The Icebreaker
JF-Expert Member
- Feb 11, 2018
- 22,278
- 65,817
Hapo ukipata zile karatasi za kuandikia barua za rangi ya light blue zilizoandikwa By Air unajiona lazima demu akubali ombi lako,Zile zama hazirudi tena."Utakapo kujua hali yangu mimi ni mzima wa afya hofu na mashaka n kwako wewe uliye mbali na upeo wa macho yangu❤, usiku kucha silali nakuota wewe, nikinywa maji nakuona kwenye glasi....wallahi ntakunywa sumu juu yako"
Hapo barua imechorwa moyo na mkuki umepita katikati kuonyesaha namna gani mtu anaumia. Karatasi imepuliziwa marashi kama yote. Enzi zile hebu na zirudi basiii Shadeeya😀😂😀