Nilifuata ushauri wa Likud Nina watoa watoto wangu shule ya English Mediums.
Niliwatoa mwaka jana katikati. So mwaka huu mzima watoto wangu wamesoma Kayumba.
1. Kwa mwaka huu mzima pamoja na kumalizia kibanda changu na kununua kiwanja kingine,nimeweza kuhifadhi shilingi milioni 8 na uchafu.
2. Hili limewezekana kwa sababu nimewatoa watoto wangu shule ya English Medium.
Nilikuwa nasomesha watoto wa3. Mtoto mmoja kwa mwaka ada tu ni milioni mbili, bado hajaweka usafiri na vikorokocho vingine tuseme ukihesabu na hivyo inakuwa milioni 3 na ushee.
So kwa watoto watatu maana yake ningekuwa nimetoa milioni kumi halafu pia nisingekuwa na akiba yani sasa hivi ningekuwa naumiza kichwa ntapata wapi hela za kuwalia wanangu.
But :
1. Nimehamia kwangu. Watoto wangu wanaishi nyumbani kwababa yao. Nisinge wahamisha hadi muda huu ningekuwa sijajenga wala nisinge kuwa na kiwanja cha ziada wala hiyo milioni nane.
2. Nina kimilioni nane changu ambacho kufikia mwakani mwezi wa kumi na.mbili kwa mipango niliyo iweka itakuwa imezalisha mara kumi yake.
3. Watoto wangu wanasoma shule kifalme. Wanaenda kwa miguu umbali wa kama dakika kumi. Wanakula vizuri, wanalala pazuri, wanavaa vizuri, shuleni wana sare pea tano tano viatu pea tano tano mabegi pea 3 tatu kila mmoja.
Nawasimamia vizuri.
Wanafanya vizuri darasani.
Nimewawekea programme za kitaaluma : home tuition; English, Hesabu na Sayansi plus programme za kitaaluma kupitia kwenye Tv ya nchi 40+ ambayo pengine nisinge weza kuinunua kama wangesoma shule ya Em coz hela yote ingeishia kwenye ada.
Asante sana Likud.
Watanzania wenzangu wenye kipato cha kawaida fikirieni mara mbili. Wacheni kujistress na ada kwenye shule za EM wakati uwezo wenu ni wa kuunga unga.
Kusomea EM at least uwe na networth ya kuanzia walau milioni 150 plus.