuna JF members wengi tuu wameenda na wanaendelea kwenda kwa babu na wewe unawaita wajinga haya ma mods mmelala au mko macho? huyu jamaa mnaturusu tumshukie mithili ya katyusha missiles zinavyoshuka ardhini?
 
kwani huyo Babu amewaita watu waende huko? Au wanaenda wenyewe? Halafu acheni ubinafsi kila kitu kizuri kiwe dar na arusha tu! Hata loliondo kuna watu ambao wananufaika na huyo Babu
 
Kama ingekuwa waislamu wanakataza waumini wao wasipewe tiba basi wangekatazwa hata kwenda kutibiwa kwenye hospital za Mission.
Mtoa mada tafadhali usijaribu kuleta udini.

Mimi siyo mdini ila waislamu wenye siasa kali ndiyo wadini na wachokozi. Wanasema mtu yeyoyte ambaye siyo mwislamu ni kafiri, yaani hana dini. sasa iweje waende kwa babu anayetibu kwa imani ya kikristu? Hospitali binfsi hawatibu kwa imani ya kikristu, wanatibu kwa imani ya kisayansi
 
Huo uchunguzi wa huyo dawa wanaotaka kuufanya ni janja ya kuiondoa hiyo dawa sokoni ili waendelee kununua ARV,tangu lini mambo ya Mungu yakachunguzwa kwa darubini?
 
Mmh kuna watu wanapenda udini? Mbona huulizi wakristo wanaotibiwa na madaktari waislam?
 
Lakini mti haufanyi kazi mpaka babu afanye makarateka yake. Ukisikia ukoloni mamboleo ndo huu, wanaendelea kuukumbatia UKIMWI kwa manufaa yao!

Watamlazimisha babu awaelezee, mara tutasikia fisadi ndodi ndiye anayetibu kwa mti huo
 
Mambo haya yafuatayo yatasababisha dawa ya babu kufungiwa:
1. Ufisadi - makampuni yanayo agiza dawa mbalimbali yatatumia uwezo wao wa kifasadi kushawishi serikali ili waendelea kutunyonya wavuja jasho
2. Kimataifa - ile mijamaa ya inayotengeneza dawa za kibepari haitakubali kwa kuwa babu ataua soko lao
Naomba kuwakilisha
 
Kwa kweli nimeandika kwa uchungu sana kwa kuwa watanzania wenzangu wataendelea kufa mpaka lini wakati babu yupo?
 
Tuanadamane kama nchi za kiarabu kuilazimisha serikali isiyo halali ya kibongo kuto zuia utumiaji wa dawa hiyo
 
Lazima wamzuie, Semina na makongamano ya ukimwi na kansa zitaisha huko wizarani, kakobe atafurahi sana atajua ni maombi yake

Japokuwa umeongea kwa ufupi sana, lakini kauli yako ina ukweli mwingi. HIV tiba yake inasumbua kwa sababu baadhi ya watu wananeemeka sana na uwepo wa ugonjwa huu,...... hii ni vita kati ya Mungu na Sshetani..
Upinzani dhidi ya dawa za hiv (kwa maslahi) ndizo zina/zimechelewesha tiba ya tatizo hili,............
 
Mkubwa ndevu hizo zote ni dalili za udini hakuna lolote la maana hapa. Wizi mtupu. I have no comments on this matter.
 
BAADA ya kutumia musuli wa fedha na kuweza kuonana na Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila wilayani Loliondo mkoani Arusha, na kuwaacha wanyonge wakisota, sasa vigogo hao huenda mambo yakawatumbukia nyongo.

Mchungaji Masapila ameapa kuwa vigogo waliofanya hivyo kwa kutumia njia za mkato na kufanikiwa kumwona na kunywa dawa, hawatapona magonjwa sugu yanayowakabili.

Mchungaji huyo mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) amesema hali hiyo imesababishwa na kitendo chao cha kukiuka baadhi ya masharti ya tiba yake ambayo inakataza kufanyiwa biashara na wala kupewa upendeleo.

Hivi karibuni, baadhi ya maofisa wenye vyeo katika sekta mbalimbali nchini,
walidaiwa kutumia nafasi zao kushawishi askari wanaolinda usalama katika makazi ya Mchungaji Masapila, ili kuwavusha foleni na kupata tiba haraka.

Polisi walio eneo hilo kijijini Samunge, tarafa Sale, pia wamedaiwa kutumia nafasi zao kupitisha ndugu, jamaa na marafiki zao, jambo ambalo Mchungaji Masapila alionya kuwa halitawasaidia kwani dawa hiyo haifanyi kazi katika mazingira hayo.

"Huu ni uponyaji wa Mungu na Mungu huwa hatambui cheo au nafasi ya mtu, ukikosea utaratibu dawa inabaki kuwa maji ya kawaida," alifafanua Masapila.

Maelfu ya watu kutoka pande zote za nchi na nchi jirani wako katika kijiji hicho kwenye mbuga ya Sonjo, kata ya Digo-digo, Ngorongoro wakitumaini kupata tiba hiyo ya ajabu.

Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali, alisema jana kuwa ofisi yake inafikiria kutenga siku maalumu na hasa Jumamosi, kwa watumishi wa umma na Serikali kwenda kupata tiba hiyo ili kupunguza msongamano na kuwawezesha kurudi mapema kwenye kazi zao za utumishi kwa Taifa.

Hata hivyo, haijulikani kama Mchungaji Masapila atakubaliana na wazo hilo, kwa maana alisisitiza kuwa mtoaji huyo wa dawa anazingatia kutokuwapo kwa upendeleo katika utoaji tiba hiyo.

Katikati ya wiki hii, vurugu zilidaiwa kuzuka karibu na eneo la tiba, baada ya watu wanaodhaniwa kuwa vigogo kulazimisha kuwapita wananchi wengine waliopanga foleni kwa ajili ya kupata tiba.

Hivi sasa watu wanalazimika kukesha kwa siku nne wakisubiri zamu ya kupewa dawa na Mchungaji Masapila ambaye sasa amepata usaidizi wa wachungaji wengine watatu wanaomsaidia kuchota dawa.

Hata hivyo, Masapila analazimika kugawa dawa hiyo kwa mkono wake mwenyewe, maana bila hivyo, tiba hiyo inayotokana na mizizi iliyochemshwa na maji, haitafanya kazi.

Mkazi wa Sonjo aliyevamia moja ya masufuria na kujichotea dawa na kuinywa Jumatatu alipata msukosuko mkubwa kwani tumbo lilipata maumivu makali na kulazimisha ‘Babu’ Masapila kuingilia kati kumsaidia.

Wakati hayo yakiendelea, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Akili Mpwapwa, alisema Jeshi bado halijapokea taarifa rasmi za vifo vinavyodaiwa kutokea katika mbuga ya Sonjo ambako maelfu wamepiga kambi wakisubiri tiba.

Hata hivyo Lali juzi alithibitisha vifo sita kati ya 14 vinavyodaiwa kutokea katika eneo la Samunge.

Lali alipozungumza jana na gazeti hili, alisema misururu ya watu wanaofuata matibabu imepungua na kubaki umbali wa kilometa 15 huku magari yakibaki kati ya 1,000 na 1,500 kutoka ya awali 3,000.

Alisema katika magari hayo yakiwamo malori na mabasi na magari madogo kila gari lina watu wasiopungua watano.

Kwa mujibu wa Lali, mtu mmoja alifariki dunia wakati akisubiri matibabu na alikutwa jana walipotembelea eneo hilo.

Mkuu wa Wilaya alisema watu wamekuwa wabishi kwa kutoa wagonjwa hospitalini wakiwa mahututi na kuwaweka mistarini kwa ajili ya kupata dawa na hivyo kuzidiwa na kufariki dunia.

Mchungaji Masapila hutoa dawa hizo anazodai kuoteshwa na Mungu kwa Sh. 500 huku akidai kutibu magonjwa sugu yakiwamo ya Ukimwi, pumu, kisukari na mengineyo huku dozi yake ikiwa kikombe kimoja tu cha dawa hiyo.

Inadaiwa kuwa kutokana na misururu hiyo, gharama za magari zimeendelea kupanda kwani sasa wanaokwenda kwa magari ya kitalii wanalazimika kulipa kati ya Sh. 120,000 na Sh 150,000 na mabasi ni kati ya Sh 30,000 na Sh 50,000.
 
Jamani hii ikoje? Waislamu wenye siasa kali hupenda sana kuwakataza waislamu wenzao wasishirikiane na Wakristu maana wakristu ni makafiri wasio na dini.Nawasilisha
Mkuu Mawenzi.
Tofauti ya hao unaowasema hapa na wewe muna tofauti gani?
Wewe pia unapendelea hao waislamu wenzao wasiende kwa babu?
Ungekuwa tofauti na hao wa siasa kali basi mada yako ingekuwa on a positive note kusema wagonjwa bila ya kujali imani zao wanamiminika kwa babu kupata tiba.

Kwa nini ndugu zangu we fall into this mtego wa udini?
Waislamu na wakristo wa nchi hii wameshirikiana siku zote.
Najua kuna juhudi zinafanyika kufarakanisha makundi haya. Hao wa siasa kali kutoka pande zote wanachochea mfarakano...sasa ni vyema sisi tuone udhaifu huu na tuupige vita.

Inawezekana hukuwa umekusudia hilo la kufarakanisha lakini kwa bahati mbaya kwa ulivyoileta mada yako inataka msuguano uendelee. Yale ya Mto wa mbu yawe somo kwetu.
Tuungane kupinga kugawanywa. Na kila mtu abaki na imani yake na aheshimu imani za wengine.
 
Wengi wamepona na wake zao wanasema wanahisi kama vile wako kwenye enzi za uchumba baada kuishi kama kaka na dada kwa muda mrefu kutokana na mathara ya kisukari. Siyo maneno yangu ni ya mmoja wa mwanamke ambaye mumewe amepona sukari.
 
''Kwenye mambo ya tiba la muhimu kupona kwanza mengine baadae! Kama huamini jaribu kuchunguza wanaotoka kwenda kuombewa wakati wa mikutano ya injili utagundua hata wa dini nyingine wamo kibao. acha waitafute kweli ili wawe huru tena huyo mzee angeongeza kipengele cha kila anayetaka tiba kumkiri Yesu Kristo kwanza ndiyo apate kikombe cha uponyaji, nafikiri angesaidia sana hata kupunguza mafisadi katika nchi hii hata hivyo moja ya sharti kubwa ba mtumishi huyo wa MUNGU ni mtu yeyote anayepokea hicho kikombe kutofanya dhambi tena, nafikiri huo ni mtihani mgumu kushinda yote ila atakeyemudu hilo sharti atashinda.
 
Back
Top Bottom