Ata mimi nipo tayari kupingana hapa 😀. Usidanganywe na ule msemo wao "German Engeneering". Engine za hawa jamaa ni pain in a**. Tofauti kabisa na Toyota. Engine za toyota zipo very simple, hazina complications and easy and cheap to maintain. BMW/MB, ni wazuri kwenye kukuwekea latest technology, lakini hizi latest technology zao, ndio chanzo cha matatizo ya gari. The whole car ipo controlled with electronics, complicated electronics, kikifeli kitu utajuta. Kuna kipindi niliona BMW 7 series kutoka beforward, yaani mpaka inafika bandarini ni dola $2500 apo ukalipe ushuru tu tena. Nikaona this is a nice car, alot of features, kisha kitu ukiingia ndani kama upo kwenye ndege ivi, hata crown ya 2007 haingii ndani kwa hii kitu. Nikaona ngoja nitizame reviews ya hii gari. Ukweli ni kama imesettiwa ivi ikifika kuanzia kilomita laki moja jitaarishe kuvunja benki. Maana matatizo hayaishi. Common issue ni transmission failure. Out of nowhere, unaweza ukadrive ukajikuta gear 3 haingii, wala moja hairudi, inakwama kwenye 2 au inacheza kwenye 1 na 2. Speed ya gari nayo haivuki 40kmhr kwa sababu haibadilishi tena gia. Maintainance yake hapo, ni new Transmission tu. Sio kwamba sijui ubadilishe solenoid, unanunua new transmission na uombe hio transamission nayo bado inayo mda mrefu wa kuishi.
Ama ukija kwa comfortability na features, wajerumani wapo juu. Lakini when it comes to engine reliability, narudia tena, Mjapan (naongea kuhusu toyota) aachwe tu.
Ukitaka kujua kama hawa jamaa wana complicate mambo, BMW betri wanaweka nyuma ya gari (kwenye buti) halafu mbele kwenye engine compartment wameweka vichuma vya negative and positive kwa ajili ya kujump start gari, thats German engeneering