Mkoba wa Mama
JF-Expert Member
- May 5, 2021
- 280
- 173
Nakubaliana na wewe.Suala la lishe ni muhimu sana, lakini naona mpango wa chakula cha mchana kutolewa kwa wanafunzi inaendelea kubaki kuwa changamoto. Mtoto anatoka nyumbani saa 12/1 asubuhi anarudi saa 10/11 jioni ndio anapata chakula cha mchana, kwa tafsiri ya haraka haraka ni kwamba; watoto wa shule huwa wako kwenye mfungo wa Ramadhani na Kwaresima kwa kipindi chote cha masomo (siku 194 za mwaka).
Kwa hali hii watoto wengi wanadumaa (afya ya mwili na akili), inachangia kwa kiasi kikubwa watoto kuwa na uwezo wa chini wa kuelewa darasani na mwisho wa siku wanafeli, lakini pia inafikia hatua baadhi ya watoto kuichukia shule na kuacha masomo, pia tunaandaa taifa lisilojali kabisa kuhusu umuhimu wa lishe bora kwa mtoto.
Maoni yangu; serikali igharamie chakula cha mchana kwa shule zote za umma, ile pesa ya elimu bure ihamishiwe kwenye chakula tu, maana hiyo elimu bure bado wazazi huwa wanachangia michango mbalimbali zaidi hata ya ile ada iliyokua inatozwa mwanzo (elfu 20 kwa mwaka kwa shule za kata). La sivyo suala la lishe kwa watoto wa shule litabaki kama wimbo tu.
Wachakate kwa kweli, watoto wanateseka sanaNakubaliana na wewe.
Nashauri hela atayolipa mwanafunzi igharamikie mishahara ya walimu. Serikali igharamikie chakula na miundombinu ya shule. Hii itasaidia kuongeza mshahara wa mwalimu na kuongeza ajira za ualimu.
Wanavyodai wao, ni pamoja na michango mingine yote serikali inagharamiaHv hiyo elimu bure c ni ile 20000 kwa mwaka ya ada au kuna kingine hapo?
Sidhani kama inafikia hata 50k hapoWanavyodai wao, ni pamoja na michango mingine yote serikali inagharamia
Vyovyote, lakini waangalie namna watoto wapate chakula, wachukue hata Tshs 100 katika kila malipo ya pango tunayolipia tukinunua LUKUSidhani kama inafikia hata 50k hapo
Yah upo sahihi.Vyovyote, lakini waangalie namna watoto wapate chakula, wachukue ha Tshs 100 katika kila malipo ya pango tunayolipia tukinunua LUKU
Watoto watakuja kuzimia kwa kukosa chakulaSuala la lishe ni muhimu sana, lakini naona mpango wa chakula cha mchana kutolewa kwa wanafunzi inaendelea kubaki kuwa changamoto. Mtoto anatoka nyumbani saa 12/1 asubuhi anarudi saa 10/11 jioni ndio anapata chakula cha mchana, kwa tafsiri ya haraka haraka ni kwamba; watoto wa shule huwa wako kwenye mfungo wa Ramadhani na Kwaresima kwa kipindi chote cha masomo (siku 194 za mwaka).