Badala ya kuwa Chama cha siasa wamegeuzwa "pressure group"..na wanafurahia...

Kama kungekuwa na chaguzi halali huenda hii hoja yako ingekuwa na maana zaidi ya hii nongwa uliyooandika hapa. Sasa maelezo mengi, ikifika wakati wa uchaguzi watu wapime matakwa ya wananchi linatokea kundi linajiita system linaamua nani awe kiongozi na sio wananchi! Inshort umeamua kuanika hasira yako hadharani badala ya uchambuzi kama ulivyotaka ionekane. Unataka kuonyesha kama kuna chama cha siasa fulani kinachojitambua, lakini uhalisia unakataa.
 
Huna lolote ww jamaa
Ndugu yako Mwabukusi njaa inamsumbua. Madeni ya huko mahakamani yamemjaa mpaka shingoni.

Aligombea ubunge akashindwa na Mwakibete, kesi zake zote zinamtokea puani.

Deni la shilingi milioni 80 lipo pale pale linamsubiri. Leo anafungua kesi yeye mwenyewe halafu anataka tumchangie!.

Haraka haraka video mnaiweka mitandaoni ili wakubwa huko Marekani na Ulaya waweze kumpatia pesa za uanaharakati.

Kazi mnayo kwani serikali inawaangalia tu, inajua itawabania sehemu gani.
 
Mzee huwa una uandishi wa bendera fuata upepo, wala huna lolote jipya. Umekaa kwenye uandishi wa habari toka uko kijana, na sasa uzee umekukutia humo humo. Waandishi mmekuwa mkipambana na sheria mbaya za vyombo vya habari, lakini hadi leo hakuna mabadiliko ya maana na sheria zinazidi kuwa mbovu. Kama uko serious na una mbinu sana, kipi kimekushinda ww na waandishi wenzako wa habari kubadili hizo sheria mbovu, ili tuseme ww au nyie kuna cha kuwaiga?
 
Ugumu wa afrika kupiga hatua unaanzia katika suala zima la hivi vyama vya siasa na pressure groups nani anayeziwezesha kupata mkate wa kila siku.

Leo Lissu anazunguka Kariakoo kutangaza ubaya wa DPW, ni demokrasia anayotumia inayompa uhuru huo.

Hao hao wanamfadhili Lissu mikutano yake ya hadhara ndio hao hao waliopiga picha na viongozi wa juu wa serikali wiki iliyopita baada ya serikali kupata pesa za EU.

Hizi ndizo siasa za afrika, kila taasisi inayojionyesha machoni mwa watu inao viongozi wanaopata ulaji wao sehemu moja wakiwa wamejifungia ndani ya vyumba na hawaonwi na wapita njia.
 

Kama kuweka video huku mitandaoni ni ili kupata fedha kwa wakubwa, mbona hata serikali yetu hizo ndio zake. Ama hujui ni kwa kiwango gani serikali yetu inajibebisha kuomba hela kwa wafadhili. Kama baba anaomba kwa wazungu, kipi kinakushangaza mtoto akienda kupewa hela na wakubwa?

Eti serikali inawaangalia tu, ukisema hivyo utadhani ni serikali ya maana. Kama ingekuwa ya maana kama unavyotaka ionekane, ingejitokeza kukiri kuwa imeshindwa kuendesha bandari sasa hadi inaitoa kwa wenye uwezo?
 
Huyo mwanasheria serikali inajua imkamate sehemu gani.

Suala la bandari linakaribia kumalizika, muda sio mrefu DPW wanafunga mitambo yao bandarini. Siasa nyingi za mitandaoni zisikudanganye.
 
Mkuu P, pamoja na kukubali kuwa ni mmoja wa wachangiaji hoja wazuri; lakini kwa hili nasita kuamini kama ni Mr. P ninaye mfahamu. Hivi kweli TZ kuna Uchaguzi wa Haki, kuna Tume ya Uchaguzi Huru, Kuna Mahakama Uhuru za kutoa haki kwenye mapingamizi ya Uchaguzi.
Ebu tuwe wakweli, Tz hakuna Uchaguzi Huru na wa Haki. Vyama vya upinzani vinakwenda kwenye Chaguzi kutimiza takwa la chama cha siasa na sio takwa la Chama cha Siasa kwa tafsiri sahihi ya Democracy.
 
Ng'ombe wako wengi sana nchi hii!
 
Huyo mwanasheria serikali inajua imkamate sehemu gani.

Suala la bandari linakaribia kumalizika, muda sio mrefu DPW wanafunga mitambo yao bandarini. Siasa nyingi za mitandaoni zisikudanganye.
Sio pa kumkamatia, sema inajua pa kumkomolea.

Ni kweli watafunga hiyo mitambo na kuanza kazi, lakini bila ridhaa yetu wananchi tulio wengi. Kama siasa za mitandaoni ni za kudanganya, ww unafanya nini humu?
 
Sio pa kumkamatia, sema inajua pa kumkomolea.

Ni kweli watafunga hiyo mitambo na kuanza kazi, lakini bila ridhaa yetu wananchi tulio wengi. Kama siasa za mitandaoni ni za kudanganya, ww unafanya nini humu?
Watanzania watakuwa ni wapuuzi sana iwapo wataugomea uwekezaji wenye lengo zuri la kuongeza tija ya bandari yetu kulinganisha na washindani wetu.

Watanzania watakuwa ni wapuuzi sana iwapo watakuwa hawana sababu yoyote ya maana ya kuupinga uwekezaji mkubwa kama wa DPW utakaoisaidia sekta nzima ya uchukuzi kwa kukubali kutumiwa na wenye pesa wa huko nje.

Lakini kizuri siku zote ni lazima kipigwe mawe, hata mradi wa maji wa bwawa la Mwalimu Nyerere ulipigwa vita lakini miezi michache ijayo hao walioupiga vita wataenda kimya kimya kufaidika nao kama vile wao sio walioupinga hapo kabla.
 
Nadhani ni sahihi lakini kwa nchi yetu hapa tanzania hizo kura utapata wapi wakati mihimili yote imeshikiliwa na serikali?

ndio maana hata wabunge wetu wanasimama zaidi upande wa serikali kuliko upande wa wananchi ambao inaaminika kuwa ndio huwaweka madarakani.

hii maana yake ni kwamba chama/serikali ina mamlaka makubwa kwa mbinu zozote zile ya kuamua hatma ya mbunge kuliko sanduku la kura/wananchi.
 
Kama umekosa la kuandika heri kunyamaza badala ya kutoa utopolo.

Sent from my Infinix X689F using JamiiForums mobile app
 
How can you hate a political party to such extent man..
Waandishi mkiambiwa njaa na kujipendekeza kupata ugali mnageuka mbogo..

Tuseme CDM haipo imekufa kabisa, unadhani nini kitatokea... embu ipende nchi yako wewe.
 
Huyu jamaa atakuwa wale waarabu wa Kayenze.

Toka nijiunge JF hii issue ya bandari ndiyo kaibebea bango kuliko kitu chochote kilichowahi kuwa topic nchini.
 
Hata mradi wa bomba la gas sifa zilikuwa ni hizi. Hilo bwawa la Nyerere zitazalishwa 2,115mw wakati wa porojo za gas ilikuwa zitazalishwa 5,000mw. Je kuna kipi cha kusifia hapo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…