Babu wa Loliondo aoteshwa tena kikombe; Asema wengi watakifuata

Babu wa Loliondo aoteshwa tena kikombe; Asema wengi watakifuata

26252
Mkemia,haaa haaa makoti yake yalikuwa yanatisha
 
Mkemia mkuu wa serikali[emoji23] [emoji23] hadi sizonje alienda chezea mkemia
 
Watanzania wengi ni wagonjwa, babu aliiona fursa akapiga hela na sasa anataka kurudi kivingine..
Waliokosa nafasi kwenye meli ya Wachina wasubiri Episode 2 ya Kikombe.
 
Aisee nmecheka hii picha dah huyu babu wa loliondo ni mkemia wa wakemia wotee duniannniiii
 
DQ0R4AbW0AA5Okp.jpg
Mchungaji Ambilikile Mwasapile maarufu Babu wa Loliondo aliyehudumia maelfu ya watu ndani na nje ya nchi kwa dawa aliyoitoa kwa kipimo cha kikombe amedai ameoteshwa kuwa umati utarudi kijijini Samunge kupata dawa.
Amesema ana uhakika wa jambo hilo kwa kuwa hata mwaka 2011 kabla ya maelfu ya watu kufika nyumbani kwake alioteshwa, hivyo amejiandaa kuweka miundombinu bora zaidi na hasa ujenzi wa vibanda atakavyovitumia kutoa huduma.
Mchungaji Mwasapile alisema hayo jana Jumapili Desemba 10,2017 mbele ya ujumbe wa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Joseph Kakunda aliyekuwa mkoani Arusha kukagua miradi ya maendeleo, ikiwemo ya kuwawezesha wananchi kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Miongoni mwa waliofika kupata ‘kikombe’ kwa gharama ya Sh500 mwaka 2011 walikuwemo wafanyabiashara maarufu, wanasiasa na viongozi waandamizi serikalini.
Akizungumzia dawa yake anayodai inatibu maradhi mengi amesema kwa sasa anaitoa kwa watu wachache wanaofika kijijini hapo.

SOMA ZAID >>>
 
Huyo babu ajue kwamba bahati haiji mara mbili. Ule umati wa ajabu alioupata 2010/2011 hatauona tena ng'o!
 
Nimeangalia ITV jana,sikumbuki ni kipindi gani ila palikuwa na uonyeshwaji wa Babu wa Loliondo na maendeleo aliyoleta katika eneo.

Taasisi za serikali ikiwemo NIMR zilishughulikia suala la kikombe na naamini report yake ipo.

Kwa mwendo huu wa kushangilia kila bila kufikiri,nahisi janga lingine lipo njiani.
 
Back
Top Bottom