"Baby umependeza" Je umechangia sh ngapi au umenunua kipi? Wanaume mnaboa

"Baby umependeza" Je umechangia sh ngapi au umenunua kipi? Wanaume mnaboa

Unakuta upo kwenye mahusiano na mwanaume,kazi yake kusifia unavyopendeza
Ukimuomba kitu fulani,kiasi fulani cha fedha danadana nyiiiingi,vuta subira
Ukipita au ukienda kwake au akikuita hotel fulani au ukipost picha*Masifa kibao*

Wanaume sifia mtu wako Kama umemuwezesha kupendeza,tunaona kinyaa kunisifia kupendeza huku hakuna ulichochangia kwenye urembo wangu au asilimia zako ni ndogo sana kwenye kunipendezesha
Unapata wapi nguvu za kumsifia mwanamke na hukuchangia chochote kwenye urembo huo? Ni aibu na mnaboa na mnakera
Msifie mwanamke uliyeajibika kumpendezesha kwa asilimia 100,tunajisikia raha sana na kupendwa

Kona ya Bwiru
Unauza nini haswa hadi uumie Me kutokukuhudumia?

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Kwani mrembo iwapo your Man has paid 50% na you paid the remaining 50% Kuna tatizo akikusifia.

Wakati mwingine shukuruni hata Kwa hiko kidogo ambacho mnapewa, mkikutana na Timu ya "Kuna hela naisikilizia" hupewi hata mia mbovu 😜🙌

Kuweni na Moyo wa shukrani Kwa Wanaume wanaojitoa kwaajili yenu
Babu! Mwanamke akikupenda atataka utimize malengo yako kwanza badala ya kutumia hela kwenye mambo yasiyo ya msingi kwake
Kama hupendwi jiandae kuwa ATM machine
 
Wajibu wa mwanaume siyo kukwepa majukumu,mpendezeshe msifie

Kama huwezi kujilisha na kujipendezesha, what more can you do in life au utaweza changia nini kwenye mahusiano na mtu zaidi ya sex.

Hizo traditional roles za mwanaume haziwezi kubadilika lakini kwa maisha ya sasa soko lipo tight. Hivyo watakiwa zaidi ya muonekano na mwili wako
 
Nitajitahidi watoto wangu wakike wasiwe na mtazamo huo wa kwamba wao ni ombaomba.
Huo ni mtazamo wa hovyo Sana hakuna binadamu ambae hawezi kujihudumia mwenyewe na uhusiano sio kazi ni kufurahi pamoja.

Kama uko kwenye uhusiano na mtazamo wako ni kupewa unaishi Dunia ya zamani Sana ya mababu zetu ambao wametuambukiza kwamba mwanamke hawezi chochote ni akae nyumbani asubiri mwanaume amuhudumie na ni lazima aolewe na akiwa na chochote basi tuamini kapewa au ana danga lenye hela.

Nawaheshimu wanawake na nitajitahidi wanangu wasiwe kundi la ombaomba kwamba kupendeza kwao kutokane na msaada kutoka kwa mwingine.

Awe mpenzi au rafiki hupaswi kuwa tegemezi kwake kiasi kwamba akikuacha ndio hupendezi tena wala hupati mahitaji yako mahusiano sio ajira ni kuhusiana na kufurahishana.
 
My life goals, nitamfundisha dear daughter kuwa yeye sio kundi maalum. Ni binadamu kamili ambaye hatakiwi kuwa tegemezi kwa basic needs kama mlo na muonekano. Kiufupi mwanaume ni patner na sio solution ya matatizo madogo kama hayo

Na huu sio msimamo wangu ila ni maisha waliyoishi bibi, shangazi na mama zangu. Kwa hiyo asitafute laana yao
Maisha yatambadilisha,
 
Back
Top Bottom