Badala ya elimu bure, serikali igharamie chakula cha mchana kwa shule zote za sekondari za kutwa na shule za msingi

Mkoba wa Mama

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2021
Posts
280
Reaction score
173
Suala la lishe ni muhimu sana, lakini naona mpango wa chakula cha mchana kutolewa kwa wanafunzi inaendelea kubaki kuwa changamoto. Mtoto anatoka nyumbani saa 12/1 asubuhi anarudi saa 10/11 jioni ndio anapata chakula cha mchana, kwa tafsiri ya haraka haraka ni kwamba; watoto wa shule huwa wako kwenye mfungo wa Ramadhani na Kwaresima kwa kipindi chote cha masomo (siku 194 za mwaka).

Kwa hali hii watoto wengi wanadumaa (afya ya mwili na akili), inachangia kwa kiasi kikubwa watoto kuwa na uwezo wa chini wa kuelewa darasani na mwisho wa siku wanafeli, lakini pia inafikia hatua baadhi ya watoto kuichukia shule na kuacha masomo, pia tunaandaa taifa lisilojali kabisa kuhusu umuhimu wa lishe bora kwa mtoto.

Maoni yangu; serikali igharamie chakula cha mchana kwa shule zote za umma, ile pesa ya elimu bure ihamishiwe kwenye chakula tu, maana hiyo elimu bure bado wazazi huwa wanachangia michango mbalimbali zaidi hata ya ile ada iliyokua inatozwa mwanzo (elfu 20 kwa mwaka kwa shule za kata). La sivyo suala la lishe kwa watoto wa shule litabaki kama wimbo tu.
 
Nakubaliana na wewe.

Nashauri hela atayolipa mwanafunzi igharamikie mishahara ya walimu. Serikali igharamikie chakula na miundombinu ya shule. Hii itasaidia kuongeza mshahara wa mwalimu na kuongeza ajira za ualimu.
 
Hv hiyo elimu bure c ni ile 20000 kwa mwaka ya ada au kuna kingine hapo?
 
Nakubaliana na wewe.

Nashauri hela atayolipa mwanafunzi igharamikie mishahara ya walimu. Serikali igharamikie chakula na miundombinu ya shule. Hii itasaidia kuongeza mshahara wa mwalimu na kuongeza ajira za ualimu.
Wachakate kwa kweli, watoto wanateseka sana
 
Inawezekana kabisa! Kama serikali inaweza kutumia bajeti yake kwa mambo yasiyokuwa na tija (by CAG),inao uwezo wa kugharamia japo chakula cha kutwa kwa wanafunzi.
Lakini siyo kwa serikali hii ya Mafisadi na wala rushwa.
 
Suala la lishe ni muhimu sana, lakini naona mpango wa chakula cha mchana kutolewa kwa wanafunzi inaendelea kubaki kuwa changamoto. Mtoto anatoka nyumbani saa 12/1 asubuhi anarudi saa 10/11 jioni ndio anapata chakula cha mchana, kwa tafsiri ya haraka haraka ni kwamba; watoto wa shule huwa wako kwenye mfungo wa Ramadhani na Kwaresima kwa kipindi chote cha masomo (siku 194 za mwaka).

Kwa hali hii watoto wengi wanadumaa (afya ya mwili na akili), inachangia kwa kiasi kikubwa watoto kuwa na uwezo wa chini wa kuelewa darasani na mwisho wa siku wanafeli, lakini pia inafikia hatua baadhi ya watoto kuichukia shule na kuacha masomo, pia tunaandaa taifa lisilojali kabisa kuhusu umuhimu wa lishe bora kwa mtoto.

Maoni yangu; serikali igharamie chakula cha mchana kwa shule zote za umma, ile pesa ya elimu bure ihamishiwe kwenye chakula tu, maana hiyo elimu bure bado wazazi huwa wanachangia michango mbalimbali zaidi hata ya ile ada iliyokua inatozwa mwanzo (elfu 20 kwa mwaka kwa shule za kata). La sivyo suala la lishe kwa watoto wa shule litabaki kama wimbo tu.
Watoto watakuja kuzimia kwa kukosa chakula
 
Huwa nina ndoto siku nikianza kumiliki mkwanja wa maana, nitaenda kwenye shule niliyomazia elimu yangu ya msingi kisha nitawajengea frame za maduka(maana shule yenyewe iko town so ni eneo zuri kibiashara) ambayo ndio yatakuwa kutega uchumi cha shule hiyo hivyo basi shida na changamoto ndogo ndogo kama chakula cha wanafunzi, sijui ukarabati wa madarasa na miundo mbinu mingine hakutakuwa na haja ya walimu kuvutana mashati na wazazi wa wanafunzi, kwani mapato yatakayotokana na frame hizo nilizowajengea ndio yatatua chagamoto zote hizo.

Kwa kufanya hivyo naamini itaboast hata kiwango cha ufaulu, maana madogo kazi yao itakuwa ni kusoma tu.
 
Back
Top Bottom