Badili mtazamo wako kuhusu BMW

Hiyo ni general view kwa matakwa binafsi na vita ya ushindani wa biashara kimataifa... Bado mtu hataweza kunishawishi kwenye hizo tafiti za faults zinazompa mkorea alama nyingi kwakuwa mkorea ni mchanga sana na si maarufu kivile kwenye kuuza magari yake kimataifa
 
Kaka mshana mkorea sasaiv ni moto wa kuotea mbali,usisahau pia kwamba Hyundai/Kia ndiyo kampuni pekee ambayo inatengeneza magari kwa kutumia chuma chao wenyewe.Manufacturers wengine wananunua chuma kutengenezea magari wao wanazalisha wenyewe.

Pia shida nyingine hapo kwetu tz ni kwamba soko kubwa la magari ni ya zamani kuanzia miaka 8 na kuendelea,magari mapya ni machache sana lakini ya serikali ambayo ni Toyota na Nissan kidogo. Ukitizama soko la magari nchi zilizoendelea ushindani ni mkali sana kiasi kwamba Toyota hana free pass pamoja na akina BMW ,Mercedes nk.

Unakuta hakuna kampuni moja ambayo imeshika soko lote,kampuni inaweza hodhi segment flani tu ya soko,mfano pick up unakuta Toyota anaongoza,SUV kubwa Audi, hatchback BMW, ukija kwenye luxury sedans unakuta Mercedes na lexus wameshikana.

Hyundai/Kia wamekuja juu sana kwa sasa na pia wana luxury brand yao inaitwa Genesis ni moto wa kuotea mbali.Wao wanakula market share ya wakongwe kwa kuna na bidhaa reliable ambazo pia zina hold value mtu akinunua ikiwa mpya.Shida kubwa ya BMW nje ya reliability ni depreciation kaka, angalia beforward bei ya 7 series ya mwaka 2004 halafu fananisha na bei ya Lexus LS 500 sedan ya mwaka 2004 ushangae.
 
BMW n the like are Xcluziv beasts that why they are few... They are not for every one [emoji38] [emoji38] [emoji114] [emoji119]
 
Gari gani ambayo bmw inalingana na toyota brevis mtu kama wa singida atapata wapi spea labda awe anafata dar
Mbona Singida ndio njiapanda ya nchi mkuu. Ukishindwa kupata ukiwa Singida itakuwaje walioko Kigoma au nkasi, Sumbawanga??
 
Kuna kipindi tulikua tunaenda kijiji na Discover yale ya kizamani, likazingua njiani pale hedaru mafundi wa pale wakawa wanahangaika nalo siku 3 ndio ikapona,
Kichekesho sasa! ile siku tunaondoka mafundi wanamalizia gari yetu na walikua wa3 gari 1, mida ya saa 5 asubuhi jamaa kaja na Discover new model mpya inavujisha mafuta sana kibomba kilikatika, wote wakaacha gari yetu wakakimbilia ile iliyofika wakaingia chini wakachungulia wakakiona ila kukifikia mpaka wafungua kwa juu, walipofungua ule mfuniko wa juu ya injini wakaona namna ya kufungua mpaka wakifikie watashindwa kurudishia km ilivyo walianza kukimbia mmoja baada ya mwingine, wakamwambia jamaa akachukue chumba kabisa na demu alkua na mle maana wao hawezi mpaka fundi atoke moshi mjini au dar, jamaa alichoka lkn ikabidi akubali matokeo tuu.
 
[emoji23]
 
Kuna mtu ana alikuwa na bwm x5 ikafa feni ya a/c kubadilisha akaambiwa 1m...kuna siku nikarnda gereji nikqkuta bmw x5 nyingine imefunikeq turubai kuuliza tatizo nn nkaambiwa gear box imekufa bei yake bora ukanunua kluger mpya
aiseeh,, huyo mtu mlete hapa naye aongee lolote, maaana ntacheka sana najua[emoji23]
 
Maintainance ya hizo gari ni shida sana kwa raianwa kipato cha kawaida
 
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ hiyo yote kutaka kijiweka wa kipekee bora hizo watu wanaita mbolea kwakweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…