"Baby umependeza" Je umechangia sh ngapi au umenunua kipi? Wanaume mnaboa

Unauza nini haswa hadi uumie Me kutokukuhudumia?

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Babu! Mwanamke akikupenda atataka utimize malengo yako kwanza badala ya kutumia hela kwenye mambo yasiyo ya msingi kwake
Kama hupendwi jiandae kuwa ATM machine
 
Wajibu wa mwanaume siyo kukwepa majukumu,mpendezeshe msifie

Kama huwezi kujilisha na kujipendezesha, what more can you do in life au utaweza changia nini kwenye mahusiano na mtu zaidi ya sex.

Hizo traditional roles za mwanaume haziwezi kubadilika lakini kwa maisha ya sasa soko lipo tight. Hivyo watakiwa zaidi ya muonekano na mwili wako
 
Nitajitahidi watoto wangu wakike wasiwe na mtazamo huo wa kwamba wao ni ombaomba.
Huo ni mtazamo wa hovyo Sana hakuna binadamu ambae hawezi kujihudumia mwenyewe na uhusiano sio kazi ni kufurahi pamoja.

Kama uko kwenye uhusiano na mtazamo wako ni kupewa unaishi Dunia ya zamani Sana ya mababu zetu ambao wametuambukiza kwamba mwanamke hawezi chochote ni akae nyumbani asubiri mwanaume amuhudumie na ni lazima aolewe na akiwa na chochote basi tuamini kapewa au ana danga lenye hela.

Nawaheshimu wanawake na nitajitahidi wanangu wasiwe kundi la ombaomba kwamba kupendeza kwao kutokane na msaada kutoka kwa mwingine.

Awe mpenzi au rafiki hupaswi kuwa tegemezi kwake kiasi kwamba akikuacha ndio hupendezi tena wala hupati mahitaji yako mahusiano sio ajira ni kuhusiana na kufurahishana.
 
Maisha yatambadilisha,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…